Waheshimiwa
Na wataalum wote
wa mambo ya mahusiano,mapenzi na urafiki
naombakuuliza ni nini au ni kitu gani
Kinacho mfanya mtu kuoa au kuolewe?
Je ndoa zote ni matokeo ya upendo wa hali ya juu??
Ni hayoo tu
Ps. ..maoni yote yana karibishwa
asanteni
AD
kwa mimi ninavyofikiri, ndoa ni njia aliyoiweka Mungu, kwa wapenzi kuhalalisha mahusiano yao.
Hivyo basi, hao wanandoa ni lazima wawajibike (wawe responsible) na maamuzi yao.
Labda tujiulize UPENDO ni nini kwenye masuala ya ndoa?
Mie nafikiri Upendo ni kitu ambacho kinakua (grow)! Kuna ndoa nyingi tu, wanandoa wanazidi kupendana kadiri miaka inavyozidi kwenda, kwa sababu wanaanza kugundua wajibu wao kwenye ndoa, na pia kumuelewa partner wake.
Wengi siku hizi wanaingia kwenye ndoa bila kujua wajibu (responsibilities) wao wanapokuwa kwenye ndoa. Yaani ndoa inaendeshwa kwa hisia (feelings) zaidi kuliko reality, na hii ni mbaya sana, kwa sababu hizo feelings zikupungia, na ndoa iko hatari.
Kwa hiyo msingi wa ndoa upo kwenye kuwajibika kwa mwanandoa kwa mwingine..Kama hujui uwajibikaje ni bora ujifunze ndio uende huko. Pia ikumbukwe kuwa watu hatufanani,hivyo huwezi ku-kopi na ku-pesti mapenzi yako uliyokuwa unampa fulani, ukafikiri yatakuwa sawa kwa mtu mwingine.
Kikubwa pia ni kumshirikisha Mungu. wakati ukifika, utaona tu mambo yanaenda sawa, wala hautumii nguvu nyingi kuingia kwenye ndoa. Ndoa haitakiwi kulazimishwa sana kama mtu hayuko tayari kuwajibika