Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni watu wa usalama wamemmaliza...Kuna taarifa nyeti nikiwa tayari ntaziweka hapa
Usisahau mkuu kutudonelea hata juu juu.Ni watu wa usalama wamemmaliza...Kuna taarifa nyeti nikiwa tayari ntaziweka hapa
Maelezo yako hayaonyeshi kama ameuawa kinyama...
Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.
"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.
Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.
Mytake:
Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, viti kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Nani yuko salama?
Maelezo yako hayaonyeshi kama ameuawa kinyama...
Usalama wa Taifa ishu zao ni nyingi mno, unaweza kuona ameuwawa kwa sababu ya Usalama wa Taifa.!
Kuna chochote unakijua, au kila kitu unachukulia kiccm ccm.Mambo ya kuchukua wake za watu mabaya sana. Hata hivyo serikali iimarishe ulinzi dhidi ya raia wake, maana sheria za kudeal na wagoni zipo.