Mnaojenga nyumba, kuweni makini na watu mnaowaomba wawalindie nyumba zenu

Wasalaam,

Naomba tu kutoa wito kwa wale wenzangu na mimi tunaojidunduliza ili kujenga nyumba za kuishi na familia zetu kuwa MAKINI sana na WATU tunaowaweka wawe walinzi wa nyumba zetu....
Hata Viwanja Mkuu, ukienda kununua ukakuta mmiliki ni wale vikongwe, basi utalipia halafu mwiso wa siku ukiondoka unasahau kama ulinunua Kiwanja hadi eneo husika
 
Habari za jumapili wakuu.

Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza nmekutana na thread moja humu jf.

Kwamba mlinzi unayemuweka kulinda nyumba yako anaweza kukuchezea(kukuloga ukasahau nyumba yako) kiukweli sijawahi jua kitu kama hcho sasa wakuu naomba msaada ndio niko process za kutafuta mlinzi niangalie kitu gani? kabila, umri, kiimani: niko partially siko deep sana
niko mbeya mjini
 
Soma hiyo.

Mpaka muda huu tunapigana majini mimi na aliyekuwa akinitizamia nyumba yangu, nashukuru ninakwenda vizuri.
[emoji23][emoji23][emoji23]mama.e...tuma vitu,tuma vitu mkuu
 
Habari za jumapili wakuu.

Kweli usilolijua ni kama usiku wa giza nmekutana na thread moja humu jf.

Kwamba mlinzi unayemuweka kulinda nyumba yako anaweza kukuchezea(kukuloga ukasahau nyumba yako) kiukweli sijawahi jua kitu kama hcho sasa wakuu naomba msaada ndio niko process za kutafuta mlinzi niangalie kitu gani? kabila, umri, kiimani: niko partially siko deep sana
niko mbeya mjini
Jiandae na kesi ...maana wakati wa kumtoa haitakua rahisi. Wengi wanakuja na wake zao. Pia, watoto wao wanawaamishoa shule jirani
 
Unajua watu wengi hawafahamu kuwa wachawi wapo mjini mfano angalia nyumba nyingi ukianza kujenga ikafikia sehemu ya finishing ukaweka Mmasai mlinzi au Mmakonde na wengine ujue nyumba hiyo huwezi kuimalizia itakaa hivyo hivyo mda mrefu utakuwa umeisahau kabisa.

Mfano mimi nina nyumba buguruni barabara kubwa nina fremu 4 za maduka zipo tupu niliwahi kumpangisha mdada mmoja fremu mmoja. Na zingine nikawa sijapangisha kwa sababu nilikuwa naishi nje ya nchi ila kila 3 month nakuja Tanzania huyu mdada alipanga kwa miaka 4 lakini ajabu kila watu wakija kutaka fremu nilikuwa nakataa kupangisha moyo hautaki kabisa mdada huyu akapata fremu nyumba ya jirani akahama lakini mpaka leo sijapangisha zaidi ya miaka 10 fremu zote 4 na watu wananiijia kunibembeleza kupanga moyo unakataa mtaa wangu huu umechangamka sana maduka majirani wananishangaa sana kwa nini sipangishi na mpaka sasa nina shida ya pesa kulipa school fees ya mwanangu form 5.

Napata tabu kupata pesa na fremu ninazo na watu wanataka kupanga kila fremu laki 250 lakini nakataa naomba mniombee kila anaesoma maana kazi niliacha mda mrefu sana baada ya kuumia na umri pia.mimi najijua kuwa huyo mdada kanifanyia maana kila akiniona anatabasamu nakuniuliza hujapangisha tu au nirudi mimi
Nenda kwa Mwamposa
 
huyo hana tofauti na yule aliyenunua kiwanja ila kila akienda site hakumbuki kipo location ipi,...
 
Tena mkuu umenizinduwa usingizini, wacha nijiandae nielekee Kibaha. Nina jambo langu kule lakini sijakanyaga huu mwaka wa 5 tangu 2015 sijafika pale.

Huyu bibi jirani niliyemkabidhi eneo langu anitizamie naishia kuongea nae kwenye Simu tu miaka yote.

Kila nikitaka kwenda nasita sana.

Leo nakwenda na sijuwi kama nitakwenda kweli naona moyo bado mzito sana.
Tupe mrejesho mkuu[emoji1]
 
Unajua watu wengi hawafahamu kuwa wachawi wapo mjini mfano angalia nyumba nyingi ukianza kujenga ikafikia sehemu ya finishing ukaweka Mmasai mlinzi au Mmakonde na wengine ujue nyumba hiyo huwezi kuimalizia itakaa hivyo hivyo mda mrefu utakuwa umeisahau kabisa.

Mfano mimi nina nyumba buguruni barabara kubwa nina fremu 4 za maduka zipo tupu niliwahi kumpangisha mdada mmoja fremu mmoja. Na zingine nikawa sijapangisha kwa sababu nilikuwa naishi nje ya nchi ila kila 3 month nakuja Tanzania huyu mdada alipanga kwa miaka 4 lakini ajabu kila watu wakija kutaka fremu nilikuwa nakataa kupangisha moyo hautaki kabisa mdada huyu akapata fremu nyumba ya jirani akahama lakini mpaka leo sijapangisha zaidi ya miaka 10 fremu zote 4 na watu wananiijia kunibembeleza kupanga moyo unakataa mtaa wangu huu umechangamka sana maduka majirani wananishangaa sana kwa nini sipangishi na mpaka sasa nina shida ya pesa kulipa school fees ya mwanangu form 5.

Napata tabu kupata pesa na fremu ninazo na watu wanataka kupanga kila fremu laki 250 lakini nakataa naomba mniombee kila anaesoma maana kazi niliacha mda mrefu sana baada ya kuumia na umri pia.mimi najijua kuwa huyo mdada kanifanyia maana kila akiniona anatabasamu nakuniuliza hujapangisha tu au nirudi mimi
Aliyerogwa hajuigi kama amerogwa
 
Back
Top Bottom