Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa wa Marekani aliuawa kwa sumu iliyowekwa kwenye Toilet Paper na Maafisa wa Kitengo cha kupambana na Ugaidi kilichomo ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa baada ya kuonesha kutokujiamini kwenye Maamuzi ya kulinda Usalama wa Wamarekani. US Intelligence believe 'Security and Safety of the Nation Cannot be Compromised just for the sake of adhere the so called 'Bill of Human Right'
hiyo taarifa ilikuwa dis-classified lini? au unabeba propaganda za taasisi dhidi ya watendaji wake wasizisaliti? au unataka kutuambia mwakyembe na mwandosya walishughulikiwa in the same style
 
https://www.jamiiforums.com/habari-...ulu-na-ujenzi-wa-majumba-huko-morogoro-2.html


Ni mtendaji wa ikulu kwa jina Mbena malumbi anafanya kufuru huko morogoro maeneo ya bigwa katika barabara ya zamani ya dar-moro kutokea mjini moro.

Yasemwayo na wananchi wa huko ni kuwa watu wananunuliwa kwa hela yeyote ile unataja wewe wakita enao lako na kukuhamisha hata kama una makazi tayari.

Washajenga hotel kando ya mto inaitwa Chilakale resort na live band yao ni hali ya juu sana.

Pia kuna ujenzi unaendelea kando ya huo mto mpaka kwenye milima ya uluguru majengo yanainuka kama uyoga na wananchi wakizidi kununuliwa kila kukucha.

Niliuliza nani ndio mhusika wa haya yote anatajwa huyo mtendaji wa ikulu.

Naomba kuuliza wanajamvi mwenye taarifa kuhusu huyu mtendaji wa ikulu na utajiri wa kutisha kama huu kaupata wapi ama kuna watu nyuma yake.

Hifadhi ya mlima Uluguru karibia yote washaichukua kwa mida ya usiku unaona umeme ukuwaka mlimani wakati huku wengine kuna mgao.

Naomba tasaidiane mwenye taarifa rasmi kuhusu huyu afisa wa ikulu atujuze.

Source ni mimi mwenyewe mkazi wa Moro. Naomba radhi kama sikufuata utaratibu wa uandishi.




 
mkurugenzi wa usalama wa taifa wa marekani aliuawa kwa sumu iliyowekwa kwenye toilet paper na maafisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi kilichomo ndani ya idara ya usalama wa taifa baada ya kuonesha kutokujiamini kwenye maamuzi ya kulinda usalama wa wamarekani. Us intelligence believe 'security and safety of the nation cannot be compromised just for the sake of adhere the so called 'bill of human right'

tofautisha maslahi ya taifa kwaajili ya umma na maslahi ya wachache walio tayari kwa lolote ili tu hii keki waigawane wao.
 
"jana mida ya jioni majambaz yasiyofahamika yalimvamia bwana Mzeru na kumnyofoa moyo kwa kutumia kisu butu, yakampofoa macho, yakamwagia maji ya moto halafu yakamnyonyoa nywele zote kisha yakamtupa mtaroni na kumshindilia na jiwe lenye kilo 55" nadhani nimekufurahisha kwa maelezo hayo ya kinyama. (una roho ngumu wewe)

Mkuu nimecheka sana, na hasa hapo mwisho ulipohitimisha kwamba jamaa ana roho ngumu!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app.
 
Ile NCHI yenye AMANI iko wapi?Wengi wakiwa na njaa siku zote hakuna AMANI.Na hii inawezekana pia wamelizana pesa huko huko watokako.Vinginevyo siri yao.
 
Kwa namna yoyote mauaji hayawezi kuitwa ya kinyama. Mauaji ya kinyama mtu hana shingo, kakatwa kiuno vipande viwili huyu kauawa tu. Tunangija taarifa zaidi, jf kuna mambo!
 
Basi ameuawa kibinadamu... Inside job.

Kawaida kwa usalama wa taifa kuuwawa unapoenda kinyume na wakubwa

Unataka kuniambia UWT ndio weupe kiasi hiki kiasi wakitaka kuuana wenyewe kwa wenyewe mpaka wakasubiriane barabarani?

Tuache utani jamani, mimi naamini kuna kitu kingine na sio UWT, maana naamini wanakili zaidi ya hii, kwanini wasimpumzishe kwa amani tu ana akajifia kimyakimyaa kuliko kuja barabrani na fujo zote hizo.
 
Kwa namna yoyote mauaji hayawezi kuitwa ya kinyama. Mauaji ya kinyama mtu hana shingo, kakatwa kiuno vipande viwili huyu kauawa tu. Tunangija taarifa zaidi, jf kuna mambo!

Kwahiyo kushindiliwa risasi kama mnyama pori siyo kuuawa kinyama?Kwahiyo walimuua kwa starehe au vipi?
 
Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha.
Hao Tanzania Daima wamejuaje kama yeye ni afisa mwandamizi wa TISS?
 
Inaelekea mmesahau mauaji ya Imran Kombe...ndio wanavyokufa hao watu wa Usalama
 
Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?


Na cha kusikitisha zaidi... HIZO pikipiki unakuta ndio CCM WANAZIITA BODABODA... Wanazileta toka CHINA halafu wanawagawia VIJANA bila hata kufuatilia historia zao... ISIPOKUWA TU WAKIIMBA CCM kwa HASIRA NGUVU na UZANDIKI hapo CCM -- NAPE NNAUYE na KINANA wanawapa hizo PIKIPIKI...

Kwahiyo CCM kweli hawajui au wanajua SILAHA wanazozigawa NCHINI kwa VIJANA wa CCM BODABODA ndio hizo hizo zitatumika pia kuwashambulia wao NDANI ya CCM...

HAKUNA CHOCHOTE cha BURE kisichokuwa na DHIHAKA...
 
kwani maafisa usalama hawawezi kuuawa na majambazi? Si watu tu wa kawaida?
 


Na cha kusikitisha zaidi... HIZO pikipiki unakuta ndio CCM WANAZIITA BODABODA... Wanazileta toka CHINA halafu wanawagawia VIJANA bila hata kufuatilia historia zao... ISIPOKUWA TU WAKIIMBA CCM kwa HASIRA NGUVU na UZANDIKI hapo CCM -- NAPE NNAUYE na KINANA wanawapa hizo PIKIPIKI...

Kwahiyo CCM kweli hawajui au wanajua SILAHA wanazozigawa NCHINI kwa VIJANA wa CCM BODABODA ndio hizo hizo zitatumika pia kuwashambulia wao NDANI ya CCM...

HAKUNA CHOCHOTE cha BURE kisichokuwa na DHIHAKA...

Mkuu, ni chadema ndio waligawa pikipiki ambazo zinatumiwa na majambazi
 
Back
Top Bottom