Mmiliki wa mabasi ya Super Sami atoweka, gari lake lachomwa moto Serengeti

View attachment 708766View attachment 708767
28870378_2061738970509399_5210459689955317991_n.jpg

View attachment 708768

Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah maarufu kama Super Sami au mmiliki wa mabasi ya Super Sami amefariki huku mwili wake ukiokotwa na wavuvi katika mto Ndabaka, Serengeti, ukiwa kwenye mfuko wa Sandarusi umefungwa pamoja na mawe.

Takribani wiki mbili zilizopita, Bwana Samson alikuwa hapatikani kwenye simu wala kujulikana alipo. Gari lake limekutwa eneo la Serengeti na limechomwa moto.

Taarifa inayofuta hapo chini ilikuwa ni kupatikana kwa gari lake Serengeti kabla ya kupatikana kwa mwili wake na kuthibitishwa kuwa amefariki.

============
=================

Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah ametoweka kwa zaidi wiki mbili sasa gari lake aina ya Toyota Landcruizer kukutwa likiwa limechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara.

Gari hilo lililokutwa likitumiwa na mfanyabiashara huyo ambaye ni mkazi wa Mwanza, lilikutwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara jana likiwa limeteketea kwa moto.

Ofisi habari wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa), Mustapha Mwalongo, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kuwa mfanyabiashara huyo licha ya gari lake kukutwa limeteketea moto, hawakukuta mabaki ya mwili wake.

"Gari lake limeteketea kweli lakini hatujabaini mwili kama na yeye alikuwa kwenye gari lile kwa sababu waliofika eneo la tukio hawajakuta mwili au mabaki ya mwili ya aina yeyote", alisema Mwalongo.

Alisema baada ya mmiliki huyo wa mabasi kutoweka tangu Machi Mosi, Kamati iliundwa ya kufuatilia sababu za kutoweka kwake na wapi alipo ambayo inashirikiana na familia.

"Kamati ilipopata taarifa kuwa kuna gari limeteketea kule Serengeti, walishirikiana na Jeshi la Polisi kwenda hadi eneo la tukio na kubaini kweli ni gari lake lakini hawajabaini kama alikuwepo mle wakati linachomwa", alisema Mwalongo.

Nahisi itakua ni ushindani wa kibiashara, ugomvi wa familia au uhasama na watu binafsi tofauti na biashara na familia. Mungu ailaze Roho ya marehemu mahala pema peponi amina.
 
View attachment 708766View attachment 708767
28870378_2061738970509399_5210459689955317991_n.jpg

View attachment 708768

Mmiliki wa mabasi ya Super Sami, Samson Josiah ametoweka kwa zaidi wiki mbili sasa gari lake aina ya Toyota Landcruizer kukutwa likiwa limechomwa moto katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara.

Gari hilo lililokutwa likitumiwa na mfanyabiashara huyo ambaye ni mkazi wa Mwanza, lilikutwa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti mkoani Mara jana likiwa limeteketea kwa moto.

Ofisi habari wa Chama cha Wamiliki wa Mabasi (Taboa), Mustapha Mwalongo, aliiambia Nipashe kwa njia ya simu kuwa mfanyabiashara huyo licha ya gari lake kukutwa limeteketea moto, hawakukuta mabaki ya mwili wake.

"Gari lake limeteketea kweli lakini hatujabaini mwili kama na yeye alikuwa kwenye gari lile kwa sababu waliofika eneo la tukio hawajakuta mwili au mabaki ya mwili ya aina yeyote", alisema Mwalongo.

Alisema baada ya mmiliki huyo wa mabasi kutoweka tangu Machi Mosi, Kamati iliundwa ya kufuatilia sababu za kutoweka kwake na wapi alipo ambayo inashirikiana na familia.

"Kamati ilipopata taarifa kuwa kuna gari limeteketea kule Serengeti, walishirikiana na Jeshi la Polisi kwenda hadi eneo la tukio na kubaini kweli ni gari lake lakini hawajabaini kama alikuwepo mle wakati linachomwa", alisema Mwalongo.
Halafu hiyo inaonekana kabisa ni Nissan patrol nyie mnaita Toyota landcruiser?
 
Wamemuwa kikatili sana
Ngoja tusubiri uchunguzi Wa polisi utasemaje!

Ova
 
Mambo haya yalianza kidogo kidogo lakini kwa sasa yanataka kuwa sehemu ya maisha yetu
 
Tz bado tuko nyuma sana kwenye Forensic Investigations. Tumerely kwenye uchunguzi wa kuhoji mashuhuda na kupekua simu tu.
 
Back
Top Bottom