Mnaojenga kuweni makini mnaponunua mbao, kuna wizi wa kutisha!

Mnaojenga kuweni makini mnaponunua mbao, kuna wizi wa kutisha!

Buguruni sio sehemu ya kununua mbao!
 
Yard ya sao hill iko sehemu gani mkuu? Tafadhali tusaidie kwa kutoa maelezo ya kutosha.
Jamani msikubali kuibiwa pale Buguruni. Mbali ya kutumia vipimo feki, hata mabao zao mara nyingi zinakuwa za kuchovya tu kwenye dawa. Wadau anayetaka mbao imara na kwa bei isiyokuwa na wizi aende pale Mabibo Kiwanda kwenye yard ya Sao Hill branch ya Dar Es Salaam. Wewe mwenyewe utapenda.

Achana na hao matapeli.

Tiba
 
Yard ya sao hill iko sehemu gani mkuu? Tafadhali tusaidie kwa kutoa maelezo ya kutosha.

Mkuu Investa.tz,

Kwenye maelezo yangu nimejaribu kueleza hiyo yard ya Sao Hill iko wapi hapo Dar. Kwa faida yako na wengine, ukitokea Buguruni kuelekea Ubungo, ukiisha vuka reli kwa mbele kidogo mita kama 500 kuna msikiti upande wa kushoto. Ukiupita huo msikiti kuna baa moja hivi ambayo jina lake silikumbuki lakini next to hiyo Bar ndipo ilipo hiyo Yard ya Sao Hill. Ukifika eneo hilo muulize mtu yeyote atakuonyesha!!!!!!

Tiba
 
POLENI sSAAANa kwa wale ambap mwaka huu ndio wanajua hilo au walikuwa hawajui...SIO BUGURUNI TU poote...Usimuamini mtu kila mtu anataka akuvune jasho lako bure tu...tuwe makini na binadamu..WATZ tuache uchakachuaji...
mmmh hadi nifikie hatua ya kununua mbao ntakuwa nimeshasahau hii alert ngoja niprint niibandike ukutani.
 
mimi pia nina uzoefu wa biashara hiyo na ndio inaniweka mjini,ofisi yangu ipo ubungo riverside na nimefanya biashara hiyo mwaka wa tano sasa,ki ukweli wanaoharibu biashara hii ni madalali,na mtu kama akikubali kumuibia mteja huyo si mfanya biashara,na ngoja niwape ukweli mmoja ambao hamjaufahamu,biashara nyingi za mbao pale buguruni wauzaji sio maboss,wao huwa wanawakabidhi wafanyakazi ambao nao hushirikiana na madalali kuwaibia wateja,tatizo kubwa ndo liko hapo,na mwisho wa siku biashara nyingi pale zinaishia kufa.
 
Mkuu Investa.tz,

Kwenye maelezo yangu nimejaribu kueleza hiyo yard ya Sao Hill iko wapi hapo Dar. Kwa faida yako na wengine, ukitokea Buguruni kuelekea Ubungo, ukiisha vuka reli kwa mbele kidogo mita kama 500 kuna msikiti upande wa kushoto. Ukiupita huo msikiti kuna baa moja hivi ambayo jina lake silikumbuki lakini next to hiyo Bar ndipo ilipo hiyo Yard ya Sao Hill. Ukifika eneo hilo muulize mtu yeyote atakuonyesha!!!!!!

Tiba

Hiyo ndiyo Bongo yetu.... Ukiona mwembe mkubwa kata kushoto halafu kuna krossi kuruba halafu bombii nyumbii. Huwezi kupotea.

Kazi kweli kweli.
 
msaada anayejua wapi nitapata mabanzi kwa hapa dar!..na bei ipo vip?
 
Mkuu maichrim, Buguruni hiyo ndio kazi yao, ukifika wanakukimbia, ukitoa tape measure yako utaona wanaondoka mmmoja baada ya mwingine, maana zile za kwao wanakuwa wamezikata ili kupunguza vipimo. Aidha, kule kwenye mabati ndio kubaya zaidi, utauziwa 32G kuwa ni 30 G au 30 kuwa ni 28G na vingine vingi tu. Kuwa makini maeneo hayo, na usirihusu fundi wako akafahamu kuwa unaenda kununua kitu, then anakupeleka, wengi wanakula deal.
 
Last edited by a moderator:
Town hamna mashamba huku lami tupu akili nyingi kijijini watu huku Manjegeka msingi maneno
 
Last edited by a moderator:
...nenda na fundi wako na usimpe nafasi ya kuongea nao,ukiweza kagua tapemeasure yao,mchina ametengeneza maalum kwa ajili ya huu wizi ukiiona ni mpyaaa,kumbe famba...
 
Mimi mwenyewe niliuziwa mbao ambazo wao wanasema ni treated .Baada ya mwaka mmoja zimeanza kiuliwa na wadudu.Kwa hiyo kuweni makini na baadhi ya wauzaji.
 
Back
Top Bottom