Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
"......ila kuna hizi kondoo, unaiona imependeza kaa nayo siku tatu tu utaelewa".Kama hii haijakukuta bas nikupe hongera ila hawa watu wanafanya maisha yanakuwa magumu mnooo!
Huyu wangu naishi nae tu sijamuoa wala sina mpango huo kwa tabia hizi. Ni mtu mlalamishi sijawahi kuona, ni mvivu usifikirie. Yeye nguo zake tu hawezi kuzikagua kama zina kasoro kabla ya kuzivaa, mpaka umwambie ndio anastuka. Kusema apike mapema nikirudi nikute chakula tayari wala hana muda huo yeye ni simu na yeye, usingizi na yeye. Ilifika hatua nikamwambia wewe atakaekuoa, atapata tabu mno! Hilo neno analiongeaga mpaka leo
Wazazi, fundisheni watoto wenu kuwa wawajibikaji! Mtu unawezaje kushika glasi ya kunywea maji tena unaishikia mkono unaolia chakula na ukimaliza kula huitoi kwenda kuiosha? Mnaosema wanawake wote wako hivyo, mimi nitawakatalia mpaka kufa, kuna wanawake ukikaa nao ndani mpungufu unajiona wewe kwenye mambo ya majukumu ya nyumba
Ile ukimesap tu kidogo bibie anakupiga jicho la uzazi, unaona tu hapo kuna kitu hujakiweka mahala pake, ila kuna hizi kondoo, unaiona imependeza kaa nayo siku tatu tu utaelewa.

Hiyo ni namba ya kunyamazishwa.Ni shida, Mimi nimeshaambiwa nina gubu hadi na wakwe zangu. Siongei siku hizi.
Hiyo huwa ni "ngumu kumesa" kwa mwanaume. Ndo inafikia hatua mwanaume anahamia kule ili aondokane na mnyororo wa kutawaliwa.Hiyo ni namba ya kunyamazishwa.
Ili utawalike rasmi.
Acha gubu wewe.. mchukulie kama alivyo na hakikisha humkabidhi majukumu yanayohitaji attention kubwa na kuleta madhara.Kichwa cha habari chahusika.
-Hamna mpangilio wa ratiba ya nini akifanye kwa muda gani
-Anasema jambo lenye kuhitaji utatuzi bila kufafanua kama vile anayeambiwa yupokwenye akili yake
-Hazingatii alicho nacho hadi kinapitwa na muda wake wa matumizi na kusababisha hasara
-Akiambiwa kitu hakijakaa sawa anahisi kuonewa na kulalamika ilihali yeye ndio muhusika
Kwa ustawi wa familia mnadili vipi na mwanamke wa hivi?
Hatari sanakipindi cha mahusiano kwa asilimia kubwa huwa ni sanaa, kila mtu huficha madhaifu yake ila mkiingia ndoani ndio mtajua rangi zenu halisi. wengi ni mashahidi wa hili