Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Mmoja auawa kwa risasi na watu wanaodhaniwa kuwa majambazi - Mataa ya Airport

Unataka kuniambia UWT ndio weupe kiasi hiki kiasi wakitaka kuuana wenyewe kwa wenyewe mpaka wakasubiriane barabarani?

Tuache utani jamani, mimi naamini kuna kitu kingine na sio UWT, maana naamini wanakili zaidi ya hii, kwanini wasimpumzishe kwa amani tu ana akajifia kimyakimyaa kuliko kuja barabrani na fujo zote hizo.

Inaweza kuwa ni mbinu pia kwamba "aliuwawa na majambazi". Ni kweli wako smart, Je yule aliyekutwa kwenye kisima nyuma ya ofisi zao tusemeje, na yule aliye limwa shaba mchana kweupe Tegeta tuseme nini na ripoti za uchunguzi wa mauaji yao jiii hadi leo, Indeed they're smart.
 
R.I.P Mzeru waliokutanguliza watalipwa hapa hapa duniani..
 
There is something wrong somewhere ....
 
mwezi uliopita walimkosakosa na risasi maeneo ya jackies bar oysterbay kuna mtu alikuwa anamfuatilia muda mrefu time will tel!!
Hawa jamaa kuua kwao sio issue kabisa mfano mama Clinton aliwahi kuwa na affair na jamaa wa usalama ambae alikuwa na personal details nyingi sana za Clinton activities na familia yake kabla ya kuwa raisi.

Wakati wa uchaguzi jamaa akataka kuanza kumchafua CIA kwakuwa walishaamua ndio next president there was no other choice but dude had to die, tells you how little provocation can end ones life.

Sasa huyu ndugu yetu sijui kawakosea nini huko juu, hila naona kama ni tukio la kijambazi tu hivi watu na mbinu zao zote wakaue mchana kweupe, uneless labda kwenye briefcase alikuwa kachukua nyaraka muhimu sana au labda majambazi walijua kuna kichele sikuhizi wafanyakazi wa benki nao si wanatonya navyosikia.

Either way ni hatari sana kama watu wanaweza uwawa mchana kweupe maana yake ni kwamba response team is very slow na hawa jamaa jeshi la polisi nao siku hizi wanapokea kichele cha nguvu tu na enough fines za barabarani to improve their response teams. Haya ni matukio ya aibu kwa jeshi la polisi. Kwakuwa atuna utamaduni kwa kufukuzana kazi for poor performances jamani ni bora wenye mahela yenu muwe waangalifu mnapoenda kutoa mahela mengi, embu kuwe na utaratibu wa discreet procedures maana njaa iliyopo inaondoa maadili na utu wetu katika jamii.
 
attachment.php
 
Ukweli ndiyo huu!!! Na wale wanaosimamia zile hotel mbili za bagamoyo wapate fundisho. Wakicheza iko siku nao watawamzeru. Ila kijana ni noma. Aisee bora Beno alikubali yaishe akafanya transfer ya ile nyumba ya kijitonyama iliyonunuliwa kwa jina la Benno.

eeh usinambie classmate wangu Beno na ujanja woote wa kichaga kumbe nyumba alinunua kumfichia swahiba wake Rizimoko?/au ndo mana cku hizi hawapo karibu kivilee kama ilivokuwa awali?/duu noma
 
Mmh kwangu mimi zimeaaidia mpk nikamfumania mke wangu.. sijaona ubaya wa pikipki

Naomba Ujambazi utangazwe ni janga la kitaifa. Kila kukicha majambaz. Hv ni nani anawapa taarifa kuwa mtu fln ana fungu la hela? Tafakari chukua hatua

Matukio ya unyang’anyi wa fedha kwa kutumia silaha wakati wa mchana kwa sasa katika jiji la Dar es salaam yamekuwa ni mengi sana. Kinachowafanya watu hawa kutumia usafiri wa pikipiki ni kutafuta wepesi wa kukimbia na kupenya hata vichochoroni kwa urahisi ili wasiweze kukamatwa. Lakini pia wakitambua kabisa kwa kitendo cha kuwa na silaha wananchi wa kawaida hawawezi kuthubutu kufanya ufuatiliaji wa aina yyte ile kwa kuhofia kipigwa risasi. Kwa kweli siwezi kuwatupia lawama jeshi la polisi kwa kushindwa kudhibiti matukio haya ingawa ni wajibu wao na kazi yao kuhakikisha usalama wa raia na mali zao vyote vinalindwa. Sababu kwa idadi ya polisi waliopo katika jiji letu ni ndogo sana hawawezi hata kidogo kuweza kuwepo kila mahali matukio hayo yanapotokea. Lakini pia hili ni tatizo la kitaifa kwamba hatuna vifaa vya kutosha vya kiusalama kuweza kudhibiti matukio kama haya hasa kutokana na miundombinu ya jiji la Dar es salaam. Kikubwa ni sisi wananchi kuonesha nia ya dhati kupambana na matukio haya kwa kuwapa ushirikiano Polisi kwa namna moja au nyingine kuhakikisha tunawadhibiti watu hawa. Kwa sababu watu wanaofanya matukio haya tunawajua na tunaishi nao mitaani ila watu tumekuwa tukiwaficha.
Umeandika vzr ila ni ktk theoretical point of view inapokuja kwenye uhalisia, jambo la wananchi kushiriana na polisi ni gumu sana kwa sababu ktk polisi wenyewe kuna majambazi wengi tu( na hata polisi wenyewe wanafahamiana ila hawachujui hatua yoyote ya kudhibiti) pia kumbuka huyo jamaa aliyeuawa ndo usalama wa taifa( by definition) kwa namna moja au nyingine alikuwa anahusika ktk kuwa-identify hao waarifu lkn ktk mazingira ya kitanzania usalama wa taifa haushughuliki na mambo km haya ambayo ni senstive badala yake wasave interests za politicials na kibaya zaid majambaz hawaangalii sura wanaangalia pesa ndo mana hata wao waliotakiwa kupambana na mambo km haya wanapatwa na uhalifu km huu ambao wao huenda walifikiri ungempata mtu/ watu mbali na wao. All in all kikulacho ki nguon mwako.
 
labda huyu jamaa kauawa na wenzake labda alikua anaiba nyaraka muhimu unajua tena sasa hivi nchi imetikisika kwa haya mambo ya katiba!!
 
Soma sheria ipo ya 1972 ukiwa na pesa kuanzia 100 unarubusiwa kuomba escort sasa sheria gani unataka?
Asante kwa taarifa pia nadhani ulichepuka kidogo kusoma comment yangu, mie issue hapo ilikuwa ni kiwango cha kukaa nacho nyumbani nikiwa na maana kama watu watajenga tabia ya kufanya transaction through bank hili suala ya mtu kukaa nyumbani na mamilion ya hela litakwisha maana unakuta mtu ana milion 25 zimepigwa (hapa naona kama utani, kama ni mauzo kwanini yasifanyike through bank ili kuondoa mwanya wa fedha haramu kuwa mikoni mwa watu). Bora hata wale zinazopigwa wakati inapelekwa bank kuliko mtu kajititia nazo ndani wiki.
 
bastola je??
Tena siku hizi kila anaemilki bastola anaanzisha yeye ugomvi alafu ndio anakuwa wa kwanza kutoa bastola kutishia, kwa akili kama hizi kwanini asiitumie kwenye ujambazi (kama walivyoruhusu pikipiki kufanya biashara ya usafiri bila kuweka limit na pia kuruhusu utoaji leseni ya u-milki wa bastola bila kufanya screening ya kweli ndivyo na matukio ya ujambazi yanazidi.
 
Jamaa yangu wa CID kaniambia jamaa alikutwa na shilingi milioni 58 wakati polisi walipopekuwa gari lake
 
Jamaa yangu wa CID kaniambia jamaa alikutwa na shilingi milioni 58 wakati polisi walipopekuwa gari lake

Criminology - na kwa kweli common sense - inatuambia huu unaonekana si ujambazi, kwani majambazi wangechukua hela.
 
ujambazi ujambazi kila cku......polisi wako likizo naona
 
mwanzilishi jambaza wa kwa kutumiaa pikipiki mbona alisumbuaaa mjini hapa ila sahv ni marehemu jamaa alikuwa muda wote anatumiaa Honda 250...alikuaa na uwezo wa kupitaaa hata sebuleni kwako akatokea mlango wa nyumaa alikua pia na shabaa jamaa alikuaa mshenzi sana .. alikua na magenge wanatumia pikipiki..jambazi huyo alikuaa anaitwa ramadhani ngonji ila polisi walim kill.....huko magwepande..na jambazi hyo alikuwa anakula na baadhi ya polisi ktk deals zao..kwa hyo matukio yote yanayo tokea lazima kuna mchoro unachorwa na bad cops wanajuaa ishu nzima
 
alipostukia kua kuna watu wanamfuatilia baada ya kupata mzigo pale uwanja wa ndege,akaamua kutaka kutoroka kwa gari yake, sasa wakati anatoka,foleni ya kuingia nyerere road ndio iliharibu,katika harakati za kujiokoa akatanua,bahati mbaya gari ikakwama pembezoni mwa barabara katika kamtaro,hapo ndio jamaa waliokua wanamfuatilia na boxer wakapata nafasi ya kumfuata katika gari na kumchapa risasi na kisha kutokomea na briefcase ambayo ndani yasemekana kulikua na hela nyingi na sembe.

Kama aliwashtukia mapema kwanin yeye ndio angewawahi kabla maana ingekuwa rahisi zaidi kwake kuwalenga watu walio kwenye piki piki? au hakuna na pisto?
 
rebkim......kwa hyo huyo aliyouawa ni muuza sembe syo
 
Back
Top Bottom