TANZIA Mmiliki wa baa maarufu Magomeni, Hussein Macheni ameaga dunia ghafla nyumbani kwake

TANZIA Mmiliki wa baa maarufu Magomeni, Hussein Macheni ameaga dunia ghafla nyumbani kwake

HM.jpg
 
Maisha ya mwanadamu hapa duniani ni sawa na msafiri aliyepumzika kivulini huku akivuta muda wa kuendelea na safari yake.....
Vifo vya wapendwa wetu ni moja ya matukio yenye kuumiza lakini vinatakiwa vitupe fundisho kuwa duniani tunapita...wanadamu yatupaswa tuishi kwa upendo kwani hakuna ajuaye muda wala saa ya kunyakuliwa kwake.........

KWA HERI MACHENI MUUMBA AKUHIFADHI UNAPOSTAHILI.....
 
Aliyekuwa mmiliki wa baa maarufu ya Macheni iliyopo Magomeni jijini Dar es
Salaam, Hussein Macheni amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla akiwa
nyumbani kwake Magomeni.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ni kwamba Macheni alianguka ghafla majira ya
saa 3 asubuhi na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo iligundulika kuwa
tayari amefariki.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Muhimbili kusubiri taratibu nyingine. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. AMEN.

Chanzo : Global Publishers
Uwiiiiue uwiiiiiiie yeuwiiiiiiiiiiiu jamani uwiiiiiiiiiie yeuwiiiiiii
 
Back
Top Bottom