Mnamaanisha nini kila siku kutuletea sura zilezile katika uongozi?

Mnamaanisha nini kila siku kutuletea sura zilezile katika uongozi?

KENZY

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2015
Posts
32,529
Reaction score
76,691
Mwisho wasiku mkikaa kwenye vipaza sauti mnatusema tunawivu,ndio lazima tuwe na wivu haswa wivu wa maendeleo!.

Haiwezekani kila wakati ktk nafasi za uongozi mnatuletea sura zilezile kwani hamuwezi kuibua watu wengine vijana wasomi wakashika hizo nafasi..?

Nafikiri katika teuzi zenu muanze kuangalia na sifa ya uchungu katika taifa!.. au mnalipana fadhira kwasababu tu walisimama nanyi katika kampeni..?

Au mnafadhiriana kwasababu mnatengeneza mzunguko wa kutawala watu fulani tu..?

Makosa mnayoyafanya leo yatatupiga baadae,mambo mengine tusiangalie wewe ni nani bali taifa ni nini..?
Sio kwamba hawapo wenye sifa kushika nyadhifa hizo,wapo isipokuwa mwaleta ujuanifu hadi ktk ngazi ya taifa!.

Kauli za nchi inawenyewe sio za kubeza ni moja ya onyo Kali inayotakiwa kufanyiwa kazi haraka sana. Matabasam yenu ipo siku yatageuka kilio maana mnaitabasamia njiti ya kiberiti inayoenda kuwaka!.

Itoshe kusema ngazi za uongozi kitaifa sio Kama chama cha upatu,nanyi watu wa magamba jifungieni na mtathimini nchi yenu,kisha mje na mpango mkakati alasivyo kichuguu kinachooteshwa kikiwazidi tu mtashindwa kuking'oa.

By jitu.
 
Awamu zinabadilika, lakini watu ni walewale.
Familia ikiondoka kundi husalia lilelile.
Tutegemee maendeleo gani?
Mwisho wasiku mkikaa kwenye vipaza sauti mnatusema tunawivu,ndio lazima tuwe na wivu haswa wivu wa maendeleo!.
Haiwezekani kila wakati ktk nafasi za uongozi mnatuletea sura zilezile kwani hamuwezi kuibua watu wengine vijana wasomi wakashika hizo nafasi....
 
Mwisho wasiku mkikaa kwenye vipaza sauti mnatusema tunawivu,ndio lazima tuwe na wivu haswa wivu wa maendeleo!.
Haiwezekani kila wakati ktk nafasi za uongozi mnatuletea sura zilezile kwani hamuwezi kuibua watu wengine vijana wasomi wakashika hizo nafasi...
Miaka neenda miaka rudi watanzania ni wale wale hawabadiliki au kujifunza mbinu mpya licha ya kua na elimu na technolojia mpya.

Nyerere alituachia jamii ya tznia ambao ni:
Waoga wa mabadiliko ya aina yoyote
Walalamishi kupitiliza hata kwenye jambo wanalo weza
Wenye maneno megi bila vitendo (ni wa swahili haswa)
Wabinafsi na wala rushwa

Waoga wa mapinduzi ya kisiasa wengi wanaona umuhimu wa katiba mpya ila wanaona kwamba hiyo ni kazi ya Mbowe na wezie
Ni nchi ya Tanzania peke ambayo sio rahisi kuona tofauti ya msomi na asie msomo after all wote wanaweza kufanya kazi moja bila shida.

Majilani zetu wamepindua nchi zao kisiasa na kiuchumi ila sio watanzania kazi yetu ni kuimba kwaya hiki ni kisiwa cha amani tuna umoja, hatuna ukabila, nchi tajili, Nyerere kiongozo bora Africa nk ila wengi wana ishi kwenye umasikini ulio kithiri......ni watu wa vivu wanao taka waletewe mageuzi bila wenyewe kushughurika ni wazuri katika vita ya mitandao ya jimii (key board warriors)nk Mungu anusuru hi nchi kiongozi yoyote anaweza kufanya lolote bila upinzani wa vitendo.
 
Umenena vyema
 
Wanapeana Ili kesho walipe fadhila kwa watoto wao wakishastaafu
 
Mara nyingi Nchi za hivi huwa ni kulinda maslah ya watu, uovu, wizi.

Mwinyi alikuwa Rais Zanzibar+ Tanzania,

Mtoto ni Rais wa Zanzibar na Atakuwa Rais wa Tz!!,

Kikwete alikuwa Rais,
Mkewe n mbunge
Mtoto ni mbunge na N/waziri,

Samia ni Rais
Binti yake ni mbunge na waziri,
Mkwe wake ni mbunge na waziri.

Hovyo sana...
 
Back
Top Bottom