mdukuzi
JF-Expert Member
- Jan 4, 2014
- 20,925
- 51,688
Naweza sema ni mzee Ruksa, Mkapa na mama Samia ndio waliokota dodo chini ya mnazi, Nyerere, Kikwete na Magufuli waliutafuta urais kwa mbinu zote chafu na safi.
Leo tumuangalia Rais Magufuli, Pompeo wa bongo alivyousaka urais kwa mbinu za chini kwa chini.
Hapo mwanzo kulikuwa na jimbo moja likiitwa Biharamulo mkoani Kagera, John Pombe aligombea na mtu anaitwa Kabuye, yule mzee alimpa wakati mgumu sana Magufuli, wengine hawajui kuwa Magufuli aliwahi kuangukia pua kwenye ubunge alivyogombea kwa mara ya kwanza,
Watu wa Biharamulo ambao wengi ni kutoka kabila la Abasubi hawakumpenda John walimuita Mnyamahanga kwa maana ya wakuja.
John akaomba mizimu yake jimbo likagawanywa , Biharamulo Mashariki na Magharibi, akakimbilia Mashariki kwenye wanyamahanga wengi.
Huko akapambana kiume na wapinzani wake kibabe mpaka wengine kukimbia jimbo.
Mwaka 2006 akafanikisha kuundwa kwa wilaya ya Chato na jimbo la Chato.
Baadae akapambana Chato ikatoka Biharamulo Kagera ikaingia mkoa wa Geita mwaka 2012, huo ulikuwa ushindi mkubwa sana kwa Magufuli, unajua sababu.
Chato kuwa mkoa wa Kagera ingemuharibia sana kisiasa, watu hudhani Kagera yote ni ya Wahaya na Wahaya hawapendwi nchii hii kubali kataa, hawaaminiki kupewa madaraka makubwa.
Nikutajie sasa makabila yanayopatikana wilaya ya Chato. **** Warundi wengi sana kutoka Burundi kuna Waha, Wasumbwa, Wasubi, Wazinza, Warongo, Wahaya ,Wasukuma na watu wa Musoma. Kila mtu anaona hapa ni kwake na wazee wengi hapa wanaongea hizo lugha zote, ndivyo ilivokuwa kwa Magufuli, yeye aliamua kujiita Msukuma ila hakuwa Msukuma, ilikuwa ni sababu za kisiasa tu.
Mpaka wa Chato sasa ukaambaa kutoka Mganza, Bwanga, Buseresere, Buziku, Buzirayombo nk hizo kata mtu unaamua tu kujiita kabila lolote kati ya hayo makabila niliyotaja.
Huu ulikuwa ni mpango mkubwa sana ulihitaji mchakato wa miaka 20 akazaliwa John mpya kabila Msukuma ,kwenye kampeni ya urais 2020 akafungia kampeni Mwanza akahutubia kwa kisukuma akazoa kura za wasukuma wote hata wa Bariadi na Shinyanga. Ingekuwaje angehutubia kwa lugha ya Kirundi au Kizinza lugha alizozimudu vizuri, au angehutubia kwa kihaya, bila shaka asingepata hizo kura za kanda ya ziwa, kura za wasukuma ambao ni wengi .
Mbinu ya pili aliyotumia ni kutaka kuonekana ni msomi mzuri kwa kutafuta PhD ili kujenga trust kwa watu kuwa yupo vizuri kitaaluma. Magu hakuwa kilaza darasani ila hakuwa kipanga, ile PhD ina ukakasi jinsi ilivyopatikana lakini zote ilikuwa ni maadalizi ya kugombea Urais.
Mkakati wa tatu ilikuwa ni kujifanya yeye ni masikini kumbe alikuwani tajiri mkubwa sana huwezi kuwa wizara ya ujenzi ukafa masikini, Kilometa moja ya lami ni zaidi ya bilioni 1.5 amesimamia kilometa nyingi sana zilizojengwa chini yake. Hii mbinu hata Kikwete aliitumia sana kujifanya masikini kumbe ni mabilionea, ujue Watanzania wengi hawawapendi matajiri hudhani wao ndio sababu ya wao kuwa masikini.kwa hiyo aliigiza kuwa yeye ni mnyonge na masikini kumbe uongo lengo ni kuteka akili za masikini ambao ndio wengi na aliwapata aswaa
Itaendelea.....