Kuikomboa kutokana na nini? Yeye aliamini maendeleo ni kujenga nchi tu,Yaani miundombinu na wala hakudeal na maendeleo ya watu! Katika kipindi chake tumeshuhudia Maovu mengi sana kama watu kubambikiwa kesi, alisitisha ajira zote na kutokupandisha madaraja watumishi,lakini kubwa na baya zaidi Kuna wengine walishushwa madaraja!!! Katika kipindi chake watu waliuwawa,kukiukwa kwa misingi ya haki na Sheria. Ule mpango wake wa plea Bergain uliwahumiza sana watu,kiasi kwamba huyu mama mwenyewe aliona ni ukatili na Sasa ameanza kufuatilia waliodhulumiwa. Kwa mujibu wa Erick Kabendera na tetesi mbalimbali inasemekana kuwa Kuna watu walikuwa wanaporwa pesa waziwazi..!! Imagine..!! JIWE alikuwa Dikteta,Itoshe tu kusema hivyo.. Heri mungu alivyoingilia Kati .