Mmiliki wa Gwambina: Bodi ya Ligi walikuwa wanataka pesa kwa nguvu, usipotoa lazima ushuke daraja

Mmiliki wa Gwambina: Bodi ya Ligi walikuwa wanataka pesa kwa nguvu, usipotoa lazima ushuke daraja

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
"Ligi ilikuwa ngumu kwa sababu ilipaswa tushuke na ikiwezekana tupotee kabisa Duniani, Viongozi wa Bodi ya Ligi walikuwa wanahitaji sana hela hata tulivyokuwa ligi kuu nasikitika kuongea haya lakini hakuna namna , huku chini kuna uozo kuna watu pale Bodi ya ligi wameukamata huu mpira kama mali yao, 2021 ligi ilikuwa ngumu kwa sababu ilikuwa ni maelekezo lazima Gwambina ashushwe daraja,

Watu wanataka pesa kwa nguvu , tusipotowa pesa lazima tushuke zaidi, sisi hatukuweza kutoa pesa sababu hatukuwa na pesa , haiwezekani mimi niwalishe wachezaji , niwatibu niwasafirishe na wewe kiongozi nikulipe , kumbe chuki ilianza kwenye mechi za Simba na Yanga walikuwa wanalazimisha mechi tucheze CCM Kirumba wakati sisi tuna uwanja wetu, ulikuwa ni mpango wa kuiba mapato"- Alexander Mnyeti

Mmiliki wa Klabu ya Gwambina na Mbunge wa Jimbo la Misungwi akielezea sababu za wao kujitoa kwenye mashindano yote nchini.

Chanzo: Clouds FM

========

MAJIBU YA SHIRIKISHO LA SOKA TANZANIA (TFF)

TFF.jpg
 
Viwanja vingi vilivyo fungiwa kama mnao vitumia hamkujipanga Kwa kutoa chochote mtaendelea ku umia.
Gharama za uendeshaji wa timu lazima zitaongezeka na karibu msimu mzima mnacheza ugenini au neutral ground.

Gwambina kuweni wavumilivu hata Uongozi huu wa Tff utapita, walikuwepo wakina Muhidini Ndolanga mpaka account na Anuani za FAT alitumia zake binafsi.
Muda ulivyofika waliondolewa.
 
Watu wanataka pesa kwa nguvu, tusipotowa pesa lazima tushuke zaidi, sisi hatukuweza kutoa pesa sababu hatukuwa na pesa.
 
Kwa hiyo wote wanaoshuka daraja wanakuwa hawajatoa hela!! mbona haimake sense let's assume wote watoe hela na uhalisia ni lzm kuna timu itashuka maana points zao ni ndogo hao bodi wanafanyaje ili wasishuke kwa hizo timu kutoa hela.

Huyu anataka kuhamisha magoli tu uwezo aliokuwa nao sasa haupo baada ya utawala ule kupita kwa hiyo project zake lzm zife tu.
 
Hao wanaoshuka Daraja walikuwa hawatoi pesa,je kama wote wangekuwa wanatoa pesa ina maana ligi kuu kungekuwa hakuna timu yoyote itashuka daraja?

Huyu mmiliki wa gwambina ni mpumbavu sana failure zako unatafuta huruma kwa watu.

Na nyie mabongo lala ya simba na yanga mtambue kuendesha timu sio jambo jepesi ooh mbona hatumuoni manzooki unadhani manzooki anaokotwa tu, ooh kwanini yanga hawajaweka kambi marekani..wakienda USA watatumia makaratasi?
 
Katika taasisi ya hovyo na iliyojaa ufisadi ni Tff..., Inafikirisha sana huyu Mwenyekiti wa bodi ya ligi anafanya kazi gani katika mpira. Inawezekanaje kiongozi mmoja kwenye taasisi moja akawa na vyeo zaidi ya kimoja na akafanya vizuri...!!, Wizara husika,Takukuru vichunguze hizi tuhuma.
 
Uyo Jamaa anazungumza ukweli, sio mara ya kwanza Kwa uwanja wa gwambina kufungwa.
Gwambina wakati wapo ligi kuu, Moja ya viwanja vilivyokua Bora kabisa ulikua uwanja wao lakini ulifungiwa na mara nyingi Ili uwanja ufunguliwe unahitajika kutoa chochote.
Kinacho mponza mmiliki ni kusema ukweli Hadharani ila watu walio kwenye mpira wa miguu wanaelewa ayo mambo sio mageni kwao.
Ndio maana Kuna viwanja vinafunguliwa baada ya kufungiwa ila vikichezewa mechi Moja kinaonekana kibovu.
 
Inawezekana madai yake yakawa na msingi, TFF imetawaliwa na wahuni wenye uhuni mwingi sana, hakuna anayejielewa asiyejua ukweli huu, japo najua kwa mabavu yao na kamati zao, watamfungia Mnyeti asijihusishe na mpira.
 
Brother kwanini useme mabavu unapaswa kuwa objective ili kuondoa element of bias hapa ni sheria ifanye kazi yake
 
Hao wanaoshuka Daraja walikuwa hawatoi pesa,je kama wote wangekuwa wanatoa pesa ina maana ligi kuu kungekuwa hakuna timu yoyote itashuka daraja?

Huyu mmiliki wa gwambina ni mpumbavu sana failure zako unatafuta huruma kwa watu.

Na nyie mabongo lala ya simba na yanga mtambue kuendesha timu sio jambo jepesi ooh mbona hatumuoni manzooki unadhani manzooki anaokotwa tu, ooh kwanini yanga hawajaweka kambi marekani..wakienda USA watatumia makaratasi?
Labda wangepandisha tu hata zifike 20 lakini wasishushe kwa sababu zimetoa hela......lahaula....
 
Back
Top Bottom