TANZIA Mmiliki na Mkurugenzi wa Bar ya Chako ni Chako jijini Dodoma, God Makoi, afariki dunia kwa ajali ya gari

TANZIA Mmiliki na Mkurugenzi wa Bar ya Chako ni Chako jijini Dodoma, God Makoi, afariki dunia kwa ajali ya gari

AmKATRINA

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2012
Posts
882
Reaction score
2,044
Pumzika mpambanaji Honorath Godfrey Makoi ulikuwa na ndoto nyingi sana.
Msiba uko nyumbani kwake Swaswa.

Alikuwa mmiliki wa Bar tatu maarufu jijini Dodoma.
1. Chako ni Chako
2. GM Sport & Bar (hii aliifunga ili kuifanyia marekebisho, na mpaka sasa iko kwenye matengenezo, so sad 😔😔)
3. The Evick lounge hii imefunguliwa mwaka huu mwanzoni na ina vibe si la kitoto.
4. Alikuwa ameanza matengenezo ya bar ingine Swaswa Mpamaa sema kafariki kabla hajaimalizia.

Mdogo sana, wa mwaka 89
Ajali inamaliza ndoto za vijana wengi Duniani.

Huwa anatembeaga na pesa kwenye gari, sijui kama zimesalimika

Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.

Ameacha mchumba mmoja (Maria) akiwa na ujauzito wa miezi 7 na ilikuwa wanatarajia kufunga ndoa January 2025, pamoja na watoto wa wawili wa kike 3 na 7 (alizaa na mwanamke mwingine ambae hakufunga nae ndoa)

Screenshot_20241103-165432.jpg

Screenshot_20241103-153119.jpg

Screenshot_20241103-160414.jpg

Coaster zaidi ya 20 tunausindikiza msiba pamoja na gari binafsi za wafanyakazi wake, ndugu zake, jamaa, marafiki pamoja na wafanyabiashara wenzake kutoka sehemu mbalimbali nchini.



Hapa tulikuwa Moshi, Hugo's bar kupumzika na kupata chochote, Tulifika Moshi saa 11 alfajiri, lakini kutokana na miiko ya kwao ilibidi tusubiri kupambazuke kabisa ili tuweze kupandisha juu Kibosho...mila za kwao.
Tulitoka na coaster kama 25 zote hizo kupandisha msibani


Hapa tumeshafika kwao Kibosho
Ilibidi tushuke kwenye magari ili tutembee pale juu kulia kwenye msiba maana watu walikuwa wengi sana na magari yalikuwa mengi na hayasogei kabisa.

Ila Wachaga 🙌🙌🙌 mbege ilikuwa ya kumwaga, bado bia bado nyama...aiseee.
Sema watu walilia sana...sana.
Vifo hivi, vina siri nyingi 🤐
Imagine God kaanza vurugu zote hizi za utajiri mwaka 2015

Primary 1999-2005
Secondary 2006-2009 (vipaji maalum)
Dereva wa waziri miaka 2, jeshi miaka 2.
Kapumzika mwaka mmoja kujipanga kimaisha....2014.
kuanza kushika pesa 2015 mpaka sasa 2024 anafariki
Vijana wengine mnakwama wapi?
 
Ajali zimekuwa zinakatisha maisha ya watu wengi sana ,hasa vijana umri wa kati na mkubwa kwa namna ya ghafla na kusikitisha sana, wanakuwa katika hali ya afya njema na mipango mingi, mara boom!
Apumzike kwa amani, Chako ni chako ni chimbo maarufu sana hata kwa ambao wanafika Dodoma kwa mara ya kwanza wanapenda kwenda " kupaona".
 
Back
Top Bottom