Mnaoishi na watoto warefu mnakabiliana nao vipi wanapogoma kuadhibiwa kwa kipigo? Wamewahi kuwabadilikia?

Mnaoishi na watoto warefu mnakabiliana nao vipi wanapogoma kuadhibiwa kwa kipigo? Wamewahi kuwabadilikia?

NetMaster

JF-Expert Member
Joined
Sep 12, 2022
Posts
1,454
Reaction score
4,925
Walezi wa kiume iwe ni baba, mjomba, baba mkubwa, n.k, huwa ndio wanategemewa kusimamia kitengo cha kutia displini hasa utukutu ukizidi, hata walezi wa kike wakiona toto limekuwa tundu wanamwambia msubiri baba yako aje, mjomba wako aje, n.k.

Sasa basi unakuta sometimes kijana mdogo yupo hata form 2 kashapanda hewani kumzidi baba yake, mjomba wake, bamdogo wake, n.k.

Hali hii imewahi kuwaathiri katika kuchukua tagadhari za kutoa adhabu hasa za viboko kwa hao watoto?
 
Walezi wa kiume iwe ni baba, mjomba, baba mkubwa, n.k, huwa ndio wanategemewa kusimamia kitengo cha kutia displini hasa utukutu ukizidi, hata walezi..

Kipigo? Ukianza mpiga mtoto mapema, ujue azabu lazima ikue na mtoto, sasa kama umeanza mpiga ana mwaka, akifika 14 azabu itaongezeka kuwa nini? Labda kifo...

Kwepa kuazibu mtoto, mfano mimi watoto wangu nikigomba tu wanatoa machozi, sasa kwa nini ni wachape, ni wasikivu haswa...
 
Huwa tunaanza kwa shambulio la kushtukiza, unafungua dojo kwa buti moja la kwenye ugoko anashusha uso mwenyewe then unamchezeshea vifuti vya maana na mtama flani wa Adam Mchovu then unamtoa wenge kwa roba/kabali moja matata mithili ya kibaka mpiga roba wa Mwanjelwa-Mbeya, akijigeuza fresh anajikuta kashafungwa kudu na hapo unaendelea naye na mabuti ya kwenye mbavu mpaka mama yake atakapoanza kulia ndiyo unamuachia.
 
Aisee mbona upo weak hivo mkuu! Mtoto hata awe kama John Cenna ni mtoto tu na kichapo atakula
 
Back
Top Bottom