Mnaokwenda kwenye makanisa ya manabii, mitume, shida zenu huwa haziishi?

Mnaokwenda kwenye makanisa ya manabii, mitume, shida zenu huwa haziishi?

raslimali

JF-Expert Member
Joined
Nov 4, 2014
Posts
1,958
Reaction score
1,744
Huwa kweli nacheka sana nikiwasikiliza hawa manabii, mitume siJui maaskofu wanapowaingiza watu mkenge kuwachukulia pesa zao. Utasikia kama kiPindi hiki cha mwisho wa mwaka unaambiwa kutakuwa na ibada maalumu ya kufungua malango ya mwaka mpya.

Kumbuka wakati huohuo mwezi uliopita alikuja mhubiri huyo huyo kukutangazia ibada maalumu ya kufungua mafanikio yako maishani. Miezi miwilili iliyopita alikuja mhubiri kuKutangazia kutoa sadaka maalumu ya kufungua mafanikio ya kiuchumi. Jana usiku redioni umetangaziwa ibada inayoendana na saka (fedha!) ya kuharibu adui anayekula uchumi wako. Wiki iliyopita umetangaziwa kongamano la kuharibu laana za ukoo.

Mwaka jana uliitwa kwenye sadaka maalumu ya kuharibu laana ya ardhi. Sina muda wa kutaja haya makorokoro yote maana ni mengi mwenye kuongeza aongeze. Huwa najiuliza, HIVI HAWA WAUMINI SHIDA ZAO HUWA HAZIISHI WANAPOFIKA KWA HAO WAHUBIRI?? Maana kila siku wanaletewa topic mpya. Ni kama jana nimejifunza set theory kwenye hisabati lakini kwa sababu hisabati ina mambo mengi leo mwalimu amekuja na differential calculus.

Lakini wakati nipo darasani najua hisabati siyo set theory peke yake kuna topic nyingi. Lakini hawa wahubiri feki huwafanya waumii wao waamini kwamba siku hiyo waliyoipanga wenyewe kimchongo ili kuchota pesa ndiyo siku muumini anapewa kila kitu. Halafu kesho mhubiri yuleyule anabuni topic nyingine kukurudisha tena ale pesa zako.

Huwa njiuliza, SERIKALI ITAKAA MPAKA LINI KUWAACHA HAWA WEZI WANAOJIFICHA KWENYE KICHAKA CHA DINI KUWAIBIA WATU MCHANA KWEUPE WAKIAMINI MKONO WA SERIKALI HAUWEZI KUWAGUSA?????
 
Huwa kweli nacheka sana nikiwasikiliza hawa manabii, mitume siJui maaskofu wanapowaingiza watu mkenge kuwachukulia pesa zao. Utasikia kama kiPindi hiki cha mwisho wa mwaka unaambiwa kutakuwa na ibada maalumu ya kufungua malango ya mwaka mpya. Kumbuka wakati huohuo mwezi uliopita alikuja mhubiri huyo huyo kukutangazia ibada maalumu ya ANAOJIFICHA KWENYE KICHAKA CHA DINI KUWAIBIA WATU MCHANA KWEUPE WAKIAMINI MKONO WA SERIKALI HAUWEZI KUWAGUSA?????
Ukristo ni dini ya upigaji tu
Kila mtu atumie ujanja wake kupata riziki yke ndo ilivyo iyo dini yenu kwasababu sio dini ya Mungu ni dini iloasisiwa kiupigaji zaidi


Wajinga ndio waliwao
 
Mimi naona ungewacha tu kwa sababu zinazoliwa ni hela zao na sio za kwako, kuanzia lini serikali ikampangia mtu matumizi ya pesa zake? Wapo wanaoenda Kwa waganga wanaliwa vile vile, wengine wanaliwa Kila siku kwenye M-bet, mkeka bet tena huko wanaliwa nyingi sijaona ukiiomba serikali iingilie huko, wengine si juzi juzi wameliwa kizembe na Kalyinda au umesahau?? Kama hauliwi wewe kwanin uumie?
 
Ukristo ni dini ya upigaji tu
Kila mtu atumie ujanja wake kupata riziki yke ndo ilivyo iyo dini yenu kwasababu sio dini ya Mungu ni dini iloasisiwa kiupigaji zaidi


Wajinga ndio waliwao
Kila mtu Ana haki ya kuamini kile anachoamini na huwezi kumbadili!!Sio Lazima wote waamini unachoamini wewe ndio ubinadamu huo!!!Afu huku kwetu Africa mashariki hizo (Imani) namaanisha dini zililetwa na waarabu na wazungu na babu zetu walipokea na kila moja alivutia upande wake kwa kuiita imani yake dini ya haki!!!!!So waache tu hao watu na imani yao wana haki pia na nyote mpo sahii mbele za Mungu na mna haki sawa kiimani sababu wote viumbe wake!!!!
 
Ni heri kuibiwa wenzako wakiwa wanajua unaibiwa lkn kwa ujinga wako ukawa huambiliki au kuibiwa ukiwa hujui Kama unaibiwa kabisa ata wenzako pia hawajui Kama wanaibiwa pia????
 
Kwakweli ni upigaji sana alaf ukiangalia maisha ya hawa manabii wanavojiita ni matajir kupindukia,angalia kondoo ss.
Hvi ni kukosa elimu au?Serikali iingilie ksti wananchi wanaliwa sana pesa zao
 
Jana usiku redioni umetangaziwa ibada inayoendana na saka (fedha!) ya kuharibu adui anayekula uchumi wako. Wiki iliyopita umetangaziwa kongamano la kuharibu laana za ukoo. Mwaka jana uliitwa kwenye sadaka maalumu ya kuharibu laana ya ardhi. Sina muda wa kutaja haya makorokoro yote maana ni mengi mwenye kuongeza aongeze
Lawama zianzie kwenye mfumo wetu wa elimu, ndiyo chanzo cha hayo yote
 
Kagame tu ndo aliwaweza, sisi huku tunachukulia poa tu.
 
Kama wahusika awajalalamika na maadamu mitume na manabii awajavunja sheria za nchi sio kosa.
Mbona kwa waganga tunajazana na still shida zipo pale pale.
To be honest kwa waganga hawatapeliwi kwa wingi kama kwa manabii wa mchongo.. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
To be honest kwa waganga hawatapeliwi kwa wingi kama kwa manabii wa mchongo.. [emoji23][emoji23][emoji23]
Huwa wanaanza kupigwa kwa waganga kwanza ndipo ukimbilia kwa waganga wa makanisani
 
Hakuna watu wajinga kama hawa walokole. Wapo tayari kumpa sijui mchungaji ama nabii maisha ya kipato chao chote kuliko kumpa mungu wa uhalisia. Utasikia baba hana gari, yanachanga. Gwajima, kuhani Mussa na Mwamposa ni zaidi ya majambazi.
Mimi siku naenda kufata pussy kwa mwamposa roho iliuma sana nilivyomuona mzee amechokaaa anabeba mimaji eti yamebarikiwa.. Dahh jamaa anaroho ngumu sana.. Ndo maana pamoja na kuua watu 20 Kwake haija muuma kabisa yani
 
Huwa kweli nacheka sana nikiwasikiliza hawa manabii, mitume siJui maaskofu wanapowaingiza watu mkenge kuwachukulia pesa zao. Utasikia kama kiPindi hiki cha mwisho wa mwaka unaambiwa kutakuwa na ibada maalumu ya kufungua malango ya mwaka mpya.
Nyinyi mnaobeti mbona mpaka mnauza vitu vya nyumbani..watoto wanakosa mahitaji lakini hawawasemi...

Vumilianeni tu.. wote mmeshatekwa na pepo la umasikini na ujinga..
 
Hakuna watu wajinga kama hawa walokole. Wapo tayari kumpa sijui mchungaji ama nabii maisha ya kipato chao chote kuliko kumpa mungu wa uhalisia. Utasikia baba hana gari, yanachanga. Gwajima, kuhani Mussa na Mwamposa ni zaidi ya majambazi.
Unaweza kua sahii katika yote ila neno""YANACHANGA""Hapo mdogo wangu umekosea!!!Afu Sana uhuru wa kufanya wanayotaka sababu imani ni hiyari!!Mungu wa uhalisia ni fikira za mtu binafsi na imani yake haijalishi hiyo mtu ni mlokole,muidslamu,muhindu,au mbudha au Ana dini za kiasili za kiafirika!!!Kila mtu kwa imani yake anaamini Mungu wake ndio wa uhalisia na haki ya kusema hivyo sababu ameamini au kuaminishwa hivyo!!!Hata hao walokole wanaona watu wa imani nyingine kama wewe wajinga na Mungu wao sio wa asilia kama wewe unavyowaona mdogo wangu!!!!Huo ndio uhuru wa maisha kwa binadamu anaishi kwa kile anachokiamini
 
Back
Top Bottom