GSM ni mfanya biashara Tena mwenye mafanikiao kabla ya kuja Yanga, Ao wakina Mavunde, Kitenge n.k walipambana ku mshawishi GSM kuja kuwekeza Yanga.
GSM ata Leo akiamua kuiacha Yanga hawezi filisika ila Yanga tutarudi kwenye uhalisia wetu kama Mwanzo.
Wakati Manji ameodoka, Yanga ilikua na Logo yake na Facility zake na hakuna aliye sogea kuisaidi.
Yanga Ina mabilioni ya mashabiki ndani na nje ya Nchi lakini mpaka Sasa waliojiandikisha na kuchukua kadi hawazidi elfu 90.
Wengi wao hawatalipia kadi za uanachama msimu huu 2023/2024 na kufanya mapato ya klabu kupitia wanachama kupungua kutoka bilion Moja na ushee kufikia milioni 600 timu ikiwa imetwaa taji lake la 30.
Iyo milioni 600 ni fedha ya maji kwa wachezaji na first Aid kit ya timu kwa msimu.
GSM anacho faidika ni kutangaza Bland yake kupitia Yanga na wame Target kimataifa zaidi maana kwa hapa ndani wao ni maarufu.
GSM ana wekeza katika Yanga ili wote wafaidike lakini ata asipowekeza Yanga, Bado GSM bland Yao inaweza ku survive bila Yanga, ila Yanga iki achwa pekeyake haitokufa ila ita zimia (collapse) kama kipindi alipo ondoka Manji.
Udhamini wa Sasa ambao ni mkubwa haizidi bilion mbili kwa Mwaka ambao Simba wameingia na Sunderland.
Yanga na Simba wakati wanafanya iyo biashara ya jezi wao wenyewe walikua walikua wakipata 200 milioni ambayo kwa Sasa ni tone tu katika Bajeti zao.
Izo jezi Zina uharamia mwingi mpaka uziuze na kurudisha fedha Yako ndio maana Vunja bei alishindwa.
Wewe una print jez China/ Thailand kwa gharama kubwa na unalipa kodi,
Wahuni wako DAR wamesha print copy tayari na Wana ziuza 5000/= full kit.
Wote tulishuhudia siku za karibuni zilipo kamatwa maelfu ya Jezi haramu kwenye ma godown Chang'ombe DSM .
Kuiendesha klabu sio jambo rahisi kwa apa Nchini.