Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.

"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.

Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.

Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.

Mytake:

Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?

R.I.P Mzeru

 
Bodaboda zitatumaliza!!! Kesho utasikia pkpk haziruhusiwi!! Kwa amri ya Ikulu....

hivi umejitoa fahamu au hujui kweli,
kimsingi hapo atakuwa amekiuka miko yao na wao ndio waliomuua full stop!
 
du sad news na kifo chenye maswali mengi alikuwa msaliti au anatetea taifa au alfanya ishu nje ya uwt na wauaji n nje ya uwt
 
alipostukia kua kuna watu wanamfuatilia baada ya kupata mzigo pale uwanja wa ndege,akaamua kutaka kutoroka kwa gari yake, sasa wakati anatoka,foleni ya kuingia nyerere road ndio iliharibu,katika harakati za kujiokoa akatanua,bahati mbaya gari ikakwama pembezoni mwa barabara katika kamtaro,hapo ndio jamaa waliokua wanamfuatilia na boxer wakapata nafasi ya kumfuata katika gari na kumchapa risasi na kisha kutokomea na briefcase ambayo ndani yasemekana kulikua na hela nyingi na sembe.

Ukweli ni kwamba Mzeru alikuwa ndiye mshika fungu la operations na hata overseas missions.Ni kweli amewekeza kwenye miradi mingi.Lakini si kweli kwamba alikuwa kitengo cha madawa ya kulevya.Kwa nature ya kazi yake hapo idarani na mfumo wa fedha ulivyo ni dhahiri alikuwa na ukwasi wa kutosha.Huyo ameuzwa na mtu wake wa karibu.
 
Hawa jamaa kuua kwao sio issue kabisa mfano mama Clinton aliwahi kuwa na affair na jamaa wa usalama ambae alikuwa na personal details nyingi sana za Clinton activities na familia yake kabla ya kuwa raisi.

Wakati wa uchaguzi jamaa akataka kuanza kumchafua CIA kwakuwa walishaamua ndio next president there was no other choice but dude had to die, tells you how little provocation can end ones life.



TUPIA REFERENCE UTUAMINISHE
 
Hawa watu hawachelewi kusema Intelegensia ya Police imeona CHADEMA wanahusika, kwani walitumia pikipiki za CDM M4C kutoka china. Hapo Kova atapigiwa makofi na mambo yanaishia hapo kwenye uchunguzi.
 
Ukweli ni kwamba Mzeru alikuwa ndiye mshika fungu la operations na hata overseas missions.Ni kweli amewekeza kwenye miradi mingi.Lakini si kweli kwamba alikuwa kitengo cha madawa ya kulevya.Kwa nature ya kazi yake hapo idarani na mfumo wa fedha ulivyo ni dhahiri alikuwa na ukwasi wa kutosha.Huyo ameuzwa na mtu wake wa karibu.
Kwa kifupi tunaweza kusema alikuwa kibaka wa mali za uma?
 
Jamaa atakuwa ametofautiana na wakubwa kuhusu muundo wa serikali. labda anataka muungano wa shirikisho wenye ukakasi kwa watawala tutasikia mengi. pumzika panapostahili bwana afisaaaa
 
nkongu ndasu;

Angalia kichwa cha thread ndipo uchangie. Askari wa Usalama wa Taifa ameuawa kikatili kwa kupigwa risasi, wewe unakuja na ngonjera za TANZANIA ni nchi ya amani na utulivu! Kweli? You must be really joking. Maybe you're a day dreamer! Amani na Utulivu wa nchi ya Tanzania uliondoka na waasisi wa Taifa hili Mwalimu J.K.Nyerere na Sheikh Abeid Amani Karume!

Tumeanza kushuhudia mauaji ya Kisiasa Tanzania kwa mara ya kwanza kule Pemba mwaka 2001 walipouawa wafuasi wa CUF 21 waiokuwa wakiandamana kupinga matokeo ya Urais Zanzibar kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2000 baada ya CUF kudhulumiwa ushindi na CCM chini ya Ben Mkapa.Hii ilikuwa miaka 2 tu baada ya Kifo cha Baba wa Taifa.Tangu hapo nchi imeingia kwenye laana ya mauaji ya Wanasiasa, Wanausalama na Raia pia.

Kama Raia anaweza kuuawa kwa kuchinjwa kama kuku au kuteswa kwa kunyofolewa macho,kucha na meno na Serikali hiyo hiyo, unashangaa nini katika mazingira hayohayo Raia nao wanapoamua kulipiza kisasi???

Ukweli ni kwamba CCM nchi imewashinda na tutaendelea kushuhudia mauaji kama haya kila kukicha. Dawa iliyobakia kwa sasa ni kupigania Katiba mpya na baadaye kuing'oa serikali dhalimu ya CCM ili kurudisha AMAN na UTULIVI kama ulivoachwa na waasisi wetu.
Hivi mtu anayeua kwa kupiga risasi na kupora unasema kuwa kalipiza kisasi? Hakika umevurugwa mkuu
 
Jamaa atakuwa ametofautiana na wakubwa kuhusu muundo wa serikali. labda anataka muungano wa shirikisho wenye ukakasi kwa watawala tutasikia mengi. pumzika panapostahili bwana afisaaaa
Mkuu, mtabaki na labda tu. na hii inadhihirisha ni kwa namna gani chombo chetu hiki kinafanya kazi kwa weledi mkubwa sana
 
Kigogo wa Usalama wa Taifa MH AMA KIGOGO Mzelu auliwa kwa risasi juzi maeneo ya Airport alipokua safarini akielekea Morogoro kibiashara..akiwa katika foleni maeneo ya Airport watu wasojulikana waliokua kwenye pikipiki walishuka na kumuua

Mh ama Kigogo Mzito huyu ajulikanae kwa jina la Mzeru alikua akiishi tabata kimanga maeneo ya chama ndani ndani kidogo na alikua akimiliki mahekalu yake maeneo ya chanika....watu wapo msibani wakiwemo majirani..ndugu na wakubwa wa usalama wa taifa pamoja na vigogo wengine wa serikali ya Jamhuri ya Tanzania wakiwa wamesindikizwa na ving"ora

Source..NEXT OF KIN

Poleni sana wafiwa.....M Mungu awape nguvu na subira kwa kipindi hichi kigumu kwenu.....!!!!!!!!
 
Hawa watu hawachelewi kusema Intelegensia ya Police imeona CHADEMA wanahusika, kwani walitumia pikipiki za CDM M4C kutoka china. Hapo Kova atapigiwa makofi na mambo yanaishia hapo kwenye uchunguzi.
Hakika hizi bodaboda za CDM bana! Zimekuwa majanga siku hizi. Bahati mbaya zaidi waliopewa bodaboda hizo ni majambazi
 
R.I.P ..alikua anaenda kupanda ndege ya morogoro ama.???? Hizo pesa c angediposit bank akifika moro aziwithdraw...????..au ndo kifo kilifika no option
 
R.I.P ..alikua anaenda kupanda ndege ya morogoro ama.???? Hizo pesa c angediposit bank akifika moro aziwithdraw...????..au ndo kifo kilifika no option

Si wajua kifo hakikosi sababu ndugu
 
Usemayo ni kweli tena miongoni mwao wapo wale wanaojihusisha uokovu wa maisha yetu kila siku sijui wanaitwa nani vile!!??Huwa wanavaa sare nyeupe hivi.Wengine ni wale wanaovaa rozali kifuani ambao hujulikana kama wachunga kondoo wa bwana hususan wa kutoka lile dhehebu flani lenye nguvu na ushawishi mkubwa wa kisiasa hapa nchini.Ogopa sana watu hawa.Hii nchi ni zaidi ya uijuavyo.

hawa wavaa rozari wachunga kondoo yupo mmoja namfahamu yupo kenya anapiga kazi kwa mgongo wa rozari.yaani ni kama ile muvi ya delta force aliigiza checknoris
 
Back
Top Bottom