Mnakumbuka matukio ya ujambazi miaka ile Moshi na Arusha, njoo tukumbushane mawili matatu

Mnakumbuka matukio ya ujambazi miaka ile Moshi na Arusha, njoo tukumbushane mawili matatu

Teko Modise

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2017
Posts
2,331
Reaction score
7,733
Miaka ile kanda ya kaskazini iligubikwa na matukio mazito ya ujambazi, nakumbuka ilikuwa haupiti mwezi bila tukio kubwa la ujambazi kutokea.

Mnakumbuka wizi wa benki ya NMB pale Mwanga kama sikosei? Mnamkumbuka kamanda Chico?

Mnakumbuka kuna battle ya risasi ya majambazi na polisi ilidumu kwa masaa kadhaa pale Arusha mpaka wanajeshi wakaingilia kati?

Mengi yalisemwa kwamba Wakenya ndio waliokuwa wanakuja Tanzania kupiga matukio. Unakumbuka tukio lipi? Njoo utujuze..
 
Zama hizo ngunguli ndio alikuwa big boss, maboss wa pgo walihama na majambazi wao.
Kuna mmoja ilikuwa KILA akihama anawapelekea kilio alipohamishiwa
 
Nimepata laki saba leo tu nakutana na mauzi ya hivi mfululizo acheni hizo nyinyi
 
Kuna Uzi mrefu sana humu kuhusu hii mada, hapa ni marudio tu
 
Kuna watu waliomchoma moto mtu Moshi, mwishowe wakarejeshewa passport zao bila kesi na kutokomea kusikojulikana
Mahita na Chico walikuwa mabosi wa polisi Kilimanjaro wakati huo.
 
Back
Top Bottom