Si tulipohamia tukawa hatulali usiku, Yaani nyumba kelele hatari, mara milango inafunguliwa Mara geti linabamizwa nk. Imechukua kama 4 years ikaisha.
Huyo tuliomuweka alikaa for 4 yrs, kila tukitaka kuhamia tunasita, tulihamia gafla. Ndio kuja kupata stori kwa Majirani kuwa alikua anajitapa eti hatutakuja kuhamia kamwe! Tukaambiwa waganga mbalimbali walikua wanashinda katika nyumba..
Afadhali ukodi kampun ya ulinzi kuliko Hawa wa mitaani...
Sasa hii ndo kali zaidi, Kuna jirani yetu eti kajenga tangu 1985. Ni mtu mzima, anakujaga anaikarabati nyumba anaondoka
Imagine nyumba zipo 2 ktk kampaundi moja hata hajazipanisha anayeishi ni Hawa wababu hahaha, nyumba nzuri mno.
Yaani watu humuonea huruma sana. Babu anayetunza kashaoa Mara 5 kazaa na watoto kibao hapohapo, mwenye nyumba anakuja na kuondoka yaani huwezi kuamini kabisa.