Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Hawa UWT wamekuwa wakimaliza wenyewe kwa wenyewe, sijui huwa wanazungukana?
 
Bodaboda zitatumaliza!!! Kesho utasikia pkpk haziruhusiwi!! Kwa amri ya Ikulu....
 
Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, viti kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Nani yuko salama?

Kawaida kwa usalama wa taifa kuuwawa unapoenda kinyume na wakubwa
 
Mambo ya kuchukua wake za watu mabaya sana. Hata hivyo serikali iimarishe ulinzi dhidi ya raia wake, maana sheria za kudeal na wagoni zipo.
 
Na ukiangalia habar kama hz magezet hawez kutoa zaid yaTanzania daima tu!!
 
Usalama wa Taifa ishu zao ni nyingi mno, unaweza kuona ameuwawa kwa sababu ya Usalama wa Taifa.!

Mkuu.

Hii nayo kali! Sasa hao usalama wa Taifa kama ndio wenyewe, hawana namna nyingine ya kulinda usalama wa Taifa mpaka wamuue mwana usalama wa Taifa mwenzao?!
 
Back
Top Bottom