Mnaoibeba Yanga hamuisaidii, mnaiumiza...

Mnaoibeba Yanga hamuisaidii, mnaiumiza...

Hoja zako zinaonyesha licha tu ya kuzidiwa na mahaba ya timu uipendayo lakini hata ile sifa niliyotaka kukupa kuwa mchambuzi huru haikustahili kabisa. Kwa taarifa yako wachambuzi wote dunianiwana timu wazipendazo, wana mapenzi binafsi. Hata waamuzi pia, waandishi wa habari na viongozi wa vyama vya soka pia. Kinachowatofautisha na mashabiki na wanazi ni kuwa wanapokuwa kazini au hata kama sio kazini, inapobidi wao wanatazama jambo kwa macho mawili. Lakini wewe unadhirihisha uko tayari kufumba macho pale unapoambiwa ukweli ili mradi tu timu yako inaguswa. Waungwana hukaa kimya, pale ushahidi wa mambo unavyokuwa kinyume chao. Nitafafanua.

1. Unadai eti unbiased opinion yoyote juu ya swala hili ingepaswa kwanza kuzingatia ukweli kwamba upendeleo mkubwa kuliko wote kwenye mechi za Azam vs. Mwadui na Yanga vs. Coastal Union kwa kuzichezea mechi hizo za mkondo mmoja kwenye viwanja vya timu mojawapo. Seriously? Yaani tusijadili utumbo wa waamuzi wa jana kwa sababu ratiba haikuwa fair kwako? Ulianzisha mada hiyo ya ratiba watu wakakupinga? Sawa. Hata tukianza kuzingatia kujadili hilo kama tunataka kutenda HAKI unadhani itafaa kuanzia na mechi ya Coastal Union v. Yanga tu, au turudi nyuma zaidi kwa Yanga kucheza mechi zote za FA nyumbani kabla ya hii mechi ya Coastal Union, tena ambayo imepangwa hivi kutokana na pressure tu za wadau?

2. Unadai eti unbiased opinion yoyote juu ya maswala ya jana ingejiridhisha kwanza kwa kutizama picha kutoka pande mbalimbali za magoli ya Yanga kabla ya kujiridhisha kwamba ni ya offside/mkono au la. Kuangalia matokeo hayo kutoka upande huohuo mmoja hakutoshi kumfikisha mtu kwenye unbiased opinion. Ni kuyahukumu magoli hayo out of context.

Hii ni sheria au kanuni gani au ndio unaianzisha? Refa anapoamua offside huwa anatumia picha za TV? Walioko uwanjani wanaangalia mechi laivu unataka nao wasubiri picha za tv? Mechi zinazochezwa bila kurushwa laivu hazina offside? Wanaotazama uwanjani huwa wanapiga kelele za kupinga au kuzomea kutokana na picha za TV? Wakati Yanga wanapiga mwamuzi mwaka 2012 walitumia picha? Acha kuleta hoja nyepesi kwenye vitu serious.

3. Hoja yako hii ya mgongano wa maslahi kati ya Azam FC na TV yako sina opinion kwa sasa, japo sijui inaingiliana vipi na
utumbo wa maamuzi ya mechi kati ya Coastal Union v. Yanga

4. Hoja yako hii namba nne nakubaliana nayo kwa 100%. Hizi hoja ndio zinazotakiwa kutoka kwa mtu mwenye heshima kama wewe. Walichofanya mashabiki wa Coastal Union ni uhuni usiokubalika. Adhabu kubwa iwaandane popote walipo. Lakini adhabu hii isiishie hapo tu, TFF wachunguze pia hivi vitendo vya waamuzi Ni bahati mbaya aU kuna nguvu ya mlungula?

5. Hoja yako hii ingetolewa na mtu mwingine ningeamini ni mtu asiyejua kabisa sheria za mchezo, lakini kwa kutolewa na wewe acha tu nijiaminishe kuwa kuna mtu anatumia ID yako! Retaliation yoyote ni straight red card. Wewe hili unalijua. Kulipizia ni kosa la kadi nyekundu moja kwa moja. Suala la upimaji wa uzito wa kosa linatokana na mambo mengine kama kusukuma lakini sio kumfata mchezaji mwenzako na kumkanyaga kifuani au tumboni huku ukiwa huna dhamira ya kucheza mpira. Bila blah blah na kufariajiana haziwezi kutsaidia wachezaji wetu. Kwa kweli Oscar Joshua ana bahati kuendelea kucheza mpira baada ya tukio lile.

Kwetu sisi wengine tushajizoesha kusema nyekundu nyekundu, bluu bluu sio mara bluu bahari au bluu maziwa.
1. Kama lengo ni kukemea upendeleo, lisianzie wala kuishia kwa Yanga ama kwa mechi husika tu. Tulaumu kila upendeleo unapoonesha dalili za kujitokeza. Dalili za mwanzo za upendeleo kwenye mechi hi(z)i ni kule kuwa na timu mwenyeji na mgeni kwenye mechi moja tu ya mtoano. Inaweza kufanyika hivyo iwapo tu viwanja vya mechi hizo vitaamuliwa kabla ya mashindano kuanza na hatimaye timu ya kiwanja hicho ikasadifu kufikia hatua hiyo. European Champions League ndivyo wafanyavyo. Kutetea fairness kwa kutoanza na hilo bali na kuhukumu mechi yenyewe tu, si tofauti na kutegemea maji mtungini ilhali visima vimekauka!
2. Mbona unakataa hoja ya kutoangalia picha za upande mmoja kwa kuikubali hoja yenyewe? Kwani mwamuzi anafuatilia pambano akiwa kiwanjani kwa kuangalia TV? Si anafuatilia kwa anavyoona moja kwa moja uwanjani? Kwani TV ikija kubaini kwamba alikosea, maamuzi ya magoli yanabatilshwa? Goli la mkono wa Mungu dhidi ya Uingereza lililofungwa na Maradona lilikataliwa baada ya kuangaliwa kwenye TV? Maradona mwenyewe alikuja kupewa kadi au angalau kuonywa baada ya kubainika na mwenyewe kukiri kuwa alilifunga kwa mkono? Kwa hivyo tuseme Argentina ilibebwa? Anavyoona mwamuzi akiwa kiwanjani ni tofauti na inavyoona kamera ya TV. Ili kupata picha ya jumla ya tukio lenyewe, kunahitajika mandhari (views) mbalimbali za tukio hilohilo moja ndio ukweli halisi ubainike na ndio ibainike iwapo mwamuzi anastahili lawama ama la.
3. Inawezakana usiifahamu hoja yangu kuhusu mgongano wa kimaslahi kwa Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu na FA. Lakini kwa walio fair na objective naamini wameelewa.
4. Nashangaa kwamba unakubaliana nami kwamba kuvamia uwanja na kupiga mwamuzi ni uhuni, lakini ukakaa kimya mpaka baada ya mimi kulianika. Ndio fairness yenyewe hiyo?
5. Makosa yote yanayohusu kadi yameshatajwa, mojawapo likiwa ni retaliation. Lakini kutamkwa huko hakumnyimi fursa mwamuzi ya kutumia akili yake kabla ya kuamua. Kama nilivyosema awali, inavyoona kamera ya TV sivyo anavyoona mwamuzi. Mwamuzi anaweza kushtukia mchezaji aliyepigwa kiwiko na mwenzake akiwa anagaagaa kwa maumivu. Lakini kwa sababu hakuona tendo lenyewe likitokea, atategemea usaidizi wa assistant referee la sivyo atatumia akili yake. Kamera za (Azam) TV zimeonesha tukio la kulipiza kisasi, lakini hazikuonesha objectively mwamuzi alikuwa wapi wakati huo. Kuendelea kuzikariri picha za tukio hilo ni kuwachota kisaikolojia watizamaji waamini kwamba refa amelifumbia macho swala hilo. Inaweza isiwe hivyo, lakini dhana hii haiwezi kuepukika unapokumbuka kwamba Azam team ni mdau na mshiriki wa mashindano haya. Ndiyo huo mgongano wa kimaslahi ulioshindwa kuufahamu.
Siandiki haya kwa mapenzi ya Yanga au kutaka kuwa mchambuzi huru, la hasha. Si aibu kwangu kutokuwa mchambuzi huru kwa sababu sijawahi na sitawahi kujinasibu au kutamani niwe hivyo. Naandika haya kwa sababu ndio uhalisia unaosahauliwa na baadhi yetu mnapovaa miwani ya vioo vizito vya kulazimisha upendeleo usiokiwapo na kuufumbia mkubwa na wa dhahiri zaidi.
 
Ushauri:
Nenda na kamera taifa.Vua ushabiki wako.kaa jukwaa kuu karibu na uwanja(VIP B/VIP C ) kaa maeneo mkabala na boksi la 18(usikae nyuma/pembeni ya goli)fanya kazi moja tu mmulike mshika kibendera na offside zake...nyingi kati ya atakazonyanyua kibendera unaweza gundua hayupo kwenye sehemu sahihi...anabahatisha bahatisha tu.
 
shida ya soka tanzania inaanzia kwa Malinzi

He has no moral authority ya kuongoza soka
malinzi ndilo tatizo kwenye soka la bongo,
yaani hawa viongozi wa tff wanashindwa kuficha mapenzi yao bila kumpiha chini malinzi huwezi kuona maendeleo ya soka.

Raisi wa zamani wa tff Tenga alijitahidi sana.
 
Marefa nao wengiwao ni hivyo hivyo.mara nyingi hawaoni matukio kwa ukaribu au "angle" sahihi...aghalabu wanakuwa mbali na tukio husika...na wao wanabahatisha bahatisha tu...
Nitatoa mfano...ktk shambulizi la kustukiza(counter attack)
Geofrey Taita alimwangusha Okwi ndani ya boksi refa akapiga filimbi kuashiria faulo akiwa katikati ya uwanja...maskini hakujua kama wameangushana ndani ya boksi...watu wanajua penalti refa akaamuru ipigwe freekick...
(Mechi ya droo moja moja Stephano mwasyika/musa mgosi)
 
malinzi ndilo tatizo kwenye soka la bongo,
yaani hawa viongozi wa tff wanashindwa kuficha mapenzi yao bila kumpiha chini malinzi huwezi kuona maendeleo ya soka.

Raisi wa zamani wa tff Tenga alijitahidi sana.
Malinzi ndio kiongozi mbovu wa TFF Tanzania tumewahi lakini mpira una wadau wengi sana kama nao wangetimiza wajibu wao sidhani kama TFF wangefanya huu ujinga

1.Waamuzi
2.Makocha
3.Wachezaji
4.Viongozi wa vilabu
5.Viongozi wa vyama vya mikoa
6.Sisi mashabiki pia tunachangia sana kurudisha nyuma soka letu
 
Kwa mechi ya jana kabla hujazungumzia red card aliyopaswa kupewa Oscar ningeona ni uanamichezo kuzungumzia kiwiko alichopigwa usoni na mchezaj wa coastal laiti km refa angekuwa makini na tukio la kupigwa kiwiko kwa Oscar wkt huo akiwa karibu ya mita 6 lkn alishindwa kuchukuwa hatua.siungi mkono kadi ya njano kwenye faulu ya red card lkn lait refa angetimiza wajibu wake cdhan km ingefikia hatua ile ya Joshua kureact.Kwenye goli alofunga ngoma hakukuwa na offside kwa sababu beki wa kati wa coastal aliruka juu na yondan wkt huo hakukuwa hata na beki aliyesimama kumkaba ngoma sasa offside haiji kutokana na mtu kuwa alone bali wakat mpira unapigwa yy alikuwa ni kama hana madhara kutokana na kule mpira ulikopigwa ila akaonekana km amezidi kutokana kuwa pekeyake lkn siyo goli la ngoma ni halali kbsa na kuhusu goal la Tambwe nadhani mpira aliupiga kwa mkono ingawa refa alikuwa mbali hivyo nadhan hakuweza kuona tukio lile hata ww namimi tumeona baada ya kamera kurudia Mara kwa Mara.
 
1. Kama lengo ni kukemea upendeleo, lisianzie wala kuishia kwa Yanga ama kwa mechi husika tu. Tulaumu kila upendeleo unapoonesha dalili za kujitokeza. Dalili za mwanzo za upendeleo kwenye mechi hi(z)i ni kule kuwa na timu mwenyeji na mgeni kwenye mechi moja tu ya mtoano. Inaweza kufanyika hivyo iwapo tu viwanja vya mechi hizo vitaamuliwa kabla ya mashindano kuanza na hatimaye timu ya kiwanja hicho ikasadifu kufikia hatua hiyo. European Champions League ndivyo wafanyavyo. Kutetea fairness kwa kutoanza na hilo bali na kuhukumu mechi yenyewe tu, si tofauti na kutegemea maji mtungini ilhali visima vimekauka!
2. Mbona unakataa hoja ya kutoangalia picha za upande mmoja kwa kuikubali hoja yenyewe? Kwani mwamuzi anafuatilia pambano akiwa kiwanjani kwa kuangalia TV? Si anafuatilia kwa anavyoona moja kwa moja uwanjani? Kwani TV ikija kubaini kwamba alikosea, maamuzi ya magoli yanabatilshwa? Goli la mkono wa Mungu dhidi ya Uingereza lililofungwa na Maradona lilikataliwa baada ya kuangaliwa kwenye TV? Maradona mwenyewe alikuja kupewa kadi au angalau kuonywa baada ya kubainika na mwenyewe kukiri kuwa alilifunga kwa mkono? Kwa hivyo tuseme Argentina ilibebwa? Anavyoona mwamuzi akiwa kiwanjani ni tofauti na inavyoona kamera ya TV. Ili kupata picha ya jumla ya tukio lenyewe, kunahitajika mandhari (views) mbalimbali za tukio hilohilo moja ndio ukweli halisi ubainike na ndio ibainike iwapo mwamuzi anastahili lawama ama la.
3. Inawezakana usiifahamu hoja yangu kuhusu mgongano wa kimaslahi kwa Azam TV kuonesha mechi za Ligi Kuu na FA. Lakini kwa walio fair na objective naamini wameelewa.
4. Nashangaa kwamba unakubaliana nami kwamba kuvamia uwanja na kupiga mwamuzi ni uhuni, lakini ukakaa kimya mpaka baada ya mimi kulianika. Ndio fairness yenyewe hiyo?
5. Makosa yote yanayohusu kadi yameshatajwa, mojawapo likiwa ni retaliation. Lakini kutamkwa huko hakumnyimi fursa mwamuzi ya kutumia akili yake kabla ya kuamua. Kama nilivyosema awali, inavyoona kamera ya TV sivyo anavyoona mwamuzi. Mwamuzi anaweza kushtukia mchezaji aliyepigwa kiwiko na mwenzake akiwa anagaagaa kwa maumivu. Lakini kwa sababu hakuona tendo lenyewe likitokea, atategemea usaidizi wa assistant referee la sivyo atatumia akili yake. Kamera za (Azam) TV zimeonesha tukio la kulipiza kisasi, lakini hazikuonesha objectively mwamuzi alikuwa wapi wakati huo. Kuendelea kuzikariri picha za tukio hilo ni kuwachota kisaikolojia watizamaji waamini kwamba refa amelifumbia macho swala hilo. Inaweza isiwe hivyo, lakini dhana hii haiwezi kuepukika unapokumbuka kwamba Azam team ni mdau na mshiriki wa mashindano haya. Ndiyo huo mgongano wa kimaslahi ulioshindwa kuufahamu.
Siandiki haya kwa mapenzi ya Yanga au kutaka kuwa mchambuzi huru, la hasha. Si aibu kwangu kutokuwa mchambuzi huru kwa sababu sijawahi na sitawahi kujinasibu au kutamani niwe hivyo. Naandika haya kwa sababu ndio uhalisia unaosahauliwa na baadhi yetu mnapovaa miwani ya vioo vizito vya kulazimisha upendeleo usiokiwapo na kuufumbia mkubwa na wa dhahiri zaidi.

1. Hoja ya upendeleo kwa Yanga ni subjective na inaweza kuanzia kujadiliwa wakati wowote ule. Inategema na hoja anazoleta mtu. Tatizo ni wewe
unapolazimisha tuihusishe na uchaguzi wa uwanja wa kuchezea mechi ya jana pekee bila kukumbuka kuwa michezo hii ilianza zamani na Yanga ni mojawapo ya timu zilizonufaika zaidi kuchezea Uwanja wa Nyumbani isipokuwa jana.

2. Hoja ya kulazimisha watu watoe maoni baada ya kuangalia marudio ya picha TV haina mashiko. Kwani wewe unaamini wote wanaosema ile ilikuwa offside walikuwa wanatazama kupitia TV? Pili, mnaosema lilikuwa bao halali ninyi mnatumia marudio gani ya picha ya TV?Ni sahihi kulaumu wanaopinga bila kupata picha za marudion za TV huku ukiunga mkono wanaosema hapakuwa na offside bila na wao pia kutumia picha za Tv? Sitarajii reasoning ya aina hii kwa mtu objective.

3. Hoja yako ya tatu, nilishasema sina maoni kwa sababu haina uhusiano na mchezo au kilichotokea jana huko Tanga.
Na pia sio somo husika hapa.

4. Kushangaa kwako mimi kuunga mkono hoja ya uhuni wa mashabiki wa jana ndio kunazidi kuniaminisha kuwa wewe hauko objective katika hili. Unadhani mimi nitapinga kila kitu for the sake ya kupinga? Halafu hebu kagua vizuri kabla ya wewe kuandika hoja yako kama mimi nilikuwa nimeshatoa maoni. Hoja zako laini ndio zimenishangaza na kunivuta jukwaani. Na angekuwa ni mtu mwingine kaandika yawezekana nisinge comment chochote lakini sio wewe niliyetegemea hoja zenye kufikirisha zaidi

5. Hilo la mwamuzi kutumia 'akili' katika makosa makubwa na ya wazi ndio palipo na uvundo. Hii akili ya mtu mmoja akicheza rafu anapewa kadi stahili, mwinge mwamuzi anatumia kiachoitwa akili, ndipo palipo na jipu. Unadhani walioweka sheria za mchezo hawakujua kuna akili? Mwisho wa kutumia akili ni wapi? Hoja ya mwamuzi kuwepo au kutokuwepo kwenye tukio haina maana, maana mwamuzi anapaswa kufuata au kutazama mpira uliko. Na kama kwa mfano tuamini hakuona kwa nini alitoa kadi ya njano?
 
Leo nimeshindwa kuvumilia
waliotazama pambano la leo la Yanga na Coastal mtakuwa mashahidi

Goli la kwanza la Yanga offside ya wazi

halafu mchezaji wa Yanga mmoja akaenda 'kulipiza'
faulo mbaya sana ya makusudi kabisa akapewa kadi ya njano
badala ya nyekundu moja kwa moja

halafu Yanga goli la pili mchezaji wake aliushika kwa mkono
kwanza mpira......

Imesemwa mara nyingi Yanga inabebwa
lakini wahusika hawataki kusikia..kukweli hamuisaidii
mnazidi kuturudisha nyuma.....na ndo maana timu zetu zikienda nje
matokeo yanajulikana kabla.....

Kuna mechi Ya Ligi ya Yanga na Coastal pia ambapo Yanga alifungwa bao 2 bila
cha kushangaza refa akaongeza dakika kumi nzima
huku hakukuwa na tukio lolote la kulipia muda....

Hizo ni mechi mbili tu nimezitaja lakini wote tunajua kinachotokea...

hamuisaidii Yanga...mnaiumiza tu kiukweli....

POLE SANA. HAMIA LIGI ZA UGANDA NA RWANDA NDANI YA AZAM TV. Tatizo si Yanga kubebwa bali ni Yanga kushinda. Pole tena
 
Muungwana anapokariri hoja hizo kwa hizo ilhali zimeshajibiwa, tena bila ya kujibu jawabu ya hoja hizo, na anapoamini kwamba yeye ni objective na bado anashindana na asiye objective, hapo unashindwa kujua yupi ni objective.
 
MPIRA WA TANZANIA NA CHUKI DHIDI YA YANGA

Young Africans Sports Club, maarufu kama Yanga, ndio timu pekee Tanzania na Ukanda mzima wa Afrika Mashariki iliyobaki kwenye michuano ya vilabu Afrika. Licha ya kutokuwa na pesa, kama zilivyo klabu zingine zinazoitwa "tajiri" (mi naziita klabu zinazotumia pesa lukuki bila mpangilio ili kutafuta mafanikio ya soka), Young Africans kwa miaka ya hivi karibuni imekuwa ikifanya kila njia kuboresha timu yao uwanjani ili kutoa upinzani wa kweli kwa vilabu vikubwa Afrika.

Wala haiitaji kuwa mtaalamu wa soka aliyebobea wala kuwa kocha mwenye vyeti vya ngazi ya juu za soka, wala kuwa na PhD kuliona hili, matokeo yake ya uwanjani sambamba na uchezaji wake kwa maana ya kiwango chake, viwango vya wachezaji mmoja mmoja, wajuzi na wataalamu wa soka walioajiriwa, kwa maana ya kocha wake na benchi lake zima la ufundi, vinadhihirisha na kuongea ubora wa klabu hiyo nje na ndani ya uwanja.

Ni ufundi na utaalamu tu wa soka, na sio kingine. Matokeo mazuri mfululizo wanayoyapata ndani ya uwanja, uchezaji mzuri wa kiwango cha juu mno wanaoonesha, ubora wa wachezaji wake unaoimarika siku baada ya siku, bila kusahau ubora wa waalimu wa timu hiyo unaodhihirika siku baada ya siku, vyote kwa pamoja vimekuwa ni MWIBA MCHUNGU SANA kwa watu wanaokesha USIKU NA MCHANA kuifanyia na kusambaza chuki mbaya dhidi ya Yanga.

Tena ni zile chuki za kukerwa na mazuri ya mwenzio. Ni ile roho ya kunguni imewatawala, kiasi kwamba wakilala wakiamka wanawaza leo waandike nini baya kuhusu Yanga. Wameshindwa kabisa kupambana na Yanga kwa mbinu za utaalamu wa mpira, sasa silaha yao pekee iliyobaki ni kusambaza chuki, uongo fitna na majungu kuhusu kila wanachofanya Yanga.

KINACHOSIKITISHA ZAIDI ni kwamba, hizi chuki sasa zinaenezwa na kusambazwa na watangazaji wa televisheni, ambao nao sasa wameacha kufuata weledi wa kazi zao, wameamua kuwa "marefa wa videoni" na "wataalamu wa kanuni za soka" kwa kuangalia replay.

FURAHA yao ni kuona Yanga yenye migogoro, inayocheza soka la ovyo, inayofungwa ovyo ovyo na kila timu, wakitegemea kwamba timu wanazoshabikia zitaonekana bora zaidi, na pia itawafanya wapate cha kuongea wakijifanya wanajua kutoa hoja nzuri za kujenga. Haitoshi, timu zao kwa sasa zina matokeo mabaya mfululizo, na zinaonekana wazi kuachwa mbali mno kiuchezaji na Yanga.

Badala ya kujikita kutatua matatizo yao, yanayokuwa siku baada ya siku, wamejikita kuishambulia Yanga kwa nguvu zote, kama vile Yanga ndio inawafungisha au inawafanya wafanye madudu yao.

Kesho, keshokutwa tunatafakari ushiriki wetu kimataifa, timu ya Taifa, tunaanza kutafuta mchawi, huku tukijisahaulisha kwamba wachezaji hao wa timu ya Taifa wanatoka huku huku kwenye vilabu ambavyo tunavisukia majungu, porojo, fitna na uongo mtupu. Na hata inapotokea waamuzi wanafanya makosa viwanjani, lawama, fitna, majungu na visa vyote vinaangukia kwa Yanga.

Haijaanza jana wala juzi, hizi chokochoko zimeanza siku nyingi sana, na jana mechi dhidi ya Coastal Union ilikuwa ni kujua tu kundi kubwa la watu wenye chuki dhidi ya Yanga. Walianza kumshambulia Mwenyekiti Manji, wakijua ndio moja ya msingi mkubwa wa amani na kutulia kwa klabu na wanachama wake. Ndio moja ya nguzo muhimu ya uimara wa timu ndani na nje ya uwanja. Wameshindwa huko, sasa wamekuja viwanjani.

Wanataka kuvuruga saikolojia ya wachezaji, kuwavuruga waamuzi na kuwachochea mashabiki kufanya vurugu viwanjani, kwa kisingizio tu cha kile wanachokiita YANGA INABEBWA!!

Yale matukio ya waamuzi na wachezaji wa Yanga kupigwa mawe jana ilikuwa ni furaha nzito na kubwa sana kwao.

NDIO, NI FURAHA KUBWA KWAO!! Sasa wameshindwa kucheza mpira, wanachochea na kutetea watu wanaofanya vurugu viwanjani. Eti ndio faida ya kubeba timu. Ila matukio kama haya yoote, wakifanyiwa Yanga, wanaziba masikio na macho. Wanasema ndio sehemu ya mchezo.

NAWAKUMBUSHA TU KWAMBA, KAMWE HUWEZI KUWA NA AMANI KWA KUHARIBU AMANI YA MWINGINE. HUWEZI KUPATA MAFANIKIO KWA KUJARIBU KUZIBA AU KUVURUGA NJIA YA MAFANIKIO YA MWINGINE.

Niwakumbushe na kuwatahadhalisha pia WanaYanga wote kwamba, kamwe HAKUNA ADUI YAKO ANAYEWEZA KUKUOMBEA AU KUKUTAKIA au AKAYAPENDA MAZURI YAKO. Haipo popote kwenye maisha.

Hizi kelele wanazopiga za YANGA INABEBWA sio kwamba wanawapenda au wanaipenda sana timu, sio kwamba wanataka kuijenga timu iwe imara zaidi, sio kwamba wana uchungu na timu yenu kama nyie, lengo lao kuu ni moja tu . . . . . MVURUGANE, MSHAMBULIANE, MKOSE TIMU IMARA, MPATE MIGOGORO, NA HATIMAYE MKOSE KABISA RAHA kama ambavyo wao wanavyokosa raha kutokana na timu zao kuwa mbovu.

Wanajua kwamba, bila nguvu za fitna, majungu, porojo porojo na fugisu figisu itakuwa ngumu sana wao kuvunja UFALME WA YANGA KWENYE SOKA LA TANZANIA, maana viwanjani hawawezi tena.

Hawa watu wa majungu na fitna wapo kila sehemu siku hizi, kwenye televisheni na redio vipindi vya michezo, kwenye mitandao ya kijamii, wenyewe wakijivika vilemba vya WACHAMBUZI WA SOKA WASIOEGEMEA UPANDE WOWOTE kumbe mioyoni mwao wana ROHO YA KUNGUNI wakikusudia kuwachota mawazo yenu ili mkubalianae nao na mwisho muichukie timu yenu.

AMKA MWANA YANGA, PAZA SAUTI. USIKUBALI KUANGALIA TIMU YAKO PENDWA INASHAMBULIWA. PAZA SAUTI KUKATAA FITNA ZOTE NA MAJUNGU.
 
Ile ya Oscar Joshua ilikuwa red card kabisa lakini sijui refa kwa mapenzi yake kwa yanga akauchuna Na kutoa yellow. Jana mbeleko ilizidi kwa yanga.
 
Ile ya Oscar Joshua ilikuwa red card kabisa lakini sijui refa kwa mapenzi yake kwa yanga akauchuna Na kutoa yellow. Jana mbeleko ilizidi kwa yanga.
Na yule aliyemuumiza mchezaji wa yanga kutoka Niger mbona hammuongelei, alitakiwa apewe kadi ya blue? Mbona simba mnauumia sana yanga anavyoshinda

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app
 
Na yule aliyemuumiza mchezaji wa yanga kutoka Niger mbona hammuongelei, alitakiwa apewe kadi ya blue? Mbona simba mnauumia sana yanga anavyoshinda

Sent from my TECNO 7C using JamiiForums mobile app

Mkuu, hakuna la ajabu. Man U walipitia hayo enzi yao. Barcelona ndiyo hayo hayo na bado yanaendelea. Ukiwa juu, tegemea kelele za walio chini. Hakuna namna nyingine. Inabidi kuzoea tu.
 
Leo nimeshindwa kuvumilia
waliotazama pambano la leo la Yanga na Coastal mtakuwa mashahidi

Goli la kwanza la Yanga offside ya wazi

halafu mchezaji wa Yanga mmoja akaenda 'kulipiza'
faulo mbaya sana ya makusudi kabisa akapewa kadi ya njano
badala ya nyekundu moja kwa moja

halafu Yanga goli la pili mchezaji wake aliushika kwa mkono
kwanza mpira......

Imesemwa mara nyingi Yanga inabebwa
lakini wahusika hawataki kusikia..kukweli hamuisaidii
mnazidi kuturudisha nyuma.....na ndo maana timu zetu zikienda nje
matokeo yanajulikana kabla.....

Kuna mechi Ya Ligi ya Yanga na Coastal pia ambapo Yanga alifungwa bao 2 bila
cha kushangaza refa akaongeza dakika kumi nzima
huku hakukuwa na tukio lolote la kulipia muda....

Hizo ni mechi mbili tu nimezitaja lakini wote tunajua kinachotokea...

hamuisaidii Yanga...mnaiumiza tu kiukweli....
umeona eeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!
 
tatizo lako ni kwamba wewe ni wakitaifa tena wa mchangani. Tuache sie makombe yote ni yetu ila hamjachelewa enda kwa kombe la dr mwaka
kwa mtindo huu,nje ni kichapo kwa kwenda mbele.
 
Leo nimeshindwa kuvumilia
waliotazama pambano la leo la Yanga na Coastal mtakuwa mashahidi

Goli la kwanza la Yanga offside ya wazi

halafu mchezaji wa Yanga mmoja akaenda 'kulipiza'
faulo mbaya sana ya makusudi kabisa akapewa kadi ya njano
badala ya nyekundu moja kwa moja

halafu Yanga goli la pili mchezaji wake aliushika kwa mkono
kwanza mpira......

Imesemwa mara nyingi Yanga inabebwa
lakini wahusika hawataki kusikia..kukweli hamuisaidii
mnazidi kuturudisha nyuma.....na ndo maana timu zetu zikienda nje
matokeo yanajulikana kabla.....

Kuna mechi Ya Ligi ya Yanga na Coastal pia ambapo Yanga alifungwa bao 2 bila
cha kushangaza refa akaongeza dakika kumi nzima
huku hakukuwa na tukio lolote la kulipia muda....

Hizo ni mechi mbili tu nimezitaja lakini wote tunajua kinachotokea...

hamuisaidii Yanga...mnaiumiza tu kiukweli....
MPWA UARABUNI MLITUBEBA WA MATOPENI???AU UKUONA LILE SAMBA LA HAJA TOKA KWA MDUTCH
 
Back
Top Bottom