Hivi kwa nini watu wa ardhi hawajali wateja wao? Wanapenda sana kuzungusha wanaofika kwenye ofisi zao kwa masuala yanayohusu ardhi.
Mfano nimenunua kiwanja toka halmashauri kwa kufanya malipo yote ikiwemo gharama/fedha za kumilikishwa (hati ya kiwanja) lakini mpaka sasa ni zaidi ya mwaka mmoja sijapatiwa hati. Kila ukienda kufuatilia wanatoa sababu zisizoeleweka.
Niliwahi kumsikia waziri wa ardhi akisema kwamba hati inapatikana ndani ya muda mfupi (nafikiri saa 48 kama sikosei), hata hivyo hali ni tofauti sana. Nimefuatilia hati kwa mwaka mmoja na miezi kadhaa lakini mpaka leo sijapewa na wala sipewe sababu za msingi za kutopatiwa hati.
Inaumiza sana kila siku kwenda halmashauri kufuatilia hati bila mafanikio yoyote, leo ukienda unaambiwa mkurugenzi kasafiri, kesho unaambiwa bado haijawekwa kwenye mfumo, mara file halijarudi toka ofisi ya mkurugenzi, dah 😢 😢 😭
Kuna wakati najuta kununua kiwanja kupitia halmashauri (ofisi ya mkurugenzi), naona bora hata ningenunua kupitia madalali kwa sababu kuna watu wamenunua kupitia madalali na wakafanikiwa mapema zaidi.
Mimi ni mteja wao ambaye natakiwa kulipia kodi ya ardhi kila mwaka pamoja na kufanya maendeleo binafsi lakini wao hawajali, kila nikienda naambiwa njoo baada ya wiki, wiki mbili mara mwezi lakini kote huko hakuna hati wala sababu za kueleweka.