Mnaobeza mafanikio ya Awamu ya Sita, zungukeni Tanzania muone mafanikio ya Serikali ya Rais Samia katika utekelezaji wa miundombinu

Mnaobeza mafanikio ya Awamu ya Sita, zungukeni Tanzania muone mafanikio ya Serikali ya Rais Samia katika utekelezaji wa miundombinu

Robert S Gulenga

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2013
Posts
2,255
Reaction score
1,565
Kuna watu kazi yao wamekuwa ni kupinga na kubeza mafanikio ya Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Samia Suluh Hassan, yawezekana wanatumia uhuru wao wa kutoa maoni kikatiba au wameamua kupinga kwa sababu kazi yao ni kupinga bila kutambua hatuna Tanzania nyingine zaidi ya hii tunayoishi sasa, lakini niwakumbushe ndugu zangu hata wale wa upande wa pili kuwa MAFANIKIO YA SERIKALI YA AWAMU YA SITA WATANZANIA WANAYAONA, NAMBA HAZIDANGANYI.

Kwa muda ambao Samia Suluhu Hassan amekuwa madarakani kama Rais wa Jamhuri ya Muungano , kwa uwezo na kipawa alichopewa na Mwenyezi Mungu amejitahidi saana kusimamia utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa manufaa ya Watanzania. Kwa sasa katika kata zote 3956 Tanzania kuna miradi ya maendeleo inatekelezwa, katika vijiji vyote 12,319 hakuna Mwanakijiji anayetoka nje ya kijiji chake kufuata huduma za Afya , Elimu au Maji.

Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, ameendelea kuelekeza fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendelo. Ukizunguka mikoa yote Tanzania, kila Mkoa sasa unaendelea na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Masomo ya Sayansi kwa Wasichana, hivyo baada ya mwaka huu kuisha Mikoa yote itakuwa na shule ya masomo ya Sayansi kwa kila Mkoa, Mhe. Rasis ameelekeza zaidi ya bilioni 30 katika kuhakikisha Tanzania inakuwa na akina Mama Wanasayansi wa kutosha. Akina Mama jipigeni kifua nahodha yuko imara.

Kwenye Kila kata ambayo haikuwa na shule ya Sekondari, Serikali ya Awamu ya sita imepeleka jumla ya Shilingi bilion 232 kwa ajili ya ujenzi wa Shule za kata kupitia mradi wake wa SEQUIP, Watanzania wanaona haya mambo yote yanayoendelea.

Mhe Rais, Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kila mtoto anapata Elimu bora , ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Shule nyingine mpya za Sekondari 15 na Msingi 9, ujenzi wa Shule hizi uko hatua za mwisho, katika kutekeleza mradi huu mama ametoa Tsh bilion 17.25 kupitia mradi wa EP4R

Mhe. Rais anaposema anazunguka duniani kutafuta ni kweli anamaanisha na matokeo yake Watanzania wanaona, ukienda shule yeyote iwe ya Msingi au Sekondari lazima utakutana na ujezi wa darasa, ukamilishaji wa darasa au nyumba za Walimu, leo hii nchi zima jumla ya vyumba vya madarasa 304, mabweni 8, nyumba za Walimu 11, Matundu 548 ya vyoo, ujenzi wa Shule 10 za Msingi mpya na majengo ya Utawala 4 yamejengwa, Mhe. Rais ametoa zaidi ya bilion 12.37 kupitia mradi wa kuimarisha Ufundishaji na Ufunzaji katika Elimu ya Msingi.

Watanzania kwa umoja wetu tuendelee kumuombea Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kazi anayofanya usiku na mchana kuhakikisha gurudumu hili linasonga ni kubwa saana, toka amechukua kijiti hakuna mradi uliosimama, hakuna mkandarasii anayelalamika kutolipwa. Miradi yote ya barabara , maji vituo vya Afya, Umeme sasa karibia vitongoji vyote 64,384 vimeunganisha na umeme.

Mabilionsi ya fedha yanapelekwa kwenye Elimu, Afya, SGR,Bwawa la Mwalimu Nyerere, Ruzuku kwenye mbolea, mafuta Elimumsingi bure etc.

Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu, Serikali ya Awamu ya sita chini ya Samia Suluhu Hassan imeweka mkazo sana katika utoaji wa mikopo isiyo na riba kwa Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu ( Mikopo ya asilimia 10). Kwa mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imetoa zaidi ya bilion 59.2 kutoka Halmashauri 184.

Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu badala ya kuendelea kutumika kwenye makongamano na kutukana kwenye mitandao, tujiunge kwenye vikundi tuazishe makapuni tukachukue mikopo isiyo na riba kutoka katika Halashauri zetu, Serikali kwa mwaka huu wa fedha imetenga zaidi ya bilioni 75.98 kwa ajili ya mikopo isiyo na riba ya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu. Uamuzi ni wetu Vijana.

Hongera sana ndugu Innocent Bashungwa (MB) , Waziri Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,. Hongera sana Dr. Festo Dugange (MB) na David Silinde (MB) Naibu Waziri Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Timu yenu OR - TAMISEMI kwa usimamizi wa utekelezaji wa Miradi inayotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita, hakika mmekuwa wasimamizi wa nguvu kubwa anayopeleka Mh Samia Suluhu Hassan katika kuwaletea Watanzania maendeleo, licha ya changamoto zilizopo lakini Watanzania tunaona kazi mnazofanya. Watanzania wataendelea kuwaombea ili malengo, matamanio na matarajio ya Mh Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania yafikiwe.

Watanzania kwa Umoja wetu tuendelee kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mungu ampe Afya njema kwa kazi anayofanya usiku na Mchana.

TUJIANDAE KUHESABIWA KWA MAENDELEO YA TANZANIA, UJANJA NI KUSENSABIKA.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU MBARIKI RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, SAMIA SULUHU HASSAN
 
Mama Samia ni kiongozi hasa , ni vile tu wanaomkosoa wanajisahaulisha anayoyafanya.Hajawekeza kwenye mapambio kama mtangulizi wake laiti angefanya hivyo basi angekuwa juu kwa kusemwa positively kuliko Rais aliyepita.
 
Tunashukuru sasa hivi pesa atleast inaonekana....

Watu wanasafiri....

Posho angalau zaanza onekana..
....
No ubabe...
 
Mpuuzi mkubwa, hata wakoloni walileta reli, shule, makanisa na barabara, mfumuko wa bei sisi ndiyo tatizo letu
Unavyoweweseka kuikandia serikali ya Mama yetu SSH utadhani kama kweli ni mpinzani haswaa wa utawala huu kumbe ni kanyaboya lililo kwenye bahari kusubiri mpumbavu anasemo kisha kuzama naye majini [emoji16]
 
Kaka, tatizo sio kumbeza Rais, na hakuna anayekataa kuwa Rais hafanyi mazuri. Anafanya mazuri kama walivyo fanya wengine.

Shida ni watu wenye upeo bapa wanaotumia muda mwingi na majukwaa ya hadhara kusifu na kulazimisha shangilieni, hasa kwenye mikutano mbali mbali, kiasi cha kusahau kwamba shauku ya watu iko kwenye kutatua kero za kimaendeleo.

Wanaofanya Rais aonekane anabezwa ni hao ambao wakiwa mbele yake hawaezi sema sentensi moja bila kuchomekea ama "piga makofi kwa mama Samia, ama Makofi mengi sana kwa Mama Samia, ama nani kama Mama Samia heee, ....hadi mwisho wa hotuba zao!

Hadi kichefuchefu - wengine huko nje hawako hivyo
 
Mpuuzi mkubwa, hata wakoloni walileta reli, shule, makanisa na barabara, mfumuko wa bei sisi ndiyo tatizo letu
Asante Mkuu Bejamini Netanyahu, mfumuko wa bei kwa sasa ni tatizo la dunia, Tanzania inajitahidi saana kustabilize price , angalia mfumuko wa bei kwa nchi zote za Afrika Mashariki urudi uniambie tena Mpuuzi.
 
Tunashukuru sasa hivi pesa atleast inaonekana....

Watu wanasafiri....

Posho angalau zaanza onekana..
....
No ubabe...

Sent from my SM-A205F using JamiiForums mobile app
Kabisa mkuu ibanezafrica, Tanzania inafunguka, Wafanyabiashara wengi sasa wanasafiri, hotel na kumbi zilizokuwa zimefungwa kwa kukosa wateja sasa zinafunguliwa
 
Chawa, sikiliza afya sio Majengo, ndo maana hata pale Muhimbili kuna majengo makubwa makubwa ila wenye pesa hawawezi enda tibiwa, Hivyo vituo vilivyo jaa panadol ndo unasema huduma za afya?
Huduma za afya zisha toka kwenye majengo,
 
Shule za Secondary za kara kwa ajili ya kuzalisha wajinga? Kuna eleimu pale? Hao mnao wasifia watoto wao wanasoma hizo shule za kata? Watoto wa Mwiguru wako Feza, mwambie awepelekeke kule Kiomboi shule ya kata wakasome basi,
 
Back
Top Bottom