Sasa ngoja nieleze kwa nini nasema kuwa kulikuwa na mazingira ya ufisadi. Kuna wakati hii shule ilikuwa inaongozwa kifamilia. Let me explain. Mama (mke) ni mkuu wa shule, na Baba (mume) ni mkuu wa Dayosisi. Japokuwa kulikuwa na bodi ya shule, lakini maamuzi mengi yalikuwa yanakuwa over ruled kinyume cha sheria ya utendaji. Kwa mfano kikao cha bodi ambacho mkuu wa dayosisi hakuwa member kinakutana pale shuleni pamoja na mkuu wa shule (mke wa mkuu wa Dayosisi) na kinaamua mambo x,y,z. Wana bodi wanaondoka wakijua kwamba yaliyoendelea mkutanoni ni siri na kwamba yatatekelezwa kwa sababu bodi ina mamlaka ya mwisho. Kumbe sivyo. Mkuu wa shule (mke) ananyanyua simu anamuita mkuu wa Dayosisi (mume) wanaanzisha kikao chao kingine kabisa, yale mapendekezo x,y,z yaliyotolewa kwenye bodi yanaonekana sio favorable either kwa personal interests au sababu nyingine tusizo zijua sis, kwa hiyo mkuu wa Dayosisi (Bishop) anaamua kubadilisha, anayoyataka yeye yanakuwa ndio final decision, na hiyo bodi kwa muda mrefu ilionekana ni "lame duck" kwamba haina meno.
Kutokana na hili na mengine mengi juu ya uendeshaji tata wa shule hii, ilifikia wakati wafadhili wakawa FED UP, sio utani, kwani nilikuwa nazipata hizi za moto kutoka kwa Deanna Miller, na Mch. Tellekson. So OBA wakaanza kushinikiza mkuu wa shule ambaye ni mke wa mkuu wa Dayosisi, aondoke. Shinikizo lilichukua muda, na several trips za watu wa OBA kwenda Arusha lakini hatimaye huyu mkuu wa shule alikuja ku step down. If I remember correctly, ni miaka 3 sasa tangu wabadilishe uongozi kwenye hii shule.