Mmomonyoko wa maadili chanzo ni wazazi na walezi kwa 99.9%

Mmomonyoko wa maadili chanzo ni wazazi na walezi kwa 99.9%

Mwamuzi wa Tanzania

JF-Expert Member
Joined
Apr 7, 2020
Posts
15,486
Reaction score
45,256
Habari!
Kuna vitu vinatokea tunaanza kumsingizia shetani au makundi.
Hayo makundi mabaya yanaundwa na wanyama?

Ni watu ambao wazazi na walezi wao wameshindwa kuwaonyesha njia.
Kitaalamu tunasema tabia ya mtoto inajengwa shule, nyumbani na barabarani.

Tone la bahari ukitia kwenye mto wa maji baridi bado maji yatakuwa baridi kwakuwa kidogo humezwa na kikubwa.
Mwalimu kazi yake ni kumpa elimu mtoto na kumlea kwa % chache.

Mzazi au mlezi ndiye mlezi wa mtoto kwa 100% hivyo mtoto akiharibika mzazi hana hoja ya kujitetea. Ni yeye kamharibu.

Mtoto wako wa kike eti kisa ni mdogo unamvalisha suruali sijui vipedo vya kubana. Hizo ndizo nguo unazomwonyesha kuwa anapaswa kuvaa akiwa mkubwa. Baadaye mpaka anafika chuo atavaa vipensi na vipedo na kukatisha sebuleni kwako.

Kijana yupo likizo nyumbani ananyua kiduku baba unafurahi tu mbele za wageni na unasema eti mtoto wangu anaweza Kiingereza huyu. Subiri akija likizo nyingine kamkague chumbani kwake utakuta vipisi vya bangi ambazo kafundishwa kuvuta na yule aliyemfundisha kunyoa kiduku.

Kama mzazi lazima umkague mtoto afya ya kiroho, akili na mwili mara kwa mara. Kumlisha, kumvesha na kumsomesha tu bila kufuatilia afya yake ya Kiroho bado hujatimiza wajibu wote.

Nakuja kuendelea
 
Back
Top Bottom