Mnagombana unanuna, unafuta namba zake za simu, badae unasave tena; hakika mapenzi nyoso.

Mzee Mapenzi

Senior Member
Joined
Jan 9, 2019
Posts
122
Reaction score
439
Kwenye mahusiano bana kuna mengi hutokea hasa kwa wapendanao, ambao siku moja moja hutofautiana na kugombana sana hali inayopelekea mmoja kununa au wote kununa na kisha kufuta namba ya simu au kumblock kisha muda fulani ukipita unasave tena au unblock na maisha yanaendelea.

Je wewe uliwahi kufuta au kublock laazizi wako?

Au akikuzingua huwa unafanya nini katika ukomo wako wa hasira?

**

Mzee mapenzi nasema hivi; Mods naombeni msiunganishe uzi huu tafadhali
 
Unaifuta namba ila kabla ya kuifuta unainakili namba sehemu nyingine na kuihifadhi.
Au unafuta namba ambayo umeikariri kichwani piga ua husahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…