Mnaofuga Paka jitahidini basi kuwafundisha Adabu kidogo pale Nyumba zenu zikitembelewa na Sisi Wageni

Hakuna Support hapo, nimeuliza swali tuu kama anasema unaishi bunda vijijini aseme na unaishi kijiji gani.
Ili tujue ukweli ni upi.
It looks good when you see two damn Fools and authentic Mads support each other.
 
Mi naonaga paka waroho hivi paka akuone unakula akuangalie tu
Mnawafundishaje wanakuwa na adabu?
Paka ana asili ya ujeuri na udikteta hafundishiki, kwa ufupi hua anafanya kile anachojiskia. Mfano ukimshobokea ukamgusa anakasirika ila ukiwa huna habari nae atajipitisha ili umguse hahaha
 
Umenikumbusha stori moja alihadithia bimkubwa nachekaga sana. Kipindi hicho bado binti hajanizaa alimtembelea ndugu yake fulani hivi alikuwa anakaa ghorofani, sasa huyo ndugu yake alikuwa anafuga paka na bimkubwa wangu hapendi paka kinyama. Shida ya paka ile kupita kupita katikati ya miguu bimkubwa akasubiri mwenyeji wake ametoka kidogo akamchota yule paka teke moja mpaka huko chini kilichoendelea kuhusu yule paka hakujua[emoji1]. Baadae mtoto wa mwenyeji wake akawa anamtafuta paka wake bimkubwa akala buyu kama hajui kilichotokea.

Wengine wanaokera ni wanaofuga mapaka kwenye migahawa na bar wanazunguka sana!!
 
Paka ana asili ya ujeuri na udikteta hafundishiki, kwa ufupi hua anafanya kile anachojiskia. Mfano ukimshobokea ukamgusa anakasirika ila ukiwa huna habari nae atajipitisha ili umguse hahaha
Kweli kabisa mi humfungia jikoni Kukiwa na wageni au akinichosha lakin kuna muda anatulia kweli kuna muda mtundu huyo
 
Hawafugi paka wanapenda kwenda sehemu ya chakula
 
Moments chache sana kama hizi unapoongeaga points.

Paka wanaudhi sana. Kuna hotel moja nakubali sana mapishi yao lkn wamejaza mapaka na kila nikifika pale hata kabla sijaletewa oda yangu basi hayo yananizunguka. Kuna siku hadi nikamwambia mhudumu akae karibu anifukuzie hao paka lasivyo sitakula hio oda niondoke na nisilipe
 
Paka wa hivyo huwa tunawarushia kamfupa chini ya meza, mbele kidogo ya miguu...

Unamuacha akae sawa akilambalamba mfupa, unamfumua kama penati ya Bocco iliyoenda dondokea Chalinze...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…