Mnaoamini kuwa uchawi upo mnatumia vigezo gani?

Mnaoamini kuwa uchawi upo mnatumia vigezo gani?

Mboju

Member
Joined
May 4, 2021
Posts
78
Reaction score
178
Katika miaka niliyo nayo mpaka sasa sijawahi kukubali kuwa eti kuna uchawi sijui mtu anaweza kuloga sijiui mambo yako yasiende.

Kama kweli uchawi upo kwanini hao wachawi wasiende benki wakaloga wakachukua pesa.

Kama kuna mtu humu ndani alishawahi kulogwa njoo utupe mrejesho ilikuwaje.

Pia, kama kuna mtu anajiamini anaweza kuniloga njoo uniloge we taja unachotaka kutoka kwangu nitakupa we niloge kama kweli unaweza😂😂

Mwisho hakuna uchawi ni dhana za kufikilika tu.
 
Wanakwambia eti kama Mungu yupo basi lazima na uchawi upo..



Hao ni watoto katika imani.. Hawajui kwanza hata shetani au Malaika sio viumbe halisi basi ni symbol kuwakilisha mtu mzuri au mtu mbaya... Ila Mungu yupo na hoja za kuamini yupo ziko wazi...



Imani ni nini?

Imani ni dhamiri inayoishi inayowezesha macho kuona vizuri masikio kusikia vizuri ulimi kuonja vizuri pua kunusa vizuri na MOYO kumpenda mwenyezi MUNGU
 
Kuamini kitu ,hakufanyi kitu hicho kiwepo.
tatizo linakuja ulipo
GR96g9cbMAAzJ1j.jpg
 
Back
Top Bottom