Mnadhani kwa huu mpango kabambe wa viongozi wa Yanga utaacha kuleta lawama na makelele kwa watu makini kama Mimi na wengineo?

Hersi kupita bila kupingwa sio hoja sana kwani Hersi anasimamia maslahi ya mwekezaji ambaye ameiwezesha Yanga kufanya vizuri katika misimu mitatu iliyopita. Kuna uwezekano kuwa kuna upigaji, lakini mbona kipindi Yanga haina mwekezaji huwa hatuoni hizo fedha zinazosemwa zinaliwa. Kama Yanga ingekua na fedha wakati ule Mwinyi Zahera asingekuwa kocha na mdhamini wa timu. Fedha walizonazo Yanga kwa sasa zinatokana na uwekezaji wa GSM, sasa kuna walafi wanataka wajipenyeze wale vya bure kwa kiulaini. GSM akiondoka hapo Yanga na akina Mzee Magoma wanarudi mashimoni walikotokea.
 
Usiumize kichwa ndugu, wengi wa wanao comment in negative way ni Makolo hayo, yanadhani mafanikio ya timu lao bovu hayawezi kuja bila ya Yanga kuvurugika kwanza.
 
Kuendesha timu ya mpira siyo kama familia
 
Hersi ana wakilisha upande wa mwekezaji au mashabiki?
Au ni pande zote?
 
"Hersi tuachie timu yetu."Alisikika mlamihogo mmoja mwenye njaa kali akisema hivyo huku akipiga myayo.
 
Game zinapigwa, timu inapata ushindi... Wachezaji wanalipwa... Mashabiki na wanachama wanafurahi... Hayo ndio ya msingi kwasasa
 
Game zinapigwa, timu inapata ushindi... Wachezaji wanalipwa... Mashabiki na wanachama wanafurahi... Hayo ndio ya msingi kwasasa
Matajiri hufa pia,Akikata moto kama manji itakuwaje
 
Kama haja kuelewa mpka hapa basi tena
 
Watanzania ndivyo tulivyo. Hapa hata katiba sheria zikivunjwa mashabiki tutafutahi as long as mambo yanaenda poa. Siku matokeo yakienda kombo timu ikaanza kutofanya vizuri, utasikia wale wale tuliokuwa tuanshangilia tukianza lawama. Na hili ndilo limekuwa pia likitokea kwa simba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…