Mnaokula Kitimoto, Kuleni "Kwa Raha Zenu," Yesu Ameruhusu

Mnaokula Kitimoto, Kuleni "Kwa Raha Zenu," Yesu Ameruhusu

14 Wale waliokuwa wakichunga hao nguruwe (NGURUWE walifugwa kibiashara na Wayahudi wenyewe waliopokea maagizo kutoka kwa Mungu) wakakimbilia mjini na vijijini kueleza yaliyotokea. Watu wakatoka kwenda kujionea mambo hayo.

15 Wakaja kwa Yesu, wakamwona yule mtu aliyekuwa amepagawa na pepo akiwa ameketi, amevaa nguo na pia akiwa na akili timamu. Wakaogopa. 16 Wale walioyaona mambo haya waliwaeleza wengine yaliyomto kea yule aliyekuwa na pepo na lile kundi la nguruwe. 17 Basi watu wakaanza kumwomba Yesu aondoke (kwa sababu ameleta uhaba wa kitimoto?) katika wilaya yao.
 
Hiyo ndo nyama gani tena?
Ni nyama ile inayoliwa chumbani na watu wawili wa jinsia tofauti wakiwa wamefunga milango ya vyumba vyao!.
Wengine ili kutaka majirani wasijue kwamba huko chumbani kuna nyama zinakulana hufungulia radio au television kwa sauti kubwa ili watu wanje wasijue kinachoendelea ndani!
Nadhani Binti sayuni kwa maelezo haya huna swali la nyongeza !😆😆😆.
 
wewe umesoma biblia gani?
soma hapa

Mambo ya Walawi 11:7-8
"Na nguruwe, kwa kuwa ana kwato zilizogawanyika, ni kweli, lakini hacheui; yeye ni najisi kwenu. Nyama yao msile, wala mizoga yao msiiguse; hao ni najisi kwenu."

2. Kumbukumbu la Torati 14:8
"Tena nguruwe, maana ana kwato zilizogawanyika, lakini hacheui, ni najisi kwenu; msile nyama yao, wala msiiguse mizoga yao."
3.Matendo ya Mitume 10:13-15
"Kisha sauti ikamjia, 'Ondoka Petro, uchinje ule.' Lakini Petro akasema, 'Hasha, Bwana, kwa maana sijakula kamwe kitu kilicho kichafu au najisi.' Sauti ikamjia mara ya pili, 'Vitu alivyo vitakasa Mungu, usiviite wewe najisi.'"

4.Marko 7:18-19
"Naye akawaambia, 'Hivi nanyi hamwelewi? Hamjui ya kuwa kitu chochote kinachoingia ndani ya mtu kutoka nje hakiwezi kumtia unajisi; kwa kuwa hakimwingii moyoni mwake, bali tumboni, kisha hutoka nje?' Hivyo alitangaza vyakula vyote kuwa safi."
 
Ni nyama ile inayoliwa chumbani na watu wawili wa jinsia tofauti wakiwa wamefunga milango ya vyumba vyao!.
Wengine ili kutaka majirani wasijue kwamba huko chumbani kuna nyama zinakulana hufungulia radio au television kwa sauti kubwa ili watu wanje wasijue kinachoendelea ndani!
Nadhani Binti sayuni kwa maelezo haya huna swali la nyongeza !😆😆😆.
Kumbe ndiyo mnavyofanyaga hivi Chief😁😁😁
 
Napitatuu
Someni hapo
 
Attachments

  • Screenshot_20250311-185633.jpg
    Screenshot_20250311-185633.jpg
    390.2 KB · Views: 1
  • Screenshot_20250311-185626.jpg
    Screenshot_20250311-185626.jpg
    423.2 KB · Views: 1
Walawi 11:7-8 Na NGURUWE kwasababu anazo kwato,ni mwenye miguu iliyopasuka kati,lakini hacheui,yeye ni najisi kwenu.Msile nyama yao wala msiguse mizoga yao.

Ila kwakua kitabu chenu huwa mnakifanyia Amendment kama katiba ya Ccm utakuja na jibu kuwa hiyo ilikua ni zamani ila sahivi mnaruhusiwa lakini cha ajabu maandiko hayo bado yapo.

Wazee wa kufanyia mabadiliko maandiko mara kwa mara ili muweze kufanya yale yanayofurahisha mioyo yenu, na jinsi Papa Francis alivyotoa kauli ya kubariki ndoa za jinsia moja kizazi cha mwaka 2097 kitakuta tayari maandiko yameruhusu tayari na hizo ndoa za jinsia moja
 
Napitatuu
Someni hapo
Asante! Shida Hawa wagalatia wakionyeshwa maandiko hayo husema agano la kale haliwahusu kwakuwa wao mamekombolewa kwa agano jipya!
Ndio maana maandiko yote waliyoyaleta kuhalalisha kitimoto wameyatoa ndani ya agano jipya!.
 
Ni nyama ile inayoliwa chumbani na watu wawili wa jinsia tofauti wakiwa wamefunga milango ya vyumba vyao!.
Wengine ili kutaka majirani wasijue kwamba huko chumbani kuna nyama zinakulana hufungulia radio au television kwa sauti kubwa ili watu wanje wasijue kinachoendelea ndani!
Nadhani Binti sayuni kwa maelezo haya huna swali la nyongeza !😆😆😆.
Ufunuo 21:8
Lakini waoga, wasioamini, wachafu, wauaji, wazinzi, wachawi, waabudu sanamu, pamoja na waongo wote, mahali pao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
 
Kwani wewe Binti sayuni ukitaka kula nyama hiyo huwa unailaje?! Hufungi milango ?! Watoto wakiingia je ?!😄😄😄
Waefeso 5:3:
"Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote, wala tamaa mbaya, kama iwapasavyo watakatifu." (Waefeso 5:3, SUV)
 
Kati ya mudi boy na yesu ni nani aliye alalisha ulaji wa kitimoto ? Kama ukiniuliza mimi ili swali basi jibu langu lingekuwa ni Muhammad....yesu akualamisha chakula chochote wala kualalisha chakula chochote ...kama unatumia akili utagundua hekima iliyo nyuma ya yale maneno ya yesu kuwa kimwingiacho mtu akiwezi kumtia unajisi bali kimtokacho nafsini ...hapa pana siri kubwa sana maana ya yesu ni kwamba hata ukila ugali na maharage unaweza kuwa najisi ikiwa moyoni mwako kumeshuhudia uovu mfano ukila kwa ulafi ...ukila kwa choyo...ukila kwa kumuasi mungu hapo dhamili yako ndiyo ikutiayo dhambi ...hivyo ukisoma kwa kutumia akili utagundua Yesu akuhalalisha kula nguruwe au kutokumla
 
Walawi 11:7-8 Na NGURUWE kwasababu anazo kwato,ni mwenye miguu iliyopasuka kati,lakini hacheui,yeye ni najisi kwenu.Msile nyama yao wala msiguse mizoga yao.
Kuna mambo kadhaa yaliyoandikwa katika Agano la Kale ambayo Yesu mwenyewe ameya-ammend katika Agano Jipya.

Kwa mfano, Agano la Kale mtu akikupiga na wewe ulikuwa unaruhusiwa kumchapa. Kutoka 21:24 (SRUV) jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu

Katika Agano Jipya Yesu ame-ammend sheria hiyo. Sasa hivi ukipigwa, huruhusiwi kujibu mapigo; badala yake Yesu anasema katika Mathayo 5:38-39 SRUV
Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino; Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili.

Kwahiyo ni kweli ilikatazwa kula nguruwe wakati wa Agano la Kale. Lakini Yesu alipokuja ali-ammend sheria hiyo. Sasa hivi nguruwe ni ruksa kuitafuna. Ila marufuku kuishushia na pombe.
 
...kama unatumia akili utagundua hekima iliyo nyuma ya yale maneno ya yesu kuwa kimwingiacho mtu akiwezi kumtia unajisi bali kimtokacho nafsini ...
Wewe umesoma Andiko hilo moja tu ukaishia hapo. Na hili je:
1 Timotheo 4:4-5
Kwa sababu kila kilichoumbwa na Mungu ni chema, wala hakuna cha kukataliwa...
 
Wewe umesoma Andiko hilo moja tu ukaishia hapo. Na hili je:
1 Timotheo 4:4-5
Kwa sababu kila kilichoumbwa na Mungu ni chema, wala hakuna cha kukataliwa...
Yote hayo yana thibitisha ninacho sema....sema wewe ujaelewa tu...sasa wacha nikupe akili ...turudi hadi bustani ya aden aliyo kuwako Adam na Eva nenda kajifunze pale ndiyo utagundua hekima ya hayo maneno ya yesu...maana pale pia kuna kisa cha kula tunda ...sasa tumia akili yako vizuri.
 
Back
Top Bottom