Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 1,679
- 2,123
Mungu ameruhusu tule nyama yoyote ya wanyama aliowaumba. Yesu ni Mungu, alipokuja hapa duniani aliidhinisha tule hata kitimoto🐖(nyama ya nguruwe).
Alitoa ruhusa hiyo katika Marko 7:14-23(BHN). Imeandikwa hivi:
Yesu aliuita tena ule umati wa watu, akawaambia, “Nisikilizeni nyote, mkaelewe. Hakuna kitu kinachoingia ndani ya mtu kutoka nje kinachoweza kumtia mtu unajisi. Lakini kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia mtu unajisi.” Mwenye masikio na asikie!
Alipouacha umati wa watu na kuingia nyumbani, wanafunzi wake walimwuliza maana ya huo mfano. Naye akawaambia, “Je, hata nyinyi hamwelewi? Je, hamwelewi kwamba kitu kinachomwingia mtu kutoka nje, hakiwezi kumtia unajisi, kwa maana hakimwingii moyoni, ila tumboni, na baadaye hutolewa nje chooni?” (Kwa kusema hivyo, Yesu alihalalisha vyakula vyote.)
Akaendelea kusema, “Kinachotoka ndani ya mtu ndicho kinachomtia unajisi. Maana kutoka ndani, moyoni mwa mtu, hutoka mawazo mabaya, uasherati, wizi, uuaji, uzinzi, uchoyo, uovu, udanganyifu, ufisadi, wivu, kashfa, kiburi na upumbavu. Maovu hayo yote yatoka ndani ya mtu, nayo humtia mtu unajisi.”
Ila kama kwa kula kwako nyama unamkwaza ndugu yako, acha mara moja.
Warumi 14:21 (NEN)
Ni afadhali kutokula nyama wala kunywa divai au kufanya jambo lingine lolote litakalomsababisha ndugu yako ajikwae.