Jamani msikubali kuibiwa pale Buguruni. Mbali ya kutumia vipimo feki, hata mabao zao mara nyingi zinakuwa za kuchovya tu kwenye dawa. Wadau anayetaka mbao imara na kwa bei isiyokuwa na wizi aende pale Mabibo Kiwanda kwenye yard ya Sao Hill branch ya Dar Es Salaam. Wewe mwenyewe utapenda.
Achana na hao matapeli.
Tiba
Yard ya sao hill iko sehemu gani mkuu? Tafadhali tusaidie kwa kutoa maelezo ya kutosha.
mmmh hadi nifikie hatua ya kununua mbao ntakuwa nimeshasahau hii alert ngoja niprint niibandike ukutani.
Mkuu Investa.tz,
Kwenye maelezo yangu nimejaribu kueleza hiyo yard ya Sao Hill iko wapi hapo Dar. Kwa faida yako na wengine, ukitokea Buguruni kuelekea Ubungo, ukiisha vuka reli kwa mbele kidogo mita kama 500 kuna msikiti upande wa kushoto. Ukiupita huo msikiti kuna baa moja hivi ambayo jina lake silikumbuki lakini next to hiyo Bar ndipo ilipo hiyo Yard ya Sao Hill. Ukifika eneo hilo muulize mtu yeyote atakuonyesha!!!!!!
Tiba
Hahaha si kwa enzi ya magufuli (kwasauti ya mwana fa)mmmh hadi nifikie hatua ya kununua mbao ntakuwa nimeshasahau hii alert ngoja niprint niibandike ukutani.