Mmoja auawa kwa kisu kwenye Mabishano ya Simba Vs Yanga Mbozi-Songwe

Mmoja auawa kwa kisu kwenye Mabishano ya Simba Vs Yanga Mbozi-Songwe

TAARIFA KWA UMMA
MMOJA AUAWA KWA KISU BAADA YA MABISHANO YA SIMBA NA YANGA - MBOZI-SONGWE
​
Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa taarifa ya tukio la mauaji lililotokea mnamo tarehe 16 mwezi wa 9 mwaka 2025 saa 12:50 jioni katika Kitongoji cha Ululu, Kijiji na Kata ya Idiwili, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe.

Katika tukio hilo, Evaristo Zabroni Mwambogolo, mwenye umri wa miaka 28, Mkulima Mkazi wa Ululu Wilaya ya Mbozi alichomwa kisu kifuani, eneo la moyo, na mtu anayefahamika kwa jina la Exavery Jamsoni Mwaweza, baada ya mabishano ya mpira wa miguu kati ya timu za Simba na Yanga.

Marehemu alijeruhiwa vibaya na alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa kwenye Zahanati ya Iyula iliyopo Wilaya ya Mbozi kwa ajili ya matibabu.

Uchunguzi wa awali, umeonyesha chanzo cha tukio hilo ni ushabiki wa mpira wa timu ya Simba na Yanga kati ya marehemu na mtuhumiwa, ambapo mtuhumiwa alitumia kisu alichokuwa nacho wakati wa ugomvi huo na mara baada ya kutenda kosa hilo, alitoroka kusikojulikana.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linaendelea na msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa huyo ili akamatwe na aweze kuhukumiwa kwa mujibu wa Sheria.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa wito kwa wananchi kuepuka kujichukulia sheria mkononi, na kutojihusisha na vitendo vya vurugu vinavyoweza kusababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na upotevu wa maisha, na linawaita kuendelea kudumisha amani, mshikamano na utulivu, hasa wakati wa mijadala au mabishano ya kawaida, ikiwemo michezo.​
ujinga mtupu🚮🚮
 
17 Septemba 2025

TAARIFA KWA UMMA

MMOJA AUAWA KWA KISU BAADA YA MABISHANO YA SIMBA NA YANGA- MBOZI-SONGWE

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa taarifa ya tukio la mauaji lililotokea mnamo tarehe 16 mwezi wa 9 mwaka 2025 saa 12:50 jioni katika kitongoji cha Ululu, kijiji na kata ya Idiwili, Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe.

Katika tukio hilo, Evaristo Zabroni Mwambogolo, mwenye umri wa miaka 28, Mkulima Mkazi wa Ululu Wilaya ya Mbozi alichomwa kisu kifuani, eneo la moyo, na mtu anayefahamika kwa jina la Exavery Jamsoni Mwaweza, baada ya mabishano ya mpira wa miguu kati ya timu za Simba na Yanga.

Marehemu alijeruhiwa vibaya na alifariki dunia akiwa njiani akipelekwa kwenye Zahanati ya lyula iliyopo Wilaya ya Mbozi kwa ajili ya matibabu.

Uchunguzi wa awali, umeonesha chanzo cha tukio hilo ni ushabiki wa mpira wa timu ya Simba na Yanga kati ya marehemu na mtuhumiwa, ambapo mtuhumiwa alitumia kisu alichokuwa nacho wakati wa ugomvi huo na mara baada ya kutenda kosa hilo, alitoroka kusikojulikana.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linaendelea na msako mkali wa kumtafuta mtuhumiwa huyo ili akamatwe na aweze kuhukumiwa kwa mujibu wa Sheria.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Songwe linatoa wito kwa wananchi kuepuka kujichukulia sheria mkononi, na kutojihusisha na vitendo vya vurugu vinavyoweza kusababisha madhara makubwa, ikiwa ni pamoja na upotevu wa maisha, na linawataka kuendelee kudumisha amani, mshikamano na utulivu, hasa wakati wa mijadala au mabishano ya kawaida, ikiwemo michezo.
 

Attachments

  • 3723.jpg
    3723.jpg
    442.6 KB · Views: 17
Ukiwa shabiki wa simba na Yanga ni lazima uwe na matatizo ya akili
 
Kwa akili hizi ndio wanataka kufanya jambo tarehe 29 Octoba?
 
Back
Top Bottom