Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 21,470
- 40,593
Kuna watu ambao kwa bahati mbaya wengine ni wanachama waandamizi wa CHADEMA, wanabeza msimamo wa Lissu wa kusimamia maamuzi ya vikao vya chama kuwa "No reforms No election" kuwa ni jambo lisilowezekana.
Lakini Klabu ya Simba kwa kusimamia Kanuni za ligi ya Tanganyika, imefanikiwa kugomea mchezo wake na Yanga hadi bodi ya ligi hiyo kuamua kuahirisha mechi husika.
CHADEMA wamechoka kutekwa, kuuawa, kuzuiwa kufanya siasa, chaguzi kuvurugwa na kura kuibiwa kufunguliwa kesi bandia, na hivyo kuamua kuwa kama hakuna mabadiliko hakuna uchaguzi Tanzania.
Kama Simba wameweza kwa nini CHADEMA ishindwe kuwaongoza watanzania kulazimisha kuwa kama hakutakuwa na mabadiliko basi hakutakuwa na uchaguzi?
Together Stronger 💪