Mnadili vipi na mwanamke ambaye ni careless

Kama hii haijakukuta bas nikupe hongera ila hawa watu wanafanya maisha yanakuwa magumu mnooo!

Huyu wangu naishi nae tu sijamuoa wala sina mpango huo kwa tabia hizi. Ni mtu mlalamishi sijawahi kuona, ni mvivu usifikirie. Yeye nguo zake tu hawezi kuzikagua kama zina kasoro kabla ya kuzivaa, mpaka umwambie ndio anastuka. Kusema apike mapema nikirudi nikute chakula tayari wala hana muda huo yeye ni simu na yeye, usingizi na yeye. Ilifika hatua nikamwambia wewe atakaekuoa, atapata tabu mno! Hilo neno analiongeaga mpaka leo


Wazazi, fundisheni watoto wenu kuwa wawajibikaji! Mtu unawezaje kushika glasi ya kunywea maji tena unaishikia mkono unaolia chakula na ukimaliza kula huitoi kwenda kuiosha? Mnaosema wanawake wote wako hivyo, mimi nitawakatalia mpaka kufa, kuna wanawake ukikaa nao ndani mpungufu unajiona wewe kwenye mambo ya majukumu ya nyumba

Ile ukimesap tu kidogo bibie anakupiga jicho la uzazi, unaona tu hapo kuna kitu hujakiweka mahala pake, ila kuna hizi kondoo, unaiona imependeza kaa nayo siku tatu tu utaelewa.
 
"......ila kuna hizi kondoo, unaiona imependeza kaa nayo siku tatu tu utaelewa".
Kweli umekereka mkuu.
 
Hiyo ni namba ya kunyamazishwa.
Ili utawalike rasmi.
Hiyo huwa ni "ngumu kumesa" kwa mwanaume. Ndo inafikia hatua mwanaume anahamia kule ili aondokane na mnyororo wa kutawaliwa.
 
Akili ya mwanamke usiichukulie serious sana as long as she's faithful... Akili yako inatosha yeye ni abiria tu kwenye safari ya maisha.

Sasa mkuu unataka demu anafikiria kama eisten?
 
Acha gubu wewe.. mchukulie kama alivyo na hakikisha humkabidhi majukumu yanayohitaji attention kubwa na kuleta madhara.

Ishi simple usiishi kwa principles utamtesa sana huyo mke na watoto.
 
Ukiona mwanamke anafanya hivyo jua alikuonyesha hizo tabia na wewe ukazichekea mwishowe mnaishi pamoja unakasirika na yeye anakushangaa.

Mwanamke akikuonyesha tabia mbovu mapema mkemee akionyesha hayupo tayari kuiacha basi wewe muache na hiyo tabia yake abakie nayo kama ni deal sana.
 
Atakuwa last born huyo, ukiwa unamuelekeza jambo mwambie kwa sauti ya upole ambayo haina ugomvi huwa wanasikiliza na kubadilika. Ukimwambia kwa ukali anazidi kukosea na wala haelewi chochote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…