mwangalingimungu
JF-Expert Member
- Jul 29, 2013
- 1,301
- 733
1. Kama lengo ni kukemea upendeleo, lisianzie wala kuishia kwa Yanga ama kwa mechi husika tu. Tulaumu kila upendeleo unapoonesha dalili za kujitokeza. Dalili za mwanzo za upendeleo kwenye mechi hi(z)i ni kule kuwa na timu mwenyeji na mgeni kwenye mechi moja tu ya mtoano. Inaweza kufanyika hivyo iwapo tu viwanja vya mechi hizo vitaamuliwa kabla ya mashindano kuanza na hatimaye timu ya kiwanja hicho ikasadifu kufikia hatua hiyo. European Champions League ndivyo wafanyavyo. Kutetea fairness kwa kutoanza na hilo bali na kuhukumu mechi yenyewe tu, si tofauti na kutegemea maji mtungini ilhali visima vimekauka!Hoja zako zinaonyesha licha tu ya kuzidiwa na mahaba ya timu uipendayo lakini hata ile sifa niliyotaka kukupa kuwa mchambuzi huru haikustahili kabisa. Kwa taarifa yako wachambuzi wote dunianiwana timu wazipendazo, wana mapenzi binafsi. Hata waamuzi pia, waandishi wa habari na viongozi wa vyama vya soka pia. Kinachowatofautisha na mashabiki na wanazi ni kuwa wanapokuwa kazini au hata kama sio kazini, inapobidi wao wanatazama jambo kwa macho mawili. Lakini wewe unadhirihisha uko tayari kufumba macho pale unapoambiwa ukweli ili mradi tu timu yako inaguswa. Waungwana hukaa kimya, pale ushahidi wa mambo unavyokuwa kinyume chao. Nitafafanua.
1. Unadai eti unbiased opinion yoyote juu ya swala hili ingepaswa kwanza kuzingatia ukweli kwamba upendeleo mkubwa kuliko wote kwenye mechi za Azam vs. Mwadui na Yanga vs. Coastal Union kwa kuzichezea mechi hizo za mkondo mmoja kwenye viwanja vya timu mojawapo. Seriously? Yaani tusijadili utumbo wa waamuzi wa jana kwa sababu ratiba haikuwa fair kwako? Ulianzisha mada hiyo ya ratiba watu wakakupinga? Sawa. Hata tukianza kuzingatia kujadili hilo kama tunataka kutenda HAKI unadhani itafaa kuanzia na mechi ya Coastal Union v. Yanga tu, au turudi nyuma zaidi kwa Yanga kucheza mechi zote za FA nyumbani kabla ya hii mechi ya Coastal Union, tena ambayo imepangwa hivi kutokana na pressure tu za wadau?
2. Unadai eti unbiased opinion yoyote juu ya maswala ya jana ingejiridhisha kwanza kwa kutizama picha kutoka pande mbalimbali za magoli ya Yanga kabla ya kujiridhisha kwamba ni ya offside/mkono au la. Kuangalia matokeo hayo kutoka upande huohuo mmoja hakutoshi kumfikisha mtu kwenye unbiased opinion. Ni kuyahukumu magoli hayo out of context.
Hii ni sheria au kanuni gani au ndio unaianzisha? Refa anapoamua offside huwa anatumia picha za TV? Walioko uwanjani wanaangalia mechi laivu unataka nao wasubiri picha za tv? Mechi zinazochezwa bila kurushwa laivu hazina offside? Wanaotazama uwanjani huwa wanapiga kelele za kupinga au kuzomea kutokana na picha za TV? Wakati Yanga wanapiga mwamuzi mwaka 2012 walitumia picha? Acha kuleta hoja nyepesi kwenye vitu serious.
3. Hoja yako hii ya mgongano wa maslahi kati ya Azam FC na TV yako sina opinion kwa sasa, japo sijui inaingiliana vipi na
utumbo wa maamuzi ya mechi kati ya Coastal Union v. Yanga
4. Hoja yako hii namba nne nakubaliana nayo kwa 100%. Hizi hoja ndio zinazotakiwa kutoka kwa mtu mwenye heshima kama wewe. Walichofanya mashabiki wa Coastal Union ni uhuni usiokubalika. Adhabu kubwa iwaandane popote walipo. Lakini adhabu hii isiishie hapo tu, TFF wachunguze pia hivi vitendo vya waamuzi Ni bahati mbaya aU kuna nguvu ya mlungula?
5. Hoja yako hii ingetolewa na mtu mwingine ningeamini ni mtu asiyejua kabisa sheria za mchezo, lakini kwa kutolewa na wewe acha tu nijiaminishe kuwa kuna mtu anatumia ID yako! Retaliation yoyote ni straight red card. Wewe hili unalijua. Kulipizia ni kosa la kadi nyekundu moja kwa moja. Suala la upimaji wa uzito wa kosa linatokana na mambo mengine kama kusukuma lakini sio kumfata mchezaji mwenzako na kumkanyaga kifuani au tumboni huku ukiwa huna dhamira ya kucheza mpira. Bila blah blah na kufariajiana haziwezi kutsaidia wachezaji wetu. Kwa kweli Oscar Joshua ana bahati kuendelea kucheza mpira baada ya tukio lile.
Kwetu sisi wengine tushajizoesha kusema nyekundu nyekundu, bluu bluu sio mara bluu bahari au bluu maziwa.
2. Mbona unakataa hoja ya kutoangalia picha za upande mmoja kwa kuikubali hoja yenyewe? Kwani mwamuzi anafuatilia pambano akiwa kiwanjani kwa kuangalia TV? Si anafuatilia kwa anavyoona moja kwa moja uwanjani? Kwani TV ikija kubaini kwamba alikosea, maamuzi ya magoli yanabatilshwa? Goli la mkono wa Mungu dhidi ya Uingereza lililofungwa na Maradona lilikataliwa baada ya kuangaliwa kwenye TV? Maradona mwenyewe alikuja kupewa kadi au angalau kuonywa baada ya kubainika na mwenyewe kukiri kuwa alilifunga kwa mkono? Kwa hivyo tuseme Argentina ilibebwa? Anavyoona mwamuzi akiwa kiwanjani ni tofauti na inavyoona kamera ya TV. Ili kupata picha ya jumla ya tukio lenyewe, kunahitajika mandhari (views) mbalimbali za tukio hilohilo moja ndio ukweli halisi ubainike na ndio ibainike iwapo mwamuzi anastahili lawama ama la.
3. Inawezakana usiifahamu hoja yangu kuhusu mgongano wa kimaslahi kwa Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu na FA. Lakini kwa walio fair na objective naamini wameelewa.
4. Nashangaa kwamba unakubaliana nami kwamba kuvamia uwanja na kupiga mwamuzi ni uhuni, lakini ukakaa kimya mpaka baada ya mimi kulianika. Ndio fairness yenyewe hiyo?
5. Makosa yote yanayohusu kadi yameshatajwa, mojawapo likiwa ni retaliation. Lakini kutamkwa huko hakumnyimi fursa mwamuzi ya kutumia akili yake kabla ya kuamua. Kama nilivyosema awali, inavyoona kamera ya TV sivyo anavyoona mwamuzi. Mwamuzi anaweza kushtukia mchezaji aliyepigwa kiwiko na mwenzake akiwa anagaagaa kwa maumivu. Lakini kwa sababu hakuona tendo lenyewe likitokea, atategemea usaidizi wa assistant referee la sivyo atatumia akili yake. Kamera za (Azam) TV zimeonesha tukio la kulipiza kisasi, lakini hazikuonesha objectively mwamuzi alikuwa wapi wakati huo. Kuendelea kuzikariri picha za tukio hilo ni kuwachota kisaikolojia watizamaji waamini kwamba refa amelifumbia macho swala hilo. Inaweza isiwe hivyo, lakini dhana hii haiwezi kuepukika unapokumbuka kwamba Azam team ni mdau na mshiriki wa mashindano haya. Ndiyo huo mgongano wa kimaslahi ulioshindwa kuufahamu.
Siandiki haya kwa mapenzi ya Yanga au kutaka kuwa mchambuzi huru, la hasha. Si aibu kwangu kutokuwa mchambuzi huru kwa sababu sijawahi na sitawahi kujinasibu au kutamani niwe hivyo. Naandika haya kwa sababu ndio uhalisia unaosahauliwa na baadhi yetu mnapovaa miwani ya vioo vizito vya kulazimisha upendeleo usiokiwapo na kuufumbia mkubwa na wa dhahiri zaidi.