mgt software
JF-Expert Member
- Nov 1, 2010
- 13,778
- 7,145
Alikiuka mashariti ya UWT
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jamaa atakuwa ametofautiana na wakubwa kuhusu muundo wa serikali. labda anataka muungano wa shirikisho wenye ukakasi kwa watawala tutasikia mengi. pumzika panapostahili bwana afisaaaa
Nakubaliana na wewe Mkuu. Kuna watu humu uwezo wao wa kuchangia ni mdogo sanaMkuu na ww uwezo wako wa kuchangia ndio umefikia hapa? Sasa si bora uwe msomaji tu.
Alikiuka mashariti ya UWT
eh...ilikuwa usiku siku hiyo....
Unataka kuniambia UWT ndio weupe kiasi hiki kiasi wakitaka kuuana wenyewe kwa wenyewe mpaka wakasubiriane barabarani?
Tuache utani jamani, mimi naamini kuna kitu kingine na sio UWT, maana naamini wanakili zaidi ya hii, kwanini wasimpumzishe kwa amani tu ana akajifia kimyakimyaa kuliko kuja barabrani na fujo zote hizo.
Alikiuka mashariti ya UWT
duuuh akili za ccm ni laana tuuu......hazkutoshi weweee
ni gharana kiasi gani utaingia kama ukiamua kuomba askari ili wakusindikize? si zaidi ya elfu hamsini na unakuwa na ulinzi wa uhakika. huu ujinga mwingine wa kuangalia faida tuu bila kutaka matumiziz mazao yake ndo hayo
Maelezo yako hayaonyeshi kama ameuawa kinyama...
Jamaa huwa anachangia alafu baadae ndo anafikiria
Nakubaliana nawewe mkuu,hawa jamaa wamezidi kuchukua wake za watu hasa makazini huko wanawatishatisha tu!Mambo ya kuchukua wake za watu mabaya sana. Hata hivyo serikali iimarishe ulinzi dhidi ya raia wake, maana sheria za kudeal na wagoni zipo.
Mkuu na ww uwezo wako wa kuchangia ndio umefikia hapa? Sasa si bora uwe msomaji tu.
Ofisa mwandamizi wa idara ya Usalama wa Taifa nchini Bwana Silvanus Mzeru ameuwawa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha. Mauwaji hayo ambayo taarifa zake zimeibua hofu kubwa, yalitokea jana jioni katika mataa ya barabarani ya karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwl Julius Nyerere jijini Dar es salaam.
Habari zinasema mara baada ya kufanyika kwa tukio hilo la kinyama wauwaji hao waliondoka na briefcase ya marehemu huyo ambayo haijajulikani ndani yake ilikuwa na vitu gani.
Kwa mujibu wa watu walioshuhudia tukio hilo, kabla ya kuuwawa kwa Mzeru watu wawili waliokuwa kwenye pikipiki walirusha risasi kuelekea katika gari yake.
"Baada ya risasi hizo kurindima, Mzeru aliendesha gari lake kwa kasi na kwenda kugonga magari mengine yaliyokuwa mbele yake na kisha gari lake kutumbukia mtaroni" Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo.
Mashuhuda hao waliongeza kuwa wauwaji wa Mzeru walimfuata katika mtaro na kuumua kabla ya kuondoka na briefcase iliyokuwa kwenye gari.
Chanzo: Tanzanidaima Toleo namba 3436 Uk 3 la leo Alhamisi, Mei 1 2014.
Mytake:
Kama watu wa usalama wa Taifa wanaweza kuuwawa kinyama kiasi hicho, vipi kuhusu raia wa kawaida?! Kama raia wa kawaida wamekuwa wanapigwa risasi na kuuwa kwa mabomu kwenye mikutano ya vyama vya siasa na waliopaswa kulinda usalama wao, Kumbe haina tofauti na watu wa usalama wa Taifa?! Kama usalama wa taifa huwa wanalalamikiwa kwa kuteka na kutesa kama ilivyosemwa kwa Dr Ulimboka, Nani yuko salama?
Mkuu, mtabaki na labda tu. na hii inadhihirisha ni kwa namna gani chombo chetu hiki kinafanya kazi kwa weledi mkubwa sana