TANZIA Mmiliki wa baa maarufu Magomeni, Hussein Macheni ameaga dunia ghafla nyumbani kwake

Rogart Ngaillo

JF-Expert Member
Joined
Apr 27, 2013
Posts
908
Reaction score
1,911
Mmiliki wa baa maarufu ya Macheni iliyopo Magomeni jijini Dar es Salaam, Hussein Macheni amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla akiwa nyumbani kwake Magomeni.



Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ni kwamba Macheni alianguka ghafla majira ya saa 3 asubuhi na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo iligundulika kuwa tayari amefariki.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Muhimbili kusubiri taratibu nyingine. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. AMEN.

Chanzo : Global Publishers
 
Pole Kwa Ndugu, jamaa na marafiki. Nakumbuka nilikuwa nakatiza asubuhi nikiingia zangu skuli Azania, asubuhi saa moja nakuta bado kuna mtu kibao zinapata mambo. Kwa Macheni kweli enzi hiyo.

Pumzika Kwa Amani Hussein.
 

Mapema mno jamani hati zote bado zinasomeka jina lake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…