Mmuya aanza ziara ya kikazi mkoani Mtwara

Mmuya aanza ziara ya kikazi mkoani Mtwara

Wizara ya Ardhi

Govt Institution
Joined
May 14, 2024
Posts
306
Reaction score
165
IMG-20260713-WA0098.jpg

Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Kaspar Mmuya, amewasili mkoani Mtwara kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara na Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Kanali Donald Wilson Msengi.

Mara baada ya kuwasili, Mhe. Mmuya amepokea taarifa kuhusu utekelezaji wa shughuli za sekta ya Ardhi pamoja na hatua zinazochukuliwa katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi mkoani humo.

Ziara hiyo, inayofanyika kuanzia Julai 13 hadi 14, 2026, inalenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyo chini ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi zinazohusu sekta ya ardhi.
 
Ni jambo zuri ajitahidi kutatua kero kubwa ya wananchi ni ardhi.
 
Hivi kwa nini watu wa ardhi hawajali wateja wao? Wanapenda sana kuzungusha wanaofika kwenye ofisi zao kwa masuala yanayohusu ardhi.

Mfano nimenunua kiwanja toka halmashauri kwa kufanya malipo yote ikiwemo gharama/fedha za kumilikishwa (hati ya kiwanja) lakini mpaka sasa ni zaidi ya mwaka mmoja sijapatiwa hati. Kila ukienda kufuatilia wanatoa sababu zisizoeleweka.

Niliwahi kumsikia waziri wa ardhi akisema kwamba hati inapatikana ndani ya muda mfupi (nafikiri saa 48 kama sikosei), hata hivyo hali ni tofauti sana. Nimefuatilia hati kwa mwaka mmoja na miezi kadhaa lakini mpaka leo sijapewa na wala sipewe sababu za msingi za kutopatiwa hati.

Inaumiza sana kila siku kwenda halmashauri kufuatilia hati bila mafanikio yoyote, leo ukienda unaambiwa mkurugenzi kasafiri, kesho unaambiwa bado haijawekwa kwenye mfumo, mara file halijarudi toka ofisi ya mkurugenzi, dah 😢 😢 😭

Kuna wakati najuta kununua kiwanja kupitia halmashauri (ofisi ya mkurugenzi), naona bora hata ningenunua kupitia madalali kwa sababu kuna watu wamenunua kupitia madalali na wakafanikiwa mapema zaidi.

Mimi ni mteja wao ambaye natakiwa kulipia kodi ya ardhi kila mwaka pamoja na kufanya maendeleo binafsi lakini wao hawajali, kila nikienda naambiwa njoo baada ya wiki, wiki mbili mara mwezi lakini kote huko hakuna hati wala sababu za kueleweka.
 
shughuli za sekta ya Ardhi pamoja na hatua zinazochukuliwa katika kushughulikia changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi

Baadhi ya changamoto za sekta ya ardhi zinatengenezwa na watumishi wenyewe mfano kutopatiwa hati licha ya kukamilisha taratibu zote na kufuatilia kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Changamoto kama hii nayo ni ya kumsubiri waziri aje kuishughulikia kweli?

Yaani leo mwananchi akae chini aanze kuandaa bango la kutopatiwa hati ya kiwanja asubiri ziara ya waziri ili asaidiwe kweli?
 
Back
Top Bottom