Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Mnakumbuka Matangazo ya zamani ya Radio na ITV yalivyokuwa na mvuto!?

Majira kilikuwa usiku baada ya michezo na habari
Ha ha haaaaa.
Umenikumbusha na kipinda cha majira. Na lile ziki lake.
Time hizo nakatiza mitaa kuelekea shule.
Nafkiri kilikuwa kinaletwa saa moja na nusu.
Ila sio siri, nime miss zile old days. I wish i cud go back.
 
Ile jingle ya radio one mpaka leo ipo kweli
Radiiiiioo oooone streeeeeeeo na vindegendege kwa mbali 😀😀😀
 
Unaishi Toto jijini mitaani, inahitaji kiburudisho vuta sweet menthol ni yako!!

Iwe mchana au usiku upite jangwani au porini safari ni safari ...safari lager.
 
Kijiji kimeshinda vita dhidi ya malaria, Mwenyekiti tueleze mliwezaje kushinda
Mambo vipi wanajamii.

Kwa wale vijana wenzangu tuliozaliwa enzi za Nyerere na mwinyi kuna matangazo haya utakuwa unayakumbuka. Tangazo la kwanza ni lile linaloanza hivii "Tueleze siri ya Mafanikio yako", kisha yule mrembo anajibu "Sio siri ni Levora" nakumbuka kipindi kile watu walisema kuwa yule binti ni mtoto wa tajiri Mengi.

Tangazo la Pili ni la chai jaba. Nadhani kama Diamond platnum angekuwa anafanya muziki kipindi kile wangempa hii a.k.a "Chai jaba''.

Kwa aliye na Video ama audio ya matangazo haya atuwekee hapa tujikumbushie na pia kama unayakumbuka matangazo mengine yaliyovuma enzi zile hebu tutajie hapo chini.
vita hii.
 
Mshindi sabuni yenye nguvuuuu
Yenye kutakatisha kuliko zoteeee
Mshindii eeeeheee
Mshindi eeehe eeee
 
Back
Top Bottom