TANZIA Mmiliki wa baa maarufu Magomeni, Hussein Macheni ameaga dunia ghafla nyumbani kwake

TANZIA Mmiliki wa baa maarufu Magomeni, Hussein Macheni ameaga dunia ghafla nyumbani kwake

HM.jpg
Kumbe ndio huyu nilikua simjui miaka yote
 
Aliyekuwa mmiliki wa baa maarufu ya Macheni iliyopo Magomeni jijini Dar es
Salaam, Hussein Macheni amefariki dunia leo baada ya kuanguka ghafla akiwa
nyumbani kwake Magomeni.

Kwa mujibu wa ndugu wa marehemu ni kwamba Macheni alianguka ghafla majira ya
saa 3 asubuhi na kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambapo iligundulika kuwa
tayari amefariki.

Mwili wa marehemu umehifadhiwa Muhimbili kusubiri taratibu nyingine. Mwenyezi Mungu Ailaze Roho ya Marehemu Mahali Pema Peponi. AMEN.

Chanzo : Global Publishers

Duh.....apumzike kwa amani..nilikuwa namfahamu kwa mbali...
 
Jana nilimuona Mbezi beach, nikawa najiuliza hii sura nimeiona wapi.
Baada ya dakika kama tano nikamkumbuka. Alikuwa anapiga monde akiwa na rafiki yake mishen town mmoja
aliyekuwa Mbunge pamoja na mabinti wawili. Maisha mafupi sana.

RIP Macheni
We hukuwa na ka binti huko. ...

Wanasemaga wanadam tunatembea na kifo duh
 
Back
Top Bottom