Simbamteme
JF-Expert Member
- Sep 10, 2011
- 804
- 2,131
Wasalaam,
Naomba tu kutoa wito kwa wale wenzangu na mimi tunaojidunduliza ili kujenga nyumba za kuishi na familia zetu kuwa MAKINI sana na WATU tunaowaweka wawe walinzi wa nyumba zetu. Kuna tukio lilitokea hapa kitaani likaniacha Mimi na baadhi ya majirani tulioshuhudia tukio hilo kubaki midomo wazi
TUKIO LENYEWE:
Hapa ninapoishi nipo tokea Mwaka 1999 nikiwa mdogo sana..kuna nyumba kama ya 5 hivi kutoka hapa ninapokaa kuanzia mwaka huo 1999 ilikuwa imejengwa ila haikuwa imemalizika ndani madirisha na milango vilikwepo
Tokea mwaka 1999 hiyo nyumba ilikuwa hivyo hadi mwaka 2005 hivi kuendelea, mwenye nyumba akaizunguishia ukuta (ndani ilikuwa vilevile)
Ilikaa hvyo kwa miaka mingi kidogo then ikaanza kukarabatiwa na kufanyiwa finishing kali ikapendeza kweli
Sasa mwezi kama mmoja hivi uliopita tulisikia vurumati ndani ya hiyo nyumba, watu kutukanana, kugombana kwa sauti kali, ikabidi tujisogeze kujua nini shida
Ndipo yule jamaa aliekuwa anafoka kutuambia kuwa ile nyumba ni yake na huyo tuliemdhania kwamba anamiliki ile nyumba aliwekwa na huyo jamaa kama mlinzi tu
Ila baada tu ya kumuweka huyo jamaa kama mlinzi ALISAHAU kabisa kuhusu ile nyumba na hakuwahi kukumbuka kama ana ile nyumba mpaka alipobahatika kwenda kuombewa huko kwenye makanisa ya walokole (though alienda kwa shida nyingine).
Dunia ina mambo mengi sana, TUWENI MAKINI JAMANI