Mnaofuga Paka jitahidini basi kuwafundisha Adabu kidogo pale Nyumba zenu zikitembelewa na Sisi Wageni

Mnaofuga Paka jitahidini basi kuwafundisha Adabu kidogo pale Nyumba zenu zikitembelewa na Sisi Wageni

Hakuna Support hapo, nimeuliza swali tuu kama anasema unaishi bunda vijijini aseme na unaishi kijiji gani.
Ili tujue ukweli ni upi.
It looks good when you see two damn Fools and authentic Mads support each other.
 
Mi naonaga paka waroho hivi paka akuone unakula akuangalie tu
Mnawafundishaje wanakuwa na adabu?
Paka ana asili ya ujeuri na udikteta hafundishiki, kwa ufupi hua anafanya kile anachojiskia. Mfano ukimshobokea ukamgusa anakasirika ila ukiwa huna habari nae atajipitisha ili umguse hahaha
 
Umenikumbusha stori moja alihadithia bimkubwa nachekaga sana. Kipindi hicho bado binti hajanizaa alimtembelea ndugu yake fulani hivi alikuwa anakaa ghorofani, sasa huyo ndugu yake alikuwa anafuga paka na bimkubwa wangu hapendi paka kinyama. Shida ya paka ile kupita kupita katikati ya miguu bimkubwa akasubiri mwenyeji wake ametoka kidogo akamchota yule paka teke moja mpaka huko chini kilichoendelea kuhusu yule paka hakujua[emoji1]. Baadae mtoto wa mwenyeji wake akawa anamtafuta paka wake bimkubwa akala buyu kama hajui kilichotokea.

Wengine wanaokera ni wanaofuga mapaka kwenye migahawa na bar wanazunguka sana!!
 
Paka ana asili ya ujeuri na udikteta hafundishiki, kwa ufupi hua anafanya kile anachojiskia. Mfano ukimshobokea ukamgusa anakasirika ila ukiwa huna habari nae atajipitisha ili umguse hahaha
Kweli kabisa mi humfungia jikoni Kukiwa na wageni au akinichosha lakin kuna muda anatulia kweli kuna muda mtundu huyo
 
Umenikumbusha stori moja alihadithia bimkubwa nachekaga sana. Kipindi hicho bado binti hajanizaa alimtembelea ndugu yake fulani hivi alikuwa anakaa ghorofani, sasa huyo ndugu yake alikuwa anafuga paka na bimkubwa wangu hapendi paka kinyama. Shida ya paka ile kupita kupita katikati ya miguu bimkubwa akasubiri mwenyeji wake ametoka kidogo akamchota yule paka teke moja mpaka huko chini kilichoendelea kuhusu yule paka hakujua[emoji1]. Baadae mtoto wa mwenyeji wake akawa anamtafuta paka wake bimkubwa akala buyu kama hajui kilichotokea.

Wengine wanaokera ni wanaofuga mapaka kwenye migahawa na bar wanazunguka sana!!
Hawafugi paka wanapenda kwenda sehemu ya chakula
 
Kwanza niwe muwazi ( nikiri ) kuwa GENTAMYCINE napenda sana Paka na ninae Mmoja namfuga na ukitaka Ugombane nami mguse ndipo utajua kwanini Nyoka hana Ugoko na Wimbo wa Taifa hauna Kolabo.

Hata hivyo sipendi Paka ambao Wanafugwa na wenye Nyumba ila hawana Adabu pindi Nyumba husika ikitembelewa na Wageni wasio na Ratiba Maalum akina GENTAMYCINE na Wengineo.

Jana jioni nilimtembelea Mtu Kwake ambapo alinikarimu kwa Chakula Kizuri chenye Nyama ya Kuku iliyokaangwa ambayo kwa Umasikini wangu Ulionitukuka sijala Nyama ya Kuku tokea mwaka 2019.

Nilimshukuru mno Mwenyeji wangu kwa Ukarimu wake huo wa Msosi ila nilikwazika zaidi na Paka wake alivyokuwa anakaba Kona zote utadhani Mabeki wa Yanga SC akina Job na Bangala ili nami niwe namdondoshea vipande na twende sawa hadi mwisho.

Kuna muda nikajiuliza au Mwenyeji wangu na Mmiliki wa Paka alikuwa kampa Maagizo Maalum Paka wake kuwa ahakikishe muda wote tu ananikodolea kwa Huruma ili niingiwe na Imani niwe namdonyolea nae Vipande ale?

Kiukweli kwa Kuzuga mbele ya Wenyeji wangu ili nisionekane Mchoyo na nina Roho Mbaya kwa Wanyama ilinilazimu GENTAMYCINE nijifanya Mama Theresa ( Mwenye Huruma ) kwa muda mbele ya Yule Paka, ila Moyoni nilikuwa na Hasira ( Kisununu ) nae kweli kweli kiasi kwamba angejua pengine hata asingekaa Jirani nami vile na angetoka zake tu Baru ( Nduki ) ajiokoe.

Kweli nilikimaliza kile Chakula chote japo nikiri tu kuwa kwa Ukodoaji ule wa Kihuruma wa Paka huku akinilia Nyau Nyau mara Yule Kuku ni kama tuligawana nae Pasu kwa Pasu kuelekea Matumnboni mwetu.

Hata hivyo kuna muda Mwenyeji wangu na Mkewe ( Shemela ) waliingia Chumbani ( nadhani Kupekechuana cha Fasta Fasta ) hivyo kuniacha GENTAMYCINE pale Sebuleni na Paka wao ambapo nami nikaona nichukue / nitumie Fursa ile adhimu ambapo nilimpiga Bao Moja Takatifu ambalo nina uhakika ningempiga nalo Mwanadamu hivi sasa ama angekuwa ICU Muhimbili au Wodi Namba 26 ( Mortuary ) Muhimbili na Mimi kuyaanza Maisha yangu mapya na ya kudumu Gerezani Segerea.

Hebu Wafunzeni Adabu Paka wenu wawe kama huyu Wangu ambaye ana Maadili yote na hata wakija Wageni Nyumbani huonyesha Nidhamu ya hali ya Juu kiasi hadi kuna Wageni wengine humpenda na humpa Zawadi ambayo Mimi huwa naenda Kumnunulia Maziwa na Samaki na Yeye Kufurahia zaidi.

Paka ukimfunza vyema hata ukiwa Unaongea Kilugha Chenu Kiswahili, Kizanaki, Kimakuwa na Kitutsi anakusikiliza, anakuelewa na anakutii hadi utahisi labda unaishi na Mwanadamu Mwenzako wakati kumbe ni Mnyama tu.
Moments chache sana kama hizi unapoongeaga points.

Paka wanaudhi sana. Kuna hotel moja nakubali sana mapishi yao lkn wamejaza mapaka na kila nikifika pale hata kabla sijaletewa oda yangu basi hayo yananizunguka. Kuna siku hadi nikamwambia mhudumu akae karibu anifukuzie hao paka lasivyo sitakula hio oda niondoke na nisilipe
 
Paka wa hivyo huwa tunawarushia kamfupa chini ya meza, mbele kidogo ya miguu...

Unamuacha akae sawa akilambalamba mfupa, unamfumua kama penati ya Bocco iliyoenda dondokea Chalinze...
 
Back
Top Bottom