Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mambo ya kuchukua wake za
watu mabaya sana. Hata hivyo serikali iimarishe ulinzi dhidi ya raia
wake, maana sheria za kudeal na wagoni zipo.

Inaonekana unadata nyingi mkuu hebu zimwage hapa kwa maslah ya wanajamvi na tutasikitika sana ikiwa ni shemeji yetu ndie aliyechukuliwa na marehemu hakika hatastahili R.i.p

BACK TANGANYIKA
 
Maelezo yako hayaonyeshi kama ameuawa kinyama...

Huenda ulisoma kwa kudona, soma tena katikati ya mistari "...Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari..."

"...Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake..."

"...Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani..."

Haya yanatoka kwenye bandiko ulililo kwisha soma; Kama hayaonyemi uuwaji au tendo la kinyama basi unyama utakuwa na defitions nyingi sana!
 
Apumnzike kwa amani.


Sent from my iPhone using JamiiForums app.
 
Habari ndio hiyo ...Mke wa mtu ni sumu.

Wewe ndiye mume wa huyo mke?

Mke wako ana uhusiano gani na briefcase uliyopora?

Kwa nini hukumvizia gesti akiwa na mkeo? Au usingeipata briefcase?
 
Hawa jamaa kuua kwao sio issue kabisa mfano mama Clinton aliwahi kuwa na affair na jamaa wa usalama ambae alikuwa na personal details nyingi sana za Clinton activities na familia yake kabla ya kuwa raisi.

Wakati wa uchaguzi jamaa akataka kuanza kumchafua CIA kwakuwa walishaamua ndio next president there was no other choice but dude had to die, tells you how little provocation can end ones life.

Sasa huyu ndugu yetu sijui kawakosea nini huko juu, hila naona kama ni tukio la kijambazi tu hivi watu na mbinu zao zote wakaue mchana kweupe, uneless labda kwenye briefcase alikuwa kachukua nyaraka muhimu sana au labda majambazi walijua kuna kichele sikuhizi wafanyakazi wa benki nao si wanatonya navyosikia.

Either way ni hatari sana kama watu wanaweza uwawa mchana kweupe maana yake ni kwamba response team is very slow na hawa jamaa jeshi la polisi nao siku hizi wanapokea kichele cha nguvu tu na enough fines za barabarani to improve their response teams. Haya ni matukio ya aibu kwa jeshi la polisi. Kwakuwa atuna utamaduni kwa kufukuzana kazi for poor performances jamani ni bora wenye mahela yenu muwe waangalifu mnapoenda kutoa mahela mengi, embu kuwe na utaratibu wa discreet procedures maana njaa iliyopo inaondoa maadili na utu wetu katika jamii.
 
Hiyo hit squad imekaa ki "Mossad" zaidi.Assasination kwa piki piki ni common sana kwa jamaa wale na "wanafunzi wake" Inavyoonekana ni jamaa alitaka kutoroka na nyaraka za siri wakaamua wammalize.Tough times tough measures
 
Mambo ya kuchukua wake za watu mabaya sana. Hata hivyo serikali iimarishe ulinzi dhidi ya raia wake, maana sheria za kudeal na wagoni zipo.

Kwa hiyo ile Briefcase ndio ilikuwa na yule Mke wa watu? Unaposema serikali iimarishe ulinzi wa raia wake je hiyo serikali ni nani na huyu aliyeuawa si mmoja wa hiyo Serikali kama yeye ameuawa hao raia watalindwaje?
 
Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?

wamemuhisi ni INFORMER na wamemuua
 
Mambo ya kuchukua wake za watu mabaya sana. Hata hivyo serikali iimarishe ulinzi dhidi ya raia wake, maana sheria za kudeal na wagoni zipo.
wewe utakuwa ni product ya ugoni. Acha kufanya conclusion zako kama issue huijui.
 
Kwa hiyo ile Briefcase ndio ilikuwa na yule Mke wa watu? Unaposema serikali iimarishe ulinzi wa raia wake je hiyo serikali ni nani na huyu aliyeuawa si mmoja wa hiyo Serikali kama yeye ameuawa hao raia watalindwaje?

Mimi nimeeleza ninachokijua. Hayo mengine ni porojo tu.
 
Ni watu wa usalama wamemmaliza...Kuna taarifa nyeti nikiwa tayari ntaziweka hapa

Mkuu una-beep eeeh.. Utapigiwa soon.. jamaa wana roho ya kutu.. wanajitafuna hata wenyewe kwa wenyewe..
 
Si ndiyo yule mwenye Chilakale Resort pale mkoani Morogoro?Na Mbena Malumbi ni nani?Hizi habari zinanichanganya sana.So Mzeru Silvanus na Mbena Malumbi ni mtu mmoja.
 
Back
Top Bottom