Mnaojenga nyumba, kuweni makini na watu mnaowaomba wawalindie nyumba zenu

Mnaojenga nyumba, kuweni makini na watu mnaowaomba wawalindie nyumba zenu

Wakati mwingine ni uvivu tu wa kutingwa na majukumu ya kila siku......na kwa bahati mbaya siku unayotaka kwenda ndio siku ya kupumzika na mwili umechoka........


Uvivu au uchovu huo uwe kuanzia Januari hadi December? Mwaka wa kwanza, wa pili, tatu na kuendelea?

Cha ajabu unaweza kuta kama una eneo lingine la mbali ambalo hujarogwa utajikuta kule mbali unaendaga lakini hapo karibu unaparuka!
 
Wengine wanamashamba makubwa makubwa bagamoyo na mikoani wamepanda mazao kama vile nazi na maembe lakini hawafaidiki nayo wenyewe wananunua nazi kama wengine mtaani na maembe kama wengine wasokuwa na mashamba[emoji108][emoji108]

Waangalizi wa hayo mashamba wanapiga hela ile mbaya!
 
Atakua na nyumba nyingi huyo jamaa.

Masikini/choka mbovu mwenye kuishi kwny ka-banda ka-mbwa ka kupanga huko uswazi hawezi kusahau nyumba yake anayoijenga kamwe.
Shukuru kwamba hujawah kurogwa.dunia ina mengi Zaid ya uyajuayo
 
Tena mkuu umenizinduwa usingizini, wacha nijiandae nielekee Kibaha..
Nina jambo langu kule lakini sijakanyaga huu mwaka wa 5 tangu 2015 sijafika pale..

Huyu bibi jirani niliyemkabidhi eneo langu anitizamie naishia kuongea nae kwenye Simu tu miaka yote.

Kila nikitaka kwenda nasita sana.

Leo nakwenda na sijuwi kama nitakwenda kweli naona moyo bado mzito sana....

Mkuu tunaomba mrejesho wa safari yako kama ulifanikiwa kwenda
 
Bagamoyo mwisho[emoji16][emoji16][emoji16].
Kila dalali ana mganga wake..
Unaweza ukauziwa makaburi na ukatoa hela

[emoji38][emoji38][emoji38][emoji38]mkuu umenichekesha sana

Kunywa moja apo nakuja kulipia
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] nimecheka saaana. Nimekumbuka enzi hizo kuna mwenye nyumba aliipangisha nyumba yake yote kwa familia fulani. Ila baada ya kupita kipindi fulani na kodi ya mpangaji kuisha, mpangaji akawa halipi kodi. Mwenye nyumba akaamua kumfata kule kule. Ila kila akienda, anapotea njia, atazungukaa wee karibia siku nzima alaf anaamua tu kurudi home. Hiyo hali ikajirudia karibia miez 4 mfululizo, hadi siku hiyo akaamua kwenda na mganga, ndio akabahatika kuiona njia.

Sent from my SM-G955U using JamiiForums mobile app

Hii kiboko
 
Kuamini kwenye nguvu za giza lazima kwanza nawe uwe Mshirikina.

Pili kuamini kwamba binaadamu mwenzako mnayefanana kwa kila kitu kwamba ana uwezo wa kuhusika na hisia au nafsi yako ni kumtukuza kulikopitiliza.

Kama huyo anayetuhumiwa ana huo uwezo wa aina hiyo kwa nini asiweze kupata mali tena kwingine?, au la basi angekuwa na mali zaidi ya hiyo.

Tunaposema kupambana na umasikini, ujinga na maradhi, basi tukumbuke ya kuwa huwezi kuondoa ujinga kama bado una mamilioni ya Watu wanaoamini kwenye mambo ya kusadikika. yaliyokosa uhalisia.
TruthLover anasema

Hapo umakini wa kibinadamu hautasaidia lolote.Yesu hakuja duniani kuzurura. Alikuja akijua fika tunamuhitaji sana,hasa kwa mambo yaliyo nje ya uwezo wetu wa kibinadamu kama haya.

Haya sio maneno ya kupuuza hata kidogo. Ima unaamini uchawi ima lah!
 
Nimechekaa sana, yaani usahau nyumba yako? Basi jamaa mambo yalikuwa super au alikuwa chizi

huwa wanarogwa, mother yangu pia amewahi kunisimulia story kama hii ilitokea Kanda ya ziwa, ila utofauti ni kidogo
yule bwana alikuwa anakumbushwa na mkewe kuhusu nyumba ila anamshushia mkewe kichapo hatari,kumbe alirogwa asahau nyumba yake ambayo ilikuwa imeshakamilika kila kitu mpaka umeme na maji
 
nina jambo langu vikindu na makulunge bagamoyo, sijaenda mwaka wa pili unaenda huu, ngoja nijitahidi kufika isje kuwa kijini msahaulifu kaniingia...
 
Wasalaam,

Naomba tu kutoa wito kwa wale wenzangu na mimi tunaojidunduliza ili kujenga nyumba za kuishi na familia zetu kuwa MAKINI sana na WATU tunaowaweka wawe walinzi wa nyumba zetu

Kuna tukio lilitokea hapa kitaani likaniacha Mimi na baadhi ya majirani tulioshuhudia tukio hilo kubaki midomo wazi

TUKIO LENYEWE

Hapa nnapoishi nipo tokea Mwaka 1999 nikiwa mdogo sana..kuna nyumba kama ya 5 hivi kutoka hapa ninapokaa kuanzia mwaka huo 1999 ilikuwa imejengwa ila haikuwa imemalizika ndani madirisha na milango vilikwepo

Tokea mwaka 1999 hiyo nyumba ilikuwa hivyo hadi mwaka 2005 hivi kuendelea, mwenye nyumba akaizunguishia ukuta (ndani ilikuwa vilevile)

Ilikaa hvyo kwa miaka mingi kidogo then ikaanza kukarabatiwa na kufanyiwa finishing kali ikapendeza kweli

Sasa mwezi kama mmoja hivi uliopita tulisikia vurumati ndani ya hiyo nyumba, watu kutukanana, kugombana kwa sauti kali, ikabidi tujisogeze kujua nini shida

Ndipo yule jamaa aliekuwa anafoka kutuambia kuwa ile nyumba ni yake na huyo tuliemdhania kwamba anamiliki ile nyumba aliwekwa na huyo jamaa kama MLINZI tu

Ila baada tu ya kumuweka huyo jamaa kama mlinzi ALISAHAU kabisa kuhusu ile nyumba na hakuwahi kukumbuka kama ana ile nyumba mpaka alipobahatika kwenda kuombewa huko kwenye makanisa ya walokole (though alienda kwa shida nyingne)

Dunia ina mambo mengi sana, TUWENI MAKINI JAMANI
Hayo mambo ni huko kwenu tu bara ambako hakuna ubinadamu, hapa kwetu ni shwari hakuna kitu namna hiyo
 
Hapo hapahitaji umakini! Utakaaje miaka yote hiyo bila kwenda kutembelea eneo lako?
 
Unajua watu wengi hawafahamu kuwa wachawi wapo mjini mfano angalia nyumba nyingi ukianza kujenga ikafikia sehemu ya finishing ukaweka mmasai mlinzi au mmakonde na wengine ujue nyumba hiyo huwezi kuimalizia itakaa hivyo hivyo mda mrefu utakuwa umeisahau kabisa..
yaani nimesoma hii habari yako mwisho nimekuona mjingasana, unajaribu kuleta wazo lako hapa lakini tatizo unalo mwenyewe halafu unasingizia kurogwa sijuw upumbav gani yaani watu kama nyinyi wenye theory mgando kama hii mimi nawakwepa sana, wewe endelea bora endelea na mawazo yako finyu ukiamini kuna jambo baya umefanyiwa. poor thinker
 
Imenitokea hii kitu mkuu Maisha sometimes usipokuwa makini umekwisha.... Kipindi nasoma o-level 2009 mzee alinipanga ameanza kunishushia mjengo mungu ni mwema mpaka 2012 akanipeleka kweli kitu kimesimama nakumbuka kauli yake akaniambia nategemea hapa ndipo utapokuja kuanzia maisha yako sasa katika harakati za finishing kuna jamaa(mmoja wa mafundi) alikuwa na familia mke na watoto wawili waliomba kukaa pale kwa muda huku finishing ikimaliziwa kiufupi huwezi amini since 2013 nyumba ilisahaulika kiujumla tukawa tunawekeza kwenye mambo mengine nimekuja kushtuka mwaka jana ndio kupambana namaliza huu mwaka nikiwa nahamia kwenye jengo langu lililotelekezwa katika harakati ya safari ya maisha.Binadamu Ishi Naye Kwa Akili. Asante Sana Mzee Wangu Mungu ni Mwema[emoji120]
 
Back
Top Bottom