Mna kheri wenye mama mkwe mzee

Mna kheri wenye mama mkwe mzee

Beesmom

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Posts
17,202
Reaction score
28,732
Hakika mna kheri.Ma mkwe vijana imekuwa shida Sana,zamani walishindikana Kwa mdomo but now wameshindikana Kwa vyote...game wanataka wale na watoto wao...

Masimango na kuchagulia waume au wake watoto wao(huyu simtaki,huyu Hana Hela,huyu mfupi Sana mbegu mbaya🙄),na kuachanisha ndoa ndo wamekuwa mstari wa mbele(huwa nashangaa Sana unakuta ma mkwe yupo free kuwasiliana na mume wa mwanae kama anawasiliana na watu wengine TU,

Kinyakyusa ni mwiko....una shida mwambie mtoto wako yeye atamwambie mumewe) siyo unapiga simu Moja Kwa moja Tena bila aibu unatanguliza na kaunafki juu"Eti mwanangu🤔 Sina chochote ndani vitu vimeisha😳"

Aisee jamani...yaan alee mke na mke wa baba mkwe wake.Hapana Kwa kweli.Una shida na pesa mwombe mwanao then mwanao atajua atatoa wapi,anamwomba mumewe au mkewe ndo akupe hilo halikuhusu!

Hongera Sana wenye wakwe vikongwe hawanaga muda huu,wanashukuru wanachopata muda huo,toka Kwa nani sijui ilimradi wamekula na kuvusha Siku😘
 
Aisee, I can imagine hii shida. Mimi mama mkwe anaweza kunipigia au nimpigie kama kuna tatizo tu. Siku nyingine zote napata salamu zake na yeye anapata salamu zangu kupitia kwa mke wangu.
Ndivyo inavyotakiwa,siyo mazoea mpaka mama mkwe anakuuliza Jana usiku ulimfanya nn mwanangu😳🙄
 
Back
Top Bottom