Mnadhani kwa huu mpango kabambe wa viongozi wa Yanga utaacha kuleta lawama na makelele kwa watu makini kama Mimi na wengineo?

Ulivyoandika tu kuwa Yanga ina mabilioni ya mashabiki ndani na nnje ya nchi nikaishia hapo kwani nimeng'amua wewe ni baba wa uongo na propaganda kama CCM.
 
Hii nchi hata hatujui tunataka nini! Hivi GSM ananufaika nini ha hii yanga? Mkiachiwa timu yenu wiki tu inawashinda. Manji aliwaachia timu yenu, ilikuwaje? Miaka minne ya msoto
unafikli GSM mjinga awekeze sehemu isiyokua na faida
 
Hii nchi hata hatujui tunataka nini! Hivi GSM ananufaika nini ha hii yanga? Mkiachiwa timu yenu wiki tu inawashinda. Manji aliwaachia timu yenu, ilikuwaje? Miaka minne ya msoto
Kwa hyo hata kama mambo wanayaficha ficha na kuyaharibu waachwe kisa wanatoa hela zao?
GSM anatangaza biashara zake pale,GSM anasimamia mapato yote ya yanga pale.anajua kinachotoka na kinachoingia.faida anapata kubwa na hawezi kutuambia.
 
Wabongo ujuaji mwingi, mtu mmoja anajifanya anajua kukosoa ufundishaji, uchezaji, uchumi, n.k. hivi kabla ya ujio wa Manji, Mo na GSM hizi vilabu vilikuwa na hali gani kiuchumi, kimafanikio na kithamani? Tulikuwa tunazidiwa hadi timu za Kenya, Sudani. Leo hii GSM na Mo wamezifanya hizi timu zipande thamani, ubora na mafanikio tele Africa mnaanza majungu na fitina kuwa zinapata faida.

Je mashabiki wanataka pesa au mafanikio? Kwasababu hizo ela ambazo mnazohoji kuwa wanachukua ni matokeo ya hao hao wakina Mo na GSM kuzikuza hizo timu na mwisho kuongeza ushawishi kwa wadhamini ili kufanya wao wasipate hasara kwa kutoa pesa zao mifukoni kuendesha timu. Kabla ya ujio wa hawa watu vilabu vilikuwa vinaingiza sh ngapi kiasi kwamba tuone hivi vilabu vilikuwa na pesa za kutosha?
 
mifukoni kuendesha timu. Kabla ya ujio wa hawa watu vilabu vilikuwa vinaingiza sh ngapi kiasi kwamba tuone hivi vilabu vilikuwa na pesa za kutosha?
unataka kusema hivi vilabu Mo dewji na GSM hawapati faida
 
Mleta mada naomba utuwekee hapa Kadi yako ya Uanachama Ili tukishaiona ndiyo tujadili HOJA yako!
 
unataka kusema hivi vilabu Mo dewji na GSM hawapati faida
Inawezekana kuna wakati wakawa wanapata faida na kuna nyakati wanapata hasara hao ni wafanyabiashara. Hao wanaendesha mambo yote kwenye taasisi inayohusu Simba na Yanga hivyo gharama za matumizi ikizidi mapato ni hasara. Ila ikitokea matumizi yamezidi mapato hiyo ni hasara. Tukumbuke kuwa sisi mashabiki hatutaki kusikia mchezaji anadai mshahara au timu imeshindwa kusafiri au kushindikana jambo fulani sababu ya pesa bali tunahitaji kila kitu kiende. Hivyo ni wajibu wa hawa akina GSM na Mo kukopa au kufanya chochote kile ili ipatikane pesa mambo yaende.
 
mkuu unaongelea hisia na siyo uhalisia kabisa
 
mkuu unaongelea hisia na siyo uhalisia kabisa
Wewe ndio unaongelea hisia sio uhalisia. Unataka ulazimishe kuwa kila siku wanapata faida. Kwenye hili mimi nitakuuliza swali je unafahamu mapato halisi ya hizi timu? Je unafahamu kiwango halisi cha matumizi ya hizi timu? Ili upate uhalisia lazima uwe na data halisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…