Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Nimecheka sana mkuu 😂 😂 😂Usiwe unahangaika na walevi!Huwa wanalindwa na Mungu au mizim yao!
Mimi ukiniita hasta saa SITA kubeba mlevi siendi!mlevi hasta fisi au mchawi hamdhuru kabisa!!
Aliwahi kuja mmoja hapa kwangu midas ya saa tisa usiku akaingiza kichwa kwenye limfuko lenye chenga za mkaa akajifunika na kulala.aliamka asubuhi yupo safi TU na amejipaka mkaa kichwani nikaishia kucheka sana!
😀😀😀😀😀Nimecheka kama chiziiWeekend iliyoisha mida ya saa tatu usiku napigiwa simu "oya njoo umchukue rafiki yako huku yupo chakali!"
nikang'oka fasta mi nilikuwa sijashitua siku hiyo, kufika namkuta jamaa yupo nzwii haswa nikabeba weka kwenye bajaji huyo tukaanza safari ya kumpeleka ghetto kwake!.
tukiwa njiani jamaa akaanza kumtukana dereva bajaji kuwa anaenda kimama!, tukana mpk dereva bajaji akakasirika akatushusha hata nusu nauli hakutudai jamaa lilikuwa na matusi unaweza hata ukalia!.
kucheki safari bado ndefu, jamaa nae yupo chakali hawezi kutembea halafu tumeachwa sehemu mbovu usafiri unapita mmoja mmoja tena usiku huo vyombo vingi vinapita vimeshakodiwa!.
Dakika tano si nyingi mshikaji hali ikabadirika zaidi akalegea!, mara akaanza kutapika ktk kumuuliza kumbe alimix vinywaji!. haraka haraka nikawaza nifanye nini ktk hayo mazingira ili nimnusuru ndo nikakumbuka humu nilionaga mada inasema ati "Mkojo ni tiba!".
Na pia nikakumbuka wahenga husema mtu alielewa chakali ukimnywesha mkojo anakaa sawa!, hata sikuwaza sana nikamlaza jamaa chini akaniuliza unaenda wapi nikamuambia atulie!.
nikaenda dukani nikachukua chupa ndogo ya maji nakamwaga yale maji nikakojoleamo nikapata walau kojo nusu ya ile chupa!.
lkn kumbe mshikaji nimemuacha pale kumbe ananifatilia tu!.
Nilivyomfikia nikamuinua ile nataka nianze kumnywesha sijui nguvu alitolea wapi alilipiga banzi moja lile kopo nikasikia tu "waaaah" kopo likapeperuka mithiri ya karatasi likaenda kuangukia machakani!.
nilimtizama kwa tuo nikimshangaa!, jamaa likaanza kulalamika ati nataka nimnyweshe mkojo ili iweje..? ile hata sijaanza kumjibu akaanza matusi mazito mazito halafu aliponiuzi kabisa akawa anasema kwanza mimi naumwa UTI kali sana hivyo huo mkojo wangu ni kama ungeenda kummalizia tu!, aliongea sana kiasi kwamba kufananisha kitendo hicho ni sawa na swala la kigaidi!.
Namimi nikakasirika sasa kwanza nikamchapa banzi moja la uso, akatulia halafu kwa ukali nikamuambia "tulia hii elimu nimejifunza kwa wasomi!" .
jamaa nikaona amekuwa mpole nikaenda tena kuchukua lile kopo nikakuta mkojo wote umemwagika lakini kwa bahati nzuri nilikuwa na mkojo mwengine as emergency!, nikaweka tena mwengine ile nimemfikia tu ndugu nilikatwa mtama mmoja sijui hata nilikatwaje ubaya na ile barabara ilikuwa na vumbi nilioga vumbi mkojo kule ukamwagika tena!.
jamaa lilivyoona nimeanguka likainuka likaanza kukimbia!, namimi hasira zilikuwa zimenipanda sikumuacha nikamkimbiza nilivyomfikia ilikuwa ni mwendo wa kumchapa mabanzi tu ndo wakaja watu wakatuamua!.
Baada ya hapo kila mmoja akashika njia yake! ila nilighafirika sana halafu nanyinyi member angalieni elimu mnazozitoa tutakuja kuuana huku uraiani, hapa nishakorofishana na rafiki yangu kisa elimu zenu hizi, maana hata mimi mwenyewe baadae nilikaa chini nikajiweka kwenye hali ya mshikaji nikasema hata mimi nisingekubali!..
Hizi elimu zenu zipitiwe upya!.
Huruma ya kazi gani tupo kwenye tiba!"lakini kwa bahati nzuri nilikuwa na mkojo mwengine as emergency!, nikaweka tena mwengine"
Jua lilivyokuwa Kali hivi mtu anywe kojo 😂😂😂😂 na unasema kabisa eti reserve ilikuwepo hebu kuwa na huruma mkuu.