Mnaokwenda kwenye makanisa ya manabii, mitume, shida zenu huwa haziishi?

Nchi imejaa mafala hii
Kuna mijamaa na mishangazi inaamini katika miujiza[emoji23][emoji23]
 
Hakuna watu wajinga kama hawa walokole. Wapo tayari kumpa sijui mchungaji ama nabii maisha ya kipato chao chote kuliko kumpa mungu wa uhalisia. Utasikia baba hana gari, yanachanga. Gwajima, kuhani Mussa na Mwamposa ni zaidi ya majambazi.
Wamepora wapi
 
Hatuwezi kua sawa mna wengine wanamfanyia Mungu hali ya kua Mungu katakasika na hayo mambo
 
Ukienda Ukatoliki, Anglican, sabbato, kote huko wanasali kila week na wanatoa sadaka na mahubili yao hayana mwisho. Cha Jana kitarudiwa Mara elfu. Na watu wanatoa tuu. So shida IPO wapi kwa madabii na wengine wakifanya hivo?
 
Mkuu
Waache waende.
Wakigundua ukweli watachukua hatua binafsi yao
 
Mimi Ibadani kwa kweli sipendelei kwenda Ila napenda zile nyimbo za kusifu na kuabudu aaah hapo umenikamata mkuu, ooee wachungaji nyie mahuburi yenu bakini nayo wenyewe Ila nyimbo nzuri waimbaji watunge tufarijike na haya maisha, maana hata Mbinguni malaika wanamwimbia Mungu nyimbo za sifa
 
Kwakweli ni upigaji sana alaf ukiangalia maisha ya hawa manabii wanavojiita ni matajir kupindukia,angalia kondoo ss.
Hvi ni kukosa elimu au?Serikali iingilie ksti wananchi wanaliwa sana pesa zao
Dini hushamili zaidi katika jamii za watu masikini,umasikini na ujinga ndio mtaji wa watawala na baadhi ya wachungaji, mitume na manabii. Tunatafuta faraja ya matatizo yetu na shortcut za mafanikio .Watu wangu wanaangamia Kwa kukosa maarifa
 
Mkuu tuu kapigwa kule Nyerere na Mabehewa, Sembuse huyu pangu pakavu anaeyeonewa mpaka na Nzi,

Acha wakatafute faraja, ni mbaya sana ukiwa na majonzi halafu hata faraja ya uongo huna..

Ila bora hawa, juzi kuna Shehe kakimbia na kilo 300 Za mchele wa maulidi, Mbele ya Cha mtume, Jamaa sijui alisomewa nini, alikutwa Barabarani kasimama nao, Wakamla mapanga, watu wakaenda kupika.. bora hawa wanatumia akili, kuliko huyu mwizi.
 
Waache hao manabii waendelee kuwapumbaza hao wajinga... wanaisaidia sana serikali. Unadhani hao wajinga wote wanaojazana kwa kina Mwamposa na manabii feki wengine wakasema waache ujinga waanze kutumia akili kutatawalika? Itakuwa ni balaa.... acha manabii feki waendelee kuwatuliza hao umati wa wajinga.
 
Shida zao ni raha kwa hao manabii unategemea ziishe?
 
Nyinyi mnaobeti mbona mpaka mnauza vitu vya nyumbani..watoto wanakosa mahitaji lakini hawawasemi...

Vumilianeni tu.. wote mmeshatekwa na pepo la umasikini na ujinga..
🤣🤣🤣matatizo ni mengi sana nchi hii
 
Sio makanisa yote kilokole Ni mabaya,Ila gaya ya mafuta mfano hasa ya mwamp ukipona kwao jiandae kufa kwa janga lingine ,Mimi Ni mlokole ila miujiza ya mafuta Ni hatari kuliko mnavyodhani kupona unaweza kupona Ila huchukui muda ujapatwa na kubwa kuliko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…